Kumuuza Chama ilikuwa ni kosa kubwa Simba

Pesa iliwekwa nzuri. Pia chama kule mshahara ni mzuri zaidi.
 
Hujui mpira nenda kakate vitunguu
 
Mlifungwa na Yanga na chama na Miquissone walikuwemo ila Yanga walikuwa wanapumulia mipira na mpira wa simba ulikuwa unaonekana kabisa jinsi wanavyocheza ila sio jana

Yaani unafungwa na mpira mwingi unapigiwa
Basi ushindi wetu msimu uliopita wanajua hakina Manara na Boss Mo!

Inawezekana kulikuwepo na njia zingine zilitumiwa kuweza kufanikisha ushindi na si uwezo wa wachezaji wetu.

Tukiangalia hao Luis na Chama timu walizopo sasa zinachechemea
 
Magoli aliyokosa Mugalu yangeingia kambani haya maumivu nisingeyasikia.

Ukweli kunapokuwa na mechi ya Simba na Yanga. Fighting spirit ya wachezaji wa Yanga inakuwa juu kuliko ya wachezaji wa Simba.

Kilichokuwa kinambeba Luis ni kwamba alikuwa anajitolea kupambana mwanzo mwisho, hii kitu haipo kwa hawa wote waliobaki. Hata Chama nae hakuwa anajitoa kwenye mechi zote. Kuna wakati alikuwa anatembea tu uwanjani
 
Chama mbona kacheza Kariakoo derbies nyingi tu, na game zilikua ngumu pia. Mechi kama zile muhimu ni mtu kuhakikisha unatumia nafasi unazopata. Jana nafasi za magoli tumetengeneza nzuri tu, ila Mugalu ndo hivyo tena, kazi kutafuna big G tu.
Kagere sio mzuri sana kuhold mipira, ila ni aina ya watu kwenye nafasi mbili tegemea moja kamba.
Nadhani ifikie hatua Gomez asijisahau sana kuona anaweza kujiamulia tu chochote hata kama kinatugharimu. Kulikua na sababu gani ya Kagere kutokuepo hata bench, bila maelezo yoyote yakueleweka? Jamaa ni wazi ana chuki binafsi na Kagere, lazima ifikie hatue mashabiki tupaze sauti kwa maslahi ya club. Tunaoteseka ni sisi mitaani
 
CHAMA alitaka kuondoka mwenyewe kutokana na masilahi yake tungemzuia vipi?
Na mshahara wake huo mpya wa milioni 80 ungelipa wewe???
Tuache ujuaji sana.
Ata mimi ningeondoka bila kuaga.
 
Hii ya kuteseka mitaani ni kweli jana nimeona wengi mkiteseka toka viunga tofauti tofauti [emoji23][emoji23], poleni sana mtani.
 
Yaani kuna maeneo yake ya 18 wachezaji wa simba walikuwa wanafanya maamuzi ya hovyo saana, yaani chama pale anakufinya na anakuja mwingine ana mfinya tena halafu anatoa killer pass Kwa Mugalu The Animal
Tatizo sisi mashabiki ni wepesi kusahau

Chama na mikson walikuwepo na tukafungwa na hawa yanga jul 3 hata march 8 tulifungwa na yanga

Chama na mik walikuwepo na tukapigwa 4 na kaizer

Bado ruvu kagera na prison

Sent from my V5+ using JamiiForums mobile app
 
Boss Mo alishaanza kufokeana na Chama na baadae akahamua amuuze, yote haya ni Boss Mo.
Mo anatuharibia Tim. Kama vip bas amuweke babra acheze uanjan maana maamuz yake yako kibiashara zaidi
 
Ujuaji mwingi sana kwa mashabiki wa bongo
 
Huyu chama ilifika kipindi game zetu na yanga tulianza hisi anafanya hujuma yeye na manara


Acha kabisa huyo mleta mada hajui na hatojua mpira kamwe
 
Tungeweza kumuuza Luis Miqueson, ila kumuuza CHAMA lilikuwa kosa kubwa hasa kwa timu iliyokuwa imeshaanza safari...

Acha ubinafsi Simba ni timu ndogo tu kwa wenye ndoto kubwa. Hebu kaa upende wa wewe ungekuwa ndugu wa Chama au Chama mwenyewe.

Kumbuka wachezaji wa timu za Tanzania wana mikataba mifupi, angeondoka mwakani bure ungeandika tena kuirahumu Simba.
 
Na mashabiki wa kibongo ninavyowajua, Gomez siku zake zinahesabika
 
Kwani Simba haijawai fungwa Yanga na Chama akiwemo?
 
Amwamedi alikuwa anataka hela zake aliyotoa bila maandishi.hakuna jinsi Simba Kama Simba tu dhoofu hali
 
Chama alilazimisha mwenyewe kuondoka baada ya kupata timu itakayomlipa mshahara na marupurupu ambayo Simba haiwezi kumlipa hata robo yake. Pamoja na hayo hatujui mkataba wake ulikuwa una vipengele gani ndani yake hasa ukizingatia yule ni mchezaji wa kimataifa ambaye yeye na meneja wake wanajua vitu vingi sana kuliko hawa wachezaji wetu wa ndani. Mwisho unaweza kumlazimisha mchezaji abaki kumalizia mkataba wake lakini madhara yake ni makubwa kuliko faida kwani ataanza mgomo baridi na huna la kumfanya mwisho wa siku anakuja kuondoka bure kabisa. Pia hiyo itawafanya wachezaji wazuri wenye malengo makubwa wasije kusajili kwenye timu Simba wakijua kuwa wakipata timu zinazolipa vizuri watabaniwa kuondoka.

Kwangu mimi kuondoka Chama sio tatizo bali tatizo ni benchi la ufundi jee lilifanya juhudi kuushawishi uongozi uwaletee mchezaji/wachezaji fulani kuziba nafasi yake? Au lilijipangaje kumuandaa au kumbadilishia majukumu mchezaji fulani ili kuziba nafasi ya Chama? Au lilijiandaje wakati wa "pre season" kubadilisha mifumo ya uchezaji uwanjani ili iendane na aina wachezaji waliopo sasa?

Kwa hiyo hapa mchawi sio Chama kuondoka bali ni benchi la ufundi basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…