Kumuota mtu ambaye ameshafariki inakuwa na maana gani?

Kumuota mtu ambaye ameshafariki inakuwa na maana gani?

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
3,424
Reaction score
7,706
Mara Ninaporudi nyumbani nilipozaliwa huwa namuota sana marehemu mama yangu 🤔

Kwa namna anavyokuja ndotoni ni mtu mpole sana, mkimya,huniangalia na kutabasamu, mara nyingi huwa namuota yupo jikoni au chumbani kwake amepumzika, maana hawezi kufanya tena kazi ngumu, labda kupika tu pekee.
Mara nyingi huja kututembelea tukiwa family nzima au wanaukoo baadhi baadhi

Muda mwingine, ni kama hunionya vitu ambayo Ata sikumbuki,

👉Nawaza huenda ni kwasababu nikirudi nyumbani masaa Machache kabla sijalala kila siku huwa nachukua dk tano hadi Lisaa kumfikiria, alikuwa kama Nyerere na aina Ile ya watu ambao Ata wakifa Yan matendo yao unajikuta unayaishi Kila siku, au lazima utamtolea mfano unakumbuka fulani alifanya ABC wakati wa uhai wake.

Lakini pia, huwa nasoma vitabu vyake viwili alivyoacha ili kujichotea hekima na madini ,haswa nyakati za usku nikiwa nimetulia

👉Karibuni, wakuu kwa michango na mitazamo, Aidha ni physics ndo inafanya kazi au ni 😅ndio wafu hutembelea watu ndotoni
 
Akili hailali na mawazo yako mara nyingi ndio yanakuja kwenye ndoto, be it consciously au unconsciously.., kwahio its normal huwezi kuota an idea / kitu ambacho hujawahi kukifikiria au you can not grasp its identity / idea...
 
Kwann man unasema hvo
Ukishakuwa huna kazi za kufanya, ubongo unaanza kukumbuka hata mambo yasiyo ishi, mfano kuwakumbuka marehemu, ma - x, walimu wa shuleni hukoo. Lakini ukiwa bize sana, huwezi kukumbuka yote hayo sbb usiku unakuwa umechoka sana.
 
Akili hailali na mawazo yako mara nyingi ndio yanakuja kwenye ndoto, be it consciously au unconsciously.., kwahio its normal huwezi kuota an idea / kitu ambacho hujawahi kukifikiria au you can not grasp its identity / idea...
Uko vyema
 
Hakuna kitu napenda na kufurahia kama ninapo muota mama yangu... Huwa akinitokea ndotoni inakuwa ni furaha sana... Alikuwa mtu mwema sana, mwenye hekima na upendo wa hali ya juu... Aliweza kuficha siri za watu na kamwe sijawahi kumsikia akilalamika kumsema mtu kwa ubaya... Siku ya mazishi yake watu walitoka kila kona ya nchi kuja kumzika... Na kila mtu alikiri upendo wa ajabu aliokuwa nao mama yaani alikuwa kama malaika...
R.I.P mama best yangu kipenzi🕊️
 
Sometimes their angles follow you at night,ila kuna wkt mwingine wachawi wanavaa sura ya mtu unaemfahamu ili usiwajue wao either way soma sana dua aka maombi
 
Ni kitu inaitwa soul ties, au muunganiko wa nafsi, kutokana na bond mliyokuwa nayo nafsi zenu bado zinawasiliana. Kama huzipendi hizo ndoto fanya maombi ya kuvunja muunganiko kama unazipenda ziache.
 
Sometimes their angles follow you at night,ila kuna wkt mwingine wachawi wanavaa sura ya mtu unaemfahamu ili usiwajue wao either way soma sana dua aka maombi
But anakuja kwa upole sana in real life mama yangu alikuwa mkali sana sometimes huwa nikitoka kazini kama ni night shift nikilala. Mchana namuota pia
 
Back
Top Bottom