Kumtamkia mzazi wako nakupenda kimaadili ya Kitanzania ni utovu wa nidhamu

Kumtamkia mzazi wako nakupenda kimaadili ya Kitanzania ni utovu wa nidhamu

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,498
Reaction score
4,162
Habari wakuu,

Tangu awali nilishasea huu uzungu na haya maisha ya watoto wa kishua sijui wanampango gani na vizazi vyetu,

Siku moja kuna star mmoja na mchekeshaji maarufu alifiwa na mama yake mzazi sasa jamaa alishinda akipost video alivyokuwa anaishi na mama yake mara wabusiane mara wakumbatiane mara walishane yaani hadi nilikuwa nikitazama zile video binafsi moyo unalipuka kwa kweli kwa hili mimi nitabaki kuwa mshamba kama ushamba wenyewe ndio huo basi nipo tayari kuvishwa taji la ushamba.

Mimi binafsi nimekuwa katika mazingira ya kijijini sikuwahi kuona mtu mzima kijana akimpakata mama yake au akimkumbatia mama yake na kumbusu huu ni ujinga na kukosa heshima. Hawa watoto wa mboga saba sikui akili zao huwa ziko wapi, wao wanaamini kumpenda mzazi wako ni kumbeba kumbusu na kumkumbatia kumwambia nakupenda mama kweli?

Mimi binafsi kidume wa mkoani nililelewa na single mother alinisomesha kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu, Na hadi sasa mama yangu anajua ni kiasi gani namjali sipendi niskie hata akiwa na maumivu kidogo nipo tayari kufanya lolote ili mama yangu abaki kuwa salama, nikipata hata 100 nataman nitakachokula na yeye ale hichohicho. Namjali mama kuliko kitu chochote kile hapa duniani. viapumbele vyangu katika maisha ni mama yangu kwanza kisha wanafuata wanangu na anafuatia mke wangu, maana pasipo kuwa yy nisingekuwepo mimi hao watoto nisingepata wala mke.

Ila kwa upendo wote huo sijawahi kumtamkia mama NAKUPENDA, wala kumkukumbatia and never ever haitakaa itokee neno NAKUPENDA huwa likinijia kichwani Huwa nachukua NOTE ya elfu 10 au 20 nampa namwambia mama hii katoe sadaka kanisani, maana ninajua mama yangu addiction yake ni kanisa tu hana mambo mengine,

Cha ajabu hawa watoto waliokulia mboga saba wanawakumbatia mama zao na kuwakiss eti ndio upendo, SHUBAMIT siwezi kufanya huo ukafili mama ni mama lazima mipaka iwepo.
 
Baada ya kuoa mke ndio anakuwa namba moja wakifuata na watoto,izo akili za kumweka mama namba moja ni za kitoto
mama siku akiwa hayupo hana replacement, mke ndoa huvunjika, mke mnatarakiana, mke akifa au akiondoka utaoa mwingine maisha yataenda huduma ya mke utaipata tu ila mama hana replacement akiondoka nafasi yake hakuna wa kuiziba kama unadhani mmeo anakujali kuliko mama yake au kama unamjali mkeo kuliko mama yako tegemea laana
 
Kumbe kimaadili Tanzania hatuna neno ^upendo^ wala hata hisia za upendo!??? Au ndiyo wale mkitaka kuonesha upendo ni mwendo wa kupiga na kujeruhi!???
mkuu kasome vzuri uzi wangu mkuu hisia zipo ila sio kumkumbatia mma yako kumbushu still iwill stand in my side kitu hiko sio sahihi na siungi mlono fullstop
 
Acheni ungese kwani ukimkumbatia na kumpiga busu mama yako mnakuwa tayari mmeshatomb@n@?
Acheni mawazo ya kimasikini.
Siku mama yako akifa utatamani hata uende ukamkumbatie mbuzi na umpige busu.
Onesha upendo wako kwa namna unayoona inafaa kwako.
 
Hata kumwambia mume au mke nakupenda kiafrika Ni kosa

Waafrika tunaamini Love is not a word it is something you do

Ukimpenda mkeo au mmeo au yeyote sio kelele za ohhh honey oh my biscuit ,my chocolate na ujinga mwingine ohh I love you !!!.What do you do is more important than the word I love you na busu Kali la kunyonya midomo

Wazungu wanafiki wanapenda show off za mabarabarani kelele za I love you nyingiiiiii kutwa kuachana

Mswahili ukisikia anamwambia mkewe au Mume hadharani kuwa I love you muambiwa lazima ashtuke kuwa kwa Nini kaniambia Hivyo sio bure ana Jambo huyu au anataka kuniacha haoni nampenda kwa kumpikia vizuri nk au yeye anahisi kuwa Mimi naona hanipendi? kwa Nini aniambie Hivyo kwani Kuna lolote nilifanya au yeye kafanya ambalo imebidi atilie mkazo kuwa ananipenda?
 
Back
Top Bottom