Babu Kijiwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2010
- 4,830
- 4,729
Habari wanajamvi, Miaka ya hivi karibuni kameibuka kamtindo kakilimbukeni ka kumwagiana maji siku ya kuzaliwa. Mtindo huu umeigwa toka ng'ambo na kuletwa kwetu. (Si vibaya kuiga, lakini ni vizuri kuiga vitu vyenye tija) Unakuta mtu umevaa nguo za heshima upo ofisini anakuja mtu huko alipotoka na kukumwagia maji bila sababu za msingi kwa kigezo cha kukusababishia furaha katika siku yako ya kuzaliwa, kwa maoni yangu huo ni ulimbukeni uliopitiliza, hivi nikweli kwa jamii zetu kulikuwa na haja ya kuiga hili?
Nivema tuangalie mambo ya kuiga toka ng'ambo, haya mambo ya kuiga kila kitu ni ulimbukeni ndo maana wengine wameiga ushoga maana hawajajifunza kuiga mazuri.
Onyo: Atakaye thubutu kunimwagia maji siku ya kuzaliwa atachezea kipigo cha mbwa koko, nitamtoa meno ya mbele mpaka ashindwe kutamka neno ubwabwa, ukimwambia sema ubwabwa anasema wawaa.
@mods tafadhali usitoe