Wanabodi,
Leo siku ya Machi 17 ndio siku Taifa tulipotangaziwa kifo cha Shujaa wetu JPM, hivyo katika kumkumbuka, na kumuenzi, mnaonaje tukijikumbusha baadhi ya mabandiko ambayo tulimshauri JPM na ushauri huo ukafanyiwa kazi, kwa kutaja Bandiko, ulishauri nini, na nini kilikuja kufanyika kwa ushauri huo, na jee kulisaidia JPM? Kulisaidia nini?
Kwa vile JPM alikuwa ni mbabe kwa kufanya baadhi ya mambo kibabe, hadi kutafsiriwa ni dikiteta, hivyo baadhi ya ushauri kwa JPM pia ulitolewa kibabe kwa kumpiga Spana za kutosha, ila tukubali tukatae, Spana za JF zilimsaidia sana JPM na kulisaidia taifa.
Kumuenzi JPM, naomba tujikumbushe baadhi ya mabandiko, tuliwahi kushauri nini kwa kuandika nini na kutoa ushauri wa nini kifanyike, na kufuatia ushauri huo, nini kilifanyika na jee kilimsaidia JPM?kilimsaidia kivipi?. Jee kililisaidia taifa?, kililisaidia kivipi?
- Naanza na bandiko hili la August 2014 kutangaza ujio wa JPM nikieleza kwanini ni JPM Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli bandiko hili liliwaandaa Watanzania kwa 2015 with what to expect kwa JPM, hivyo ilipokuja kutokea kweli, it was not a surprise.
- Elections 2015 - Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo, Vunja Kambi, Jisalimishe! kwa vile uteuzi wa Magufuli uliwaumiza watu ya kambi ya Lowassa, hapa niliwashauri wavunje kambi na kukubali matokeo.
- ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote!, Life Goes On!. baada tuu ya uchaguzi, bandiko hili lilisaidia sana kuwapooza watu.
- Kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi Mkuu wa 2015 nikapandisha bandiko hili Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! lilisaidia sana kuandaa watu kisaikolojia
- Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!, hapa tulimshauri kuifuta katiba na kutawala kwa kutumia presidential decrees. Hapa ni baada ya JPM kuifuta predicts ya Uhuru kwa tamko tuu la mdomo, Bandiko hili liliwaibua watendaji wa Ikulu wakaandaa a decree ikawa backdated na kutolewa 3 days later. Hivyo bandiko hili limeisaidia serikali.
- Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake! hapa nimetoa angalizo muhimu la karma kwa serikali yetu, na it's consequences
- Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote bandiko hili limesaidia kutujulisha Watanzania kuwa Rais wa JMT akiamua, anauwezo wa kufanya chochote regardless ya katiba, sheria, taratibu na kanuni. Rais wa JMT hapangi mishahara ya watumishi wa umma, na kwa majibu wa kanuni, mshahara ukiishapangwa na kulipwa kwa kipindi cha miezi 3 mfululizo, hauwezi kupunguzwa unaweza tuu kuongezwa!. Huyu jamaa aliweza kupunguza!. Mpaka leo sijui alitumia sheria gani, kanuni gani na taratibu gani kuipunguza mishahara, hivyo aliipunguza!. Bandiko hili japo halikusaidia kitu lakini limetujulisha kuwa rais wa JMT ana inherent powers to do anything!.
- Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? bandiko hili lilisaidia sana kujua uchaguzi Mkuu wa 2020 utakuwaje, hivyo matokeo ya uchaguzi wa 2020 hayakuwa a surprise.
L
Na mwisho kwa vile sasa Samia ndie Rais wetu, JF tunapaswa kuendelea kutimiza wajibu wetu kwa kumsaidia Samia, kwa vile JPM alikuwa ni rais mbabe vivyo hivyo ushauri ulitolewa kibabe, lakini Samia no Mtaratibu, mstaarabu, jee licha ya utaribu na ustaarabu, Mama Nate tumpige Spana kama za JPM? au twende naye taratibu kama alivyo, kwa Mama iwe ni kumkuna tuu, na tusimpare kama alivyo shauri mwenyewe, kuwa ukinikuna vizuri nitakukuna ila ukinipara, nitakuparua?
Mabandiko mengi ya kuwakumbuka marehemu huishia kwa RIP kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi kwavile wanakuwa hawajui marehemu yuko wapi,, lakini mimi kwa vile tayari nimeisha kulishwa JPM yuko wapi
Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani bado kuna haja ya kuendelea kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi huku tayari najua yuko peponi?.
Pumzika Magufuli Pumzika!, Tutakukumbuka Daima!
Paskali!