Wasalaam Mkuu.
Kwanza, unapaswa kujua vigezo vya kusoma kozi husika kwa mwaka aliochaguliwa kusoma. Mara nyingi kozi ya Uhasibu wanahitaji uwe na D nne, sijafahamu kama ni LAZIMA moja iwe ya Mathematics.
Lakini, tambua kuna kozi ya awali kwa walioshindwa kufikia maksi fulani. Atasoma hiyo kozi kisha baadae atatahiniwa, na endapo atafaulu basi ruksa kuendelea na Cheti na baadae Diploma.
Je, umejiridhisha na hayo?
Pili, janga la kujua kuzungumza Kiingereza ni la Watanzania wote. Wapo mpaka wenye PhD, lakini bado lugha hiyo inawapiga chenga sana. Alishawahi kuwepo Mkuu mmoja, Kingereza kilikuwa chenga.
Unapaswa kujua kuwa, kutokujua kuzungumza lugha fulani si kosa kisheria.
Tatu, Wahasibu hawahitaji sana lugha katika kutekeleza majukumu yao. Kwao, namba ndizo za muhimu.
Lakini pia, mifumo ndiyo inachakata taarifa nyingi sana za kihasibu.
Katika kada ambazo kazi zake zipo katika hatihati ya kumezwa na teknolojia, basi ni Uhasibu. Mambo mengi sana kwa sasa yatekelezwa kwenye mfumo. Kama mhusika anaimudu katika kutekeleza kazi yake, basi hewala.
Nne, huwezi kumshtaki mhusika na chuo. Kwa miaka ile, wanafunzi walipata nafasi kwa kuomba kupitia NACTE. Kisha wao wataona kama anakidhi vigezo, kisha atapangiwa chuo.
Kwa hiyo sasa, utapaswa kwenda chuo husika ukiomba chuo hicho wamfutie cheti chake. Na kuona kama kuna uzembe ulifanyika wakati wa kuchaguliwa kwake. Kama upo, basi utawashtaki NACTE pamoja na Chuo husika. Na endapo mhusika alitumia njia za uongo kuwashawishi NACTE wamkubali, basi naye atashtakiwa.
Tano, mtaarifu mhusika kuwa una nia ya kumshtaki. Ili naye akakuloge vizuri. Mapumbu yake puani.
Haiwezekani kitendo cha kujuana na mhusika, unataka kumfanyia mambo ya kipumbavu.
Hoja yako ingejikita katika kusema madhaifu yake katika utendaji.
Hizi tunaziita husda. Kama unataka nafasi ya mwenzako, pambana kufanya kazi kwa bidii. Nafasi itakufata tu.