Kumuachisha mtoto kunyonya

Dorkan

Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
26
Reaction score
2
Habari wana jamvi, kwanza niombe radhi sababu sinahakika kama uzi huu wafaa uwe jukwaa hili.
Pili ,kiukweli naomba ushauri wenu ni njia ipi nitumie ili niweze kumuachisha mwanangu ziwa,anakaribia kutimiza miaka miwili lakini naona mpango wa kuacha yeye mwenyewe hana kabisa,kila kukicha ndivyo anavyozidi kupenda nyonyo zaidi.
Angalizo:- mazingira niliyopo hayaniruhusu kulala vitanda tofauti,au kumpa mtu mwengine alale naye!
Natanguliza shukrani
 
Weka plasta nyonyo zote,akilia mwambia donda hiiiyo ataogopa na kuacha sawia.
 
Kwa nini unataka aache kunyonya? Mnyonyeshe hadi afike miaka 3 ataacha mwenyewe. Halafu akitimiza miaka 2 aanze baby class. Mbona akiwa na homework nyonyo atasahau?
 
Wenzio tumenyonya hadi.unamuambia mama kesho nna mtihani wa hisabati, staki kunyonya nataka nithome kwandha. Muache mtoto bwana, kunyonya kunaongeza akili atii
nitajitahidi kwa hili,asante kwa ushauri,maana sina uzoefu wowote.
 
Mama yangu aliniambia kuwa enzi za utoto wangu alikuwa ananiwekea pilipili kimtindo flani mbaka ninapo acha.
 
Wenzio tumenyonya hadi.unamuambia mama kesho nna mtihani wa hisabati, staki kunyonya nataka nithome kwandha. Muache mtoto bwana, kunyonya kunaongeza akili atii

haa haa haa! Nmecheka kweli,wajua nmekua na muda mwingi sana nae niliacha kazi tangu nlipomzaa hadi leo ili nipate kuwa karibu nae nakumtake care mimi mwenyewe,nakubaliana nawe kuwa kunyonya ni vizuri kwa mtoto lakini nami pia nahitaji kuendelea kufanya mambo mengine ya kimaendeleo na sidhani kama kwa umri wake ni mbaya.
 


hapo kwenye red...heheheh au ni wa akiume? ameshaanza kupata feeling za asili. kwikwikwiiiii...usipopaka chrologuine haachi.
 
Mama yangu aliniambia kuwa enzi za utoto wangu alikuwa ananiwekea pilipili kimtindo flani mbaka ninapo acha.

asante,ila huyu wangu pili pili haogopi sijajua nikwanini!
 
Hehehe chezeiya wewe. Yaani maza akirudi unamuwahi na kigoda, afu unamletea na maji ya kunawa. Unamuambia kaa hapa, nawa mikono unitolee nono yangu! Kichwa kinapiga hesabu shaaa!

Seriously. Kwani huyo mtoto kakuzuia kufanya shughuli za kimaendeleo? Acha iwe natural. Kama una shughuli zako toka muache, akiskia njaa atakunywa maziwa ama chakula. Mambo ya kuwekeana shubiri na pilipili ni ukatili wa kizamani huo bwana!
 
Anza kumpunguzia muda wa kuvyonya taratibu kama unamnyonyesha mara saba basi mpunguzie taratibu mpaka itafikia mda unamnyonyesha usiku tu mwisho anaacha kabisa.usimwachishe ghafla anaweza kuugua na ww mwenyewe inaweza kukuletea homa!
 
Miaka inatosha kunyonyesha.Ikifika kipindi hiki,Mimi na mke huwa tunampeleka mtoto kwa bibi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…