Kumuenzi Mwl Nyerere

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Je, inatosha kumuenzi Mwl Nyerere kwa kukimbiza Mwenge wa Uhuru tu? Hatuna mbadala wa Mwenge kama namna ya kumuenzi Mwl? Agenda ya Mwl iliishia kwenye uhuru tu? Wakati wa Magufuli, Chama kupitia Mwenezi taifa wake, kilimuenzi Mwl nje ya mipaka ya nchi kwa kwenda Beijing kufanya midahalo mikubwa ikishirikiana na CPC ambapo machapisho ya Mwl yalihuishwa na kufanya China kuvitafsiri kwenye lugha yao na kuanza kutumia mawazo ya Mwl katika kusaka maendeleo zaidi. Hivyo ni vyama je, kiserikali Mwl anaenziwa na Mwenge wa Uhuru tu? Midahalo inayofanyika locally ina impact gani? Je, tunaweza kupima matokeo ya midahalo hiyo ya ndani? Kigoda cha Mwl kimemuuzaje/kimemuenzije Mwl? Tunaweza kupima matokeo ya Kigoda hicho?



Taswira kwa hisani ya google.
 
Asante kutukumbusha.
Huwa tunamuenzi Mwalimu kwa kuzima mwenge
Leo siku ya Nyerere day katika kumdurusu Mwalimu Nyerere kuna maswali najiuliza Kumuenzi Baba wa Taifa:CCM, Serikali, Viongozi na Watanzania kwa Ujumla, Je Tunamuenzi Baba wa Taifa kwa Mawazo, Maneno na kwa Vitendo?, Tunamuishi?.
Nawatakia maadhimisho mema na mapumziko mema ya Nyerere Day.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…