Jamaa alikuwa kamtongoza dada mwenye kazi kazi nzuri sana lakini bahati nzuri walikuwa hawajawahi kufanya chochote kimapenzi. Siku hiyo jamaa kamtoa mpenzi wake kwa dinner na kuruka majoka. Alishawahi kuulizia historia ya mdada hakuambiwa chochote kile ambacho kilimshtua. Kule kwenye kuruka majoka alikutana na marafiki zake wakamshtua aisee huyu dada ni aje? Jamaa akasema ndio shemeji yenu huyo ambaye tumeanza uhusiano naye hivi karibuni. Marafiki wakamwambia mbona tumewahi kusikia kaathirika na alikuwa na jamaa yake ambaye inasemekana ameshafariki. Jamaa ndio kushtuka na kuanza kumdodosa rafiki yake naye kudai hajui kama kaathirika ila ni kweli jamaa yake alifariki miezi ya karibuni. Njemba ikamuomba wakapime kama wote ni wazima, dada akamtolea nje.
Kesi kama hii je hutapenda kuijua mapema ili ujiepushe? Kama si marafiki huyu jamaa naye si ajabu baada ya muda mfupi angekuwa muathirika. Ndio unaweza kabisa kudanganywa lakini ni bora kuuliza udanganywe kuliko kutouliza chochote na baadaye kubaki unajilaumu.