Kumuangalia Mayele akitupia kambani na kisha kuitetemesha Nchi na Le dance de Mayele

Kumuangalia Mayele akitupia kambani na kisha kuitetemesha Nchi na Le dance de Mayele

Mwambie GSM aache kuwapa vipesa vijana uone Mayele kama atafumga goli 10.

Kwa wapenzi wa kandanda ambao wanaelewa components za "Perfect Skriker" ni lazima watakubaliana na mimi kwamba Fiston Mayele ni bonge la straika ambaye dunia ya sasa inamuhitaji zaidi kuliko usingizi unavyozihitaji njozi.

Sio rahisi kupata straika wa aina ya Mayele. Mayele ni kama Brenda zitengenezwazo Kiev kule kwa mwamba Putin yaani hazichagui kitu cha kusaga zinasaga mpaka meno. Basi Mayele naye hachagui mpira wa kuweka kimiani. Za kichwa twende! Acrobatic kwake ni km Samaki na maji! Freekick anaweka simply tu km mama ntilie anavyobandika maharage jikoni! Mipira ya kupress kambani anapress tu! Magoli ya kukimbizana anakukimbiza mpk jasho la meno linakutoka na kamban anaweka. Huyu Mayele ameshindikana.

Dunian kuna starehe kubwa mbili ambazo waliooa huwa wanazipata kila siku Mayele anapokuwa uwanjani:-
1. Kumuangalia Mayele akitupia kambani na kisha kuitetemesha Nchi na Le dance de Mayele
2. Mama kitunao kule Nyumbani baada ya kumaliza kula na kisha kuanza KURA.

Pah Amadu de hunter[emoji871]
 
Ndo shida yenu madalali wampira na kwawachezaji inakuaje ujadili ujinga huu wezenu Simba Fc wanazidi kujibandikia historia katika soka la afrika nadunia kiviwango.
 
Aliyefanya kuwa anayefunga goli anakuwa na sifa kuliko.anaye assist ndiye aliyeharibu baadhi ya wachezaji kuikosesha timu uashindi au magoli mengi kwa ubinafsi na kutafuta sifa za kuonekana mchezaji bora

Kama mayele baadhi ya nafasi nyingi anazozipata na kupoteza angekuwa anatoa assist yanga ingekuwa na magoli mengi sana

Sasa kwa kuwa anayefunga ndio anasifiwa na yeye anataka ujiko wa kucheza stail yake kaman Ray masterio akikupiga kwenye mieleka lazima akamilishe na six one nine hivyo hivyo kwa mayele anapoteza nafasi nyingi za magoli kwa kulazimisha kufanga hata akiwa kwenye bad angle ili acheze hiyo stail yake
 
Back
Top Bottom