Kumwagwa Kwa Fedha za Ufisadi Majimboni: Wabunge "Wapambanaji" Acheni Siasa!

Buchanan,

Tatizo la sisi Watanzania wengi ni kushindwa kuwa na msimamo mmoja. Kosa ni kosa kwasababu linamhusu mbaya wako lakini kama liko kwa kipenzi basi huyo anaonewa.

Matokeo yake tutaendelea kuhamisha goal posts ili ku fit malengo yetu.

Kwa kila siku kupiga kelele za mafisadi hata pale pasipo na ufisadi wamefanya hilo neno libadilika kutoka kuwa kosa kubwa na kuwa kijembe cha kisiasa ambacho kila mmoja anaweza kutumia dhidi ya mwingine. Hata wale mafisadi wakubwa sasa wana raha maana sio wao tu wanaotajwa na badala yake malaki ya Watanzania wanaitwa mafisadi, wakiwemo wale ambao hawajawahi kuiba hata senti tano ya mtu.

Hao wanaolalamika majimboni kwamba pesa zinamwaga, wanajua ukweli wake na ndio maana hawako tayari hata kufuatilia. Wanachokifanya sio kutatua tatizo la ufisadi, bali kuwadanganya wananchi majukwaani.

Kuna mheshimiwa mmoja, anadai kwenye mikutano yake kwamba mafisadi wanamwaga pesa na kuwapa wajumbe, yeye mwenyewe akimaliza anawapa wajumbe hao hao pesa. Mtu unabaki kujiuliza, hivi wananchi wanafanywa wajinga kiasi hicho?

Watu wanataka maendeleo na sio kelele za majukwaani. Mpambano wa 2010 utakuwa juu ya nani ana vision nzuri ya kulisukuma jimbo mbele, ikiwa ni pamoja na kupambana na majanga mbalimbali pamoja na matumizi mabaya ya pesa za wananchi, na sio tu nani ana uwezo mkubwa wa kupiga kelele za mafisadi akiwa jukwaani.
 

Sure, umeongea pointi tupu ndugu Mtanzania. Mimi sipingi vita dhidi ya ufisadi, lakini kwa jinsi mambo yanavyoenda tumeanza kupoteza mwelekeo na matokeo yake tutawapatia mafisadi nafasi ya kupumua hasa pale tunaporopoka bila kuwa na ushahidi. Mafisadi wanawaangalia "wapambanaji" kwenye sight mirror tu!
Katika post ya ndugu Kibori inaonekaka, kwa maelezo yake, kuwa "wapambanaji" ni waoga, hawataki kuonekana wabaya! Kwa hiyo njia pekee ni kuropoka kwenye vyombo vya habari. Wameshindwa kujifunza kwa Dkt Slaa ambaye aliwataja mafisadi HADHARANI, jua limewaka kweupe! Kwa hiyo Dkt Slaa tuna uhakika na hoja zake, na tuna uhakika amemlenga nani. Vyombo vya dola vikishindwa kufanyia kazi hoja zake basi lawama zote tuzihamishie huko!
 

Sure!
 
Wadau, hoja zimekauka? Au bado mnatafakari?
 
leta ushahidi otherwise ni majungu na mambo ya mitaani tu haya

Mwenye macho haambiwi tazama. Na ndio tatizo la watu wenye mwelekeo wa kifisadi - daima watadai ushahidi, hata pale mambo yanapojionyesha wazi. Hata RA ambaye uhalifu wake wote anaufanya underground anathubutu kuwaambia Watanzania watoe ushahidi kama yeye ni fisadi. Eti fedha zake zinatokana na biashara za babu zake tangu enzi hizooo.. Ebo!
 
Mwenye macho haambiwi tazama. Na ndio tatizo la watu wenye mwelekeo wa kifisadi - daima watadai ushahidi.

Hivi tukisema MzeePunch ni FISADI bila ushahidi utakubali kuwa wewe MzeePunch ni fisadi? Wapambanaji wasi-take advantage kwa kuwa wananchi wamewaamini vya kutosha! Hawajafanya lolote majimboni mwao, wanajificha kwenye mwavuli wa kupambana na ufisadi! Wajibu maswali sita (6) yafuatayo:
1. Nani alimwaga fedha?
2. Alimwaga fedha kwa ajili ya nini?
3. Alimwaga lini?
4. Aliwamwagia akina nani?
5. Alimwaga shilingi ngapi?
6. Alimwaga wapi?

Hayo maswali yasipojibiwa tuwaamini tu kwamba wanasema kweli? Mbona Dkt Harrison G. Mwakyembe alipotuhumiwa pamoja na Kamati Teule wakati wa kufuatilia mambo ya Richmond kwamba walihongwa alidai wakati anasoma taarifa ya Kamati yake wapewe ushahidi nao watawajibika kisiasa? Kama ushahidi SIO MUHIMU tuamini kwamba akina Dkt Harrison G. Mwakyembe na Kamati yote teule walihongwa kweli? Na huyo Dkt Harrison G. Mwakyembe ambaye alidai ushahidi na yeye ana MWELEKEO WA KIFISADI?
 
Buchanan nakubali maneno yako.Watajwe hao watu hao wanaogawa Ma hela ya kifisadi.UTHIBITISHO KUWA MAPESA HAYO NI YA KIFISADI UNATAKIWA!!! kama watu wamekuwa madarakani kwa miaka zaidi ya 20 watakosa vijisenti vya kuwapa walala hoi?!
 
Buchanan nakubali maneno yako.Watajwe hao watu hao wanaogawa Ma hela ya kifisadi.UTHIBITISHO KUWA MAPESA HAYO NI YA KIFISADI UNATAKIWA!!! kama watu wamekuwa madarakani kwa miaka zaidi ya 20 watakosa vijisenti vya kuwapa walala hoi?!

Sure!
 
 
Mimi kama raia fedha nachukua bse uamuzi wa kumchagua nimpendae uko ndani yangu siku ya kupiga kura!Si wana mihera ya mchezo waipeleke Kilosa!
 

Hatudanganyiki yeyote anayegombea kupitia CCM lazima amawage mapesa. Angalia chaguzi zote kuanzia chekechea hadi ujumbe wa NEC watu ni kutoa mapesa tu. Hata wewe umeshakusanya yakutosha ambayo kama kweli niyako halali nakushauri usiyatumie.

Mmmmh, huko naona kama umefika mbali mkubwa!
Mali wapi si Sofia Simba alishasema kuwa ndani ya CCM hakuna msafi?

Nimekupa senkiyu kule kwenye kitufe lakini ngoja nirudie tena hapa. Hapo nipobold ndio penyewe. Tunahangaika na kizazi cha mafisadi.
 
cherehani 100 alizotaka kutoa January Makamba huko Bumburi, huo ni mfano

Good, now you are talking!
Umebakisha masuala yafuatayo:
1. Cherehani zilitolewa kwa akina nani? 2. Zilitolewa lini? 3. Zilitolewa kwa ajili ya nini? 4. Umetoa taarifa TAKUKURU?
 

Hapa ndugu Kibori ndipo inavyoonyesha jinsi ulivyopotea njia au huna uzalendo! Kutegemea kwamba TAKUKURU wadeal na watu karibu MILIONI 40 wakati wao ni minute ni number bila msaada wa wananchi kutoa taarifa labda kazi hiyo anaiweza malaika tu! Vyombo vingine vya dola km Polisi huchukua taarifa za wahalifu toka kwa Raia wema. Wanajeshi huwa nao wanapata taarifa za intelijensia toka kwa raia wema (JWTZ walimshinda Idi Amin kwa sababu ya ushirikiano mkubwa waliouonyesha wananchi wa Uganda), nk. Sasa unapodai eti wanachi wanapewa mzigo ulitaka mzigo huo waje waupewe akina nani? Nchi hii itajenjwa na kila mmoja, sio baadhi, wengine wakiwa watazamaji, kama kwenye mpira wa miguu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…