Kumtambulisha Nusrat Hanje kama mwakilishi wa BAVICHA huko Nyamagana ni uongo wa wazi na ni kumdanganya Rais Samia

Kumtambulisha Nusrat Hanje kama mwakilishi wa BAVICHA huko Nyamagana ni uongo wa wazi na ni kumdanganya Rais Samia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kumtambulisha Nusrat Hanje kama kiongozi wa Bavicha, na kwamba ule ndio uwakilishi wa vijana wa Chadema kwenye Mkutano wa Rais na Vijana huko Nyamagana Mwanza ni kumpiga changa la macho Mh Rais .BAVICHA haikuhudhuria mkutano huo na wala haikutuma mwakilishi yeyote.

Nusrat Hanje na wenzake 18 walishafukuzwa kwenye uongozi na kuvuliwa uanachama wa Chadema kwa tuhuma za USALITI, hawa wote kwa ujumla wao hawana uwezo wa kuwakilisha chadema kwenye jambo lolote.

Aliyetangaza jambo hili la uongo alilenga kumdanganya Rais ili ionekane Mkutano ule wa vijana wa CCM na Mwenyekiti wa chama chao ni mkutano wa vijana wote wa Tanzania, wakati si kweli. Napendekeza muongo huyo atumbuliwe haraka ili kunusuru mambo yasiharibike zaidi, ikiwa na ugeni wake Mwanza ameanza na uongo duni kama huu, itakuwaje akiachwa hapo mwaka mzima?

 
Walipoambiwa

Samia = Magufuli
hawakuelewa? Unyumbu wao umewaponza
 
Katambulishwa na nani, mbona mimi nimeona kajitambulisha mwenyewe pale
 
Back
Top Bottom