Kumshitaki mhitimu

Kumshitaki mhitimu

Good morning wapendwa,,,
Naombeni msaada wa kisheria katika Hili. Kuna mtu nimekutana nae na kufahamiana nae. Elimu yake ni ngazi ya diploma(uhasibu) lakini ufaulu wake KIDATO Cha nne ni daraja la nne pointi 28.

Matokeo haya yanajumuisha "F" ya hesabu. Pamoja na matokeo hayo, Bado hawezi kuzungumza na kuandika Kwa lugha ya kiingereza. Nimekuta na maswali mengi kuhusu ufaulu wake chuoni Hadi kupata cheti Cha diploma.

Ikiwa lugha ya kufundisha ni kiingereza na mitihani hutungwa Kwa lugha ya kiingereza, alifaulu Kwa miujiza gani? Nahitaji msaada wa kisheria, kama naweza kumshitaki yeye pamoja na chuo kilichomthibitisha kuhitimu Kwa ngazi hiyo.


Ukiwa na tabia hii utakufa maskini, na utaleta laana kwenye ukoo wako, achana na maisha ya watu.
 
Ukiwa na tabia hii utakufa maskini, na utaleta laana kwenye ukoo wako, achana na maisha ya watu.
Nikupe taarifa kwamba Mimi sio maskini. Tafuta utabiri mwingine wa namna nitakavyokufa. Jinga kabisa😂
 
Sina majungu ndugu yangu. Ulipaswa kutambua kwamba vijana wengi sana wanahangaika kupata ajira Kwa sababu hii. Kilichopo kwenye vyeti hakiakisi uwezo wao wa kufanya Kwa vitendo na kufikiri. Na wengine Wana ufaulu mbovu kabisa Toka awali lakini wamepenya na kumaliza elimu za vyuo vya kati. Pamoja na haya, Bado uwezo wao ni mdogo sana. Wivu wangu uko wapi? Umbea upi nimefanya hapa? Sina maisha ya wivu kabisa Kwa mtu mwingine. Namshukuru Mungu nilipo na ninavyoishi. Tujenge Hoja za kuwasaidia hata watoto wetu Kwa baadae. Akipatikana mtu Leo, akapambania Hili jambo, vyuo vitakiwa makini kutoa wahitimu Bora na washindani. Tusichangie Kwa mihemko TU Kwa kuwa eti tunawafaham wengi wa namna hii. Vipi kuhusu kesho? Bado watu wataajiriwa Kwa misingi ya kujuana? Vipi angekuwa ni mwanao, mdogo wako au rafiki yako? Ateseke na maisha na amesoma na kumbe tatizo lipo kwenye njia yake ya elimu? Tufikirie Hilo na Mungu awabariki.
Mkuu,kwa hili upo sahihi. Tatizo tu ni kauli uliyotumia ya mumshtaki. Wala si kwamba naunga mkono kufoji. Ni kwamba tu baada ya kuona mtu kaenda ndivyo sivyo,nahisi ana sababu zake. Kuna kumkanya,kumuelekeza au kumkosoa,ikishindikana ndo njia nyingine zinafata
 
Kuna mda unabidi utulie tu hamna namna! Hv kwa akili za kuwaza kushtaki graduate tutafika mahali? Badala tuwaze namna ya kuwasapoti wapate namna ya kugeuza elimu yao kua hela, namna ya kupata hela mtaani, jinsi ya kuepuka makundi hatarishi ya mtaani na mengine ambayo yatamjenga sisi tunawaza kumshtaki akwame kbs🤣🤣dah!
Niambie! Na ukiona mtu kalianika hapa,si kwamba amekulupuka,na haiwezi ikawa mara ya kwanza. Hawa wa hivi ni wale akimuona mke wa furani na kitenge kipya, anauza mtaa mzima kwamba ameona kilipoibiwa. Ini shoti,hawana kazi ya kufanya
 
Kama unajua kushtaki sana ebu mshitaki mbunge wako kwa kutokutimiza ahadi zake alizozisema kwenye kampeni
 
Niambie! Na ukiona mtu kalianika hapa,si kwamba amekulupuka,na haiwezi ikawa mara ya kwanza. Hawa wa hivi ni wale akimuona mke wa furani na kitenge kipya, anauza mtaa mzima kwamba ameona kilipoibiwa. Ini shoti,hawana kazi ya kufanya
Yaani unajua, nikisoma comments zako na huyu ndugu yako, nawaona Hadi mnavyofanana. Wapuuzi kabisa.! Mambo ya kanga yamefikaje hapa? Hao graduates umeshasaidia wangapi ndugu huko mtaani kwako uswahilini? Hebu tujenge Hoja.
 
Yaani unajua, nikisoma comments zako na huyu ndugu yako, nawaona Hadi mnavyofanana. Wapuuzi kabisa.! Mambo ya kanga yamefikaje hapa? Hao graduates umeshasaidia wangapi ndugu huko mtaani kwako uswahilini? Hebu tujenge Hoja.
Bro mi nimewasaidia direct na indirect wengi na naendelea kwa kidogo nlichojaliwa hua naumia sana graduate akidhalilika kwa kuonekana hana akili za kujiongeza kisa hana fursa, wengine nimewaunganisha sehemu wenye ukwamo wa kifedha kama ninayo natoa. Sasa wewe rafiki yangu unawaza kushtaki muhitimu? Kweli? Toa unaomba msaada kbs
 
Back
Top Bottom