Kumtangaza Rais akiwa katika mavazi ya kijeshi katika utawala wa kiraia ni 'inferiority complex'

Hivi tulipata Uhuru kwa Mtutu wa Bunduki? Mbona CCM wanakosa ufahamu kabisa, au labda wanatishana wenyewe humo kwenye chama. Nani asiyefahamu kuwa Samia ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu? Kama wanapesa za kuchezea bora wangeweka zile picha za kihistoria wakati Mwingereza anatukabidhi Nchi.
 
Ingependeza sana katika mabango hayo yanayoitangaza siku ya uhuru wetu viwekwe vivutio vya utalii badala ya Rais wa utawala wa kiraia alievalia mavazi ya kijeshi.
kwani si tulishakubaliana rais nae ni kivutio sasa mapovu ya nini tena .. sawa basi tutamweka mbowe na lisu..
 
Sawa, sasa dawa yenu ni katiba mpya tu.
Wananchi ndio mamlaka ya mwisho ya kuamua uendeshaji wa nchi.

Kama wananchi ambao ndiyo wenye nchi wanataka katiba mpya ni nani wa kuzuia?
 
Kumbe tuna KATIBA pendekezwa ipo kabisa ambayo stage iliyokuwa imebakia ilikuwa ni kwenda kwa kwa wananchi kuipigia kura tu na kisha iwe tayari.

CCM mnaogopa nini? hebu ileteni tuipigie kura tumalize mchezo.
 
Machinery ya Serikali bado ni ya marehemu Magufuli. Government machinery ya Serikali ya Magufuli ilijengwa na watu wengi ambao ni primitive.

Ni watu wanaoamini kuwa kila kitu kinahitaji nguvu. Huku wakishindwa kutambua kuwa kitu adimu ni akili, nguvu, hata nyati anazo, na hazijawahi kumfanya nyati wa leo awe bora zaidi ya nyati wa karne iliyopita.
 
Mkuu, bado uko kwenye mavazi ya kijeshi tu?

Au ndiyo ile wenzetu wanasema 'the one who laughs last thinks slowly' 😂😂
Ukweli mchungu, unajichekesha kicheko hakiji, inakuja hasira, unatokwa mapovu.
Vumilia au mjibu kwa hoja : miaka60 ya utawala wa MaCCM maji na umeme tu vimewashinda .
Uimara wa kutesa, kupiga risasi kufunga jela na kuua wapinzani tu..?!
 
Yeye ndiye alionyesha chuki kwa demokrasia yetu.Halafu neno Mama lina heshima yake,koma kulitumia kwa watu wa hovyo kama huyu anaeonyesha chuki katika demokrasia yetuView attachment 2035428
Magu ndiye aliyeharibu hii nchi. Hata kuingamiza mifumo yote ya nchi. Angalia kwa mfano ishu ya separation of powers alivyoi paralyse! Kipindi cha kampeni Samia alikuwa bendera fuata upepo tu.


JESUS IS LORD!
 
Hiyo picha kajilazimisha mana awamu ya 5 ni bongo movie tu,hawana jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…