Kumuona Kuhani Mussa wa Kimara kwa haraka ni Tshs Laki 2

Kumuona Kuhani Mussa wa Kimara kwa haraka ni Tshs Laki 2

Ukifika pale Temboni unataka kumuona Kuhani Mussa Richard, kuna dau kama ilivyo kwa manabii wengine ila jamaa kaongeza kitu kinaitwa FAST TRACK. Hiyo ukitoa haina foleni, ile unamaliza kuhesabu pesa tu huyu hapa anakufanyia maombi.

Ila msisahau kubeba pesa za kununulia vifaa vya kiroho ambayo pia vina grade zake. Kuna vya matokeo ya papo hapo, na vile vya gradually Yaani mdogo mdogo.
Mimi nampango wa kwenda kumuona soon , nitaleta mrejesho
 
Ukweli Mungu yupo kila pahali, hayo makanisa huwadanganya watu kuwa Mungu yupo kwa hayo makanisa tu 😂
Yaani pentecostal churches huwa wanajiona bora sana kuliko watu wengine wowote.

Ni kweli Kuna mambo mengi mazuri yapo kwao hasa upande wa maombi,semina za Neno la Mungu kwa wingi na uimbaji.
Lakini hiyo haimaanishi kwamba wao ni bora sana kuliko wenzao wote.

Huwa wanakuwa na kijiubaguzi Fulani hivi...halafu wao kwa wao hata hawapendani...
Huwezi mkuta kuhani Musa aende kwa Mwamposa,ama mchungaji huyu aende kwa huyu na wakati unakuta ni makanisa ya jirani tu...
Zaidi sana wanapigana vijembe.

Hapo sasa ndipo tulipowapiga gap,,,
Sisi wenzao Kuna umoja.
Unakuta wa CCT wote ni wamoja,,kuanzia KKKT,Anglican,Moravian ,AIC, nk.

Yaani kesho utakuta kwaya ya kkt inaenda Anglican kuhudumu,Hawa wanaenda huku
Kuna kusimikwa kwa Askofu wa Anglican,,huko utakuta mabishop wa KKt,moravian Anglican.
Yaani Kuna muingiliano.
......

Haters msije sema siwapendi walokole.
Mimi mwenyewe nasali pentecostal churches ila kanisa langu formal nililozaliwa na kukulia sijahama na huwa naenda...na ndiko huko Mungu alinitengeneza tangu utoto hadi nimekuwa mtu mzima wananiona leo nipo hivi .

Kuna vitu sikubaliani na pentecostal kama kwenda kutumbukizana kwenye maji....siji kufanya na kama wakianza kujihesabia haki kunilazimisha basi ndio siku ntakayoacha rasmi.
 
semina za Neno la Mungu kwa wingi na uimbaji.
Kama ni semina na uimbaji pamoja na maombezi mbona hata mwl Mwakasege anafanya hayo yote vizuri sana kuwazidi hata hao wapentekosti?

Umewahi kusikia Mwakasege akiponda wengine?

Wapentekosti wa leo ni mbumbumbu mno na ndio maana hujisifu.
 
Mwakaseghe semina zake ni mwaka hadi mwaka

Naongelea zile continuous za Kanisani.
Japo Mungu mwema sasahivi makanisa yetu kuna uamsho sana..asilimia kubwa tumepiga hatua sana.

Mimi nawaadmire wapentecoste namna wanavyojicommit kusali..ila kuna namna huwa wanaona kama bado wengine mmepotoka.
 
Shida ya Makanisa haya ya kiroho
Ukianza kusali ni kazi sana kujitoa.

Yaani utashikiliwa huko, hawataki uondoke...
Na ukiondoka utaonekana mbaya,umepotea,,,utaanza kusemwa.

Yaani huwa wanaona Mungu yupo huko tu!,na kwewye Makanisa yetu formal hayupo.
Ni kweli kabisa, nilitumia nguvu za ziada kumchomoa mwenzangu huko, so najua vizuri sana. Hata tabia zinabadilika kabisa
 
Ni kweli kabisa, nilitumia nguvu za ziada kumchomoa mwenzangu huko, so najua vizuri sana. Hata tabia zinabadilika kabisa
Umempikia vita mwenzio dhidi ya wenzie

Ungemuacha tu atoke taratibu.
 
Umempikia vita mwenzio dhidi ya wenzie

Ungemuacha tu atoke taratibu.
Ukishaona mwanamke anashindia kanisani siku nzima ya jumapili na siku kadhaa za wiki, hapo nyumba inaenda kusambaratika. Mtumishi anakuchukua, mnaenda kwenye ATM unatoa pesa unampa kama mkopo then harudishi. Na hizo pesa unampa mimi
 
Kushinda Kanisani siyo tatizo Mkuu.
Tunashinda huko kuwaombea.

Sadaka ni hiari ya mtu...ila Kuna watumishi kweli hawana aibu,,ni wanaokopa hadi basi .
Nashukuru Mungu sijakutana na makanjanja wa aina hii.

Ila michango hata makanisa yetu formal mbona ipo mingi tu
Hasa kama unajulikana sana kuwa unazo hela basi kila harambee unapewa kipaumbele.
 
samahani.. hivi huyo kuhani huwa anaongea na Mungu moja kwa moja?
 
Kwenye madhabahu ya Ngome ya Yesu kwa Kuhani Musa ndipo ndipo nilipomjua YESU aliyehai...

Mpaka sasa nina nguvu za Rohoni sababu ya madhabahu ya hiyo...

Mungu azidi kumbariki Kuhani Musa

Bwana YESU atukuzwe
ulifanikiwa kimaisha?
 
mchaga wapi na wapi akawa nabii sijui mtume, kweli miaka hii mmepigwa sana nasikia jamaa anajenga hekalu baabkubwa kuliko lile la wakatoliki , ila haya makanisa saccos Mungu aingilie kati tu maana mijitu inaonewa na kukamuliwa mno kama mazuzu
 
Kwenye madhabahu ya Ngome ya Yesu kwa Kuhani Musa ndipo ndipo nilipomjua YESU aliyehai...

Mpaka sasa nina nguvu za Rohoni sababu ya madhabahu ya hiyo...

Mungu azidi kumbariki Kuhani Musa

Bwana YESU atukuzwe
Mtafute Yesu hapo sipo ogopa sana mitume na manabii usiende huko
 
mchaga wapi na wapi akawa nabii sijui mtume, kweli miaka hii mmepigwa sana nasikia jamaa anajenga hekalu baabkubwa kuliko lile la wakatoliki , ila haya makanisa saccos Mungu aingilie kati tu maana mijitu inaonewa na kukamuliwa mno kama mazuzu
Sadaka ni ya kwanza tu
 
Back
Top Bottom