Kumwagiana maji siku za kuzaliwa ni ushamba wakisasa

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
4,830
Reaction score
4,729
Habari wanajamvi, Miaka ya hivi karibuni kameibuka kamtindo kakilimbukeni ka kumwagiana maji siku ya kuzaliwa. Mtindo huu umeigwa toka ng'ambo na kuletwa kwetu. (Si vibaya kuiga, lakini ni vizuri kuiga vitu vyenye tija) Unakuta mtu umevaa nguo za heshima upo ofisini anakuja mtu huko alipotoka na kukumwagia maji bila sababu za msingi kwa kigezo cha kukusababishia furaha katika siku yako ya kuzaliwa, kwa maoni yangu huo ni ulimbukeni uliopitiliza, hivi nikweli kwa jamii zetu kulikuwa na haja ya kuiga hili?

Nivema tuangalie mambo ya kuiga toka ng'ambo, haya mambo ya kuiga kila kitu ni ulimbukeni ndo maana wengine wameiga ushoga maana hawajajifunza kuiga mazuri.

Onyo: Atakaye thubutu kunimwagia maji siku ya kuzaliwa atachezea kipigo cha mbwa koko, nitamtoa meno ya mbele mpaka ashindwe kutamka neno ubwabwa, ukimwambia sema ubwabwa anasema wawaa.

@mods tafadhali usitoe
 
Hehehehe kwanza sina urafiki na kenge wa aina hiyo nina marafiki smart ambao hawana upuuzi huo na akija kutokea mmoja mwenye akili hizo atarudi nyumbani hana kitu kimoja katia ya hivi.

Nyonga au kiuno.
 
Si wajua tena watz ni watu wa kucopy na kupaste yani ukimpa chabo kwenye paper ana copy mpaka jina lako, mara wanasheherekea halloween, mara sijui nini mara kumwagiana maji mpaka matope....
Any way ngoja wawe huru ila mimi uwa sisheherekea siku yangu ya kuzaliwa na ikitokea nahisi nikamwagiwa maji patachimbika
 
😛😛😛😛 hawa hawajakutana na mtu aliyepinda
 
🤣🤣🤣mimi walinimwagia oil chafu niliokota gongo nilipiga aliye mbele yangu
 
Wanaomwagiana maji ukiwachunguza huwa na matatizo ya kisaikolojia na niwabishi hivyo usiwapige jitahidi kuwazuia tu usije ukafungwa
 
kuna raha yake kufanyiwa hivyo hasa hasa maji hayo yawe ya ukoko wa ugali
 
Wengine birthday zetu kuna kipindi zinapita hata hatujui.
 
Habari wanajamvi, Miaka ya hivi karibuni kameibuka kamtindo kakilimbukeni ka kumwagiana maji siku ya kuzaliwa. Mtindo huu umeigwa toka ng'ambo na kuletwa kwetu. (Si vibaya kuiga, lakini ni vizuri kuiga vitu vyenye tija) Unakuta mtu umevaa nguo za heshima upo ofisini anakuja mtu huko alipotoka na kukumwagia maji bila sababu za msingi kwa kigezo cha kukusababishia furaha katika siku yako ya kuzaliwa, kwa maoni yangu huo ni ulimbukeni uliopitiliza, hivi nikweli kwa jamii zetu kulikuwa na haja ya kuiga hili?

Nivema tuangalie mambo ya kuiga toka ng'ambo, haya mambo ya kuiga kila kitu ni ulimbukeni ndo maana wengine wameiga ushoga maana hawajajifunza kuiga mazuri.

Onyo: Atakaye thubutu kunimwagia maji siku ya kuzaliwa atachezea kipigo cha mbwa koko, nitamtoa meno ya mbele mpaka ashindwe kutamka neno ubwabwa, ukimwambia sema ubwabwa anasema wawaa.

@mods tafadhali usitoe
Kwa sasa kuiga ndio tatizo linalowaathiri wabongo wengi..ni kweli usemacho
 
IMG-20181112-WA0037.jpg
hepi besidei tu yu
 
Kwa sasa kuiga ndio tatizo linalowaathiri wabongo wengi..ni kweli usemacho
Kibaya zaidi hata maana ya wanavyoiga hawajui, mf mbongo anaweza ona mzungu kavaa nguo nyepesi na fupi kwasababu ya joto, mbongo wa mufindi (kwenye baridi kali) anaiga na kudhani ni fasheni
 
Back
Top Bottom