Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,926
- 95,626
Ndani ya miaka 60 ya uhuru chama cha CCM kimeshindwa kutatua changamoto ndogo kabisa ya maji na umeme halafu wiki hii kuelekea siku ya uhuru 09/12/2021 Rais wa utawala wa kiraia kutoka chama hichohicho anatangazwa kwenye mabango barabarani na mitaani akiwa amevaa mavazi ya kijeshi kuhadhaa uma kuwa ni Rais imara kutoka chama imara.Naona aibu mimi.
Kutangaza picha za Rais kwenye mabango akiwa katika mavazi ya kijeshi,katika utawala wa kiraia ambao Rais aliyepo ameingia madarakani kwa mujibu wa katiba ya kiraia ni inferiority complex na haimfanyi kuwa Rais bora na kwa watu wenye akili zao ni mambo ya aibu haya.
Rais bora anapimwa kwa kutatua changamoto ngumungumu kwa muda mfupi na kwa usahihi wake na wala siyo kwa kujitangaza akiwa kwenye mavazi ya kijeshi.Ninyi CCM Mnahitaji PhD kujua mambo madogo kabisa kama haya?
Ingependeza sana katika mabango hayo yanayoitangaza siku ya uhuru wetu viwekwe vivutio vya utalii badala ya Rais wa utawala wa kiraia alievalia mavazi ya kijeshi.
Halafu ninyi CCM ambao mmeshindwa kutatua changamoto ndogo kabisa ya maji na umeme ndani ya miaka 60 ya uhuru nani aliwaeleza kuwa sherehe za uhuru ni ‘birthday’ ya kiongozi aliyepo madarakani?
Kuelekea 09/12/2021 barabara zimepambwa na picha za Rais, hatuadhimishi siku yake ya kuzaliwa, tambueni hilo.
Kama mlitaka mitaa ipendeze kwa picha, kuna waasisi wa taifa hili pamoja na wapigania uhuru wa Taifa hili,wekeni picha zao barabarani.