Kumuachisha mtoto kunyonya


asante mpenzi kwa ushauri. Kuhusiana na swali ulilouliza situation iko complicated kidogo.
 
Anza kumpunguzia muda wa kuvyonya taratibu kama unamnyonyesha mara saba basi mpunguzie taratibu mpaka itafikia mda unamnyonyesha usiku tu mwisho anaacha kabisa.usimwachishe ghafla anaweza kuugua na ww mwenyewe inaweza kukuletea homa!

yah,nlianza kumuachisha kunyonya mchana tangu akiwa na mwaka unusu,tabu ni usiku tu
 

Wengine wakiona plasta mpenzi wanabandua ila akila mualovera ule si mchezo mara mbili tu atachaa
 
Wengine wakiona plasta mpenzi wanabandua ila akila mualovera ule si mchezo mara mbili tu atachaa

Plasta au pamba inahusu. Unamwambia dudu hii.

Halafu pia weka mbadala wa Nyonyo, kama maziwa ya pakti au ya mrija, yani awe anapata maziwa ya kuvuta kama akinyonya nyonyo.

Mimi mtt wa kwanza nlimfanyia hivyo, yani ilikua usiku akiamka kutaka kunyonya nampa kiboksi cha maziwa anavuta kwa mrija.

Wa pili nlimuekea pamba, na usiku nkawa nampa maziwa ananyonya kwa chupa.
 

ok,nimekupata vizuri sana,asante!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…