Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Hii mada niliikuta sehemu imezua mjadala mkali sana baina ya mtoto (mwanafunzi) na mama yake wakati wakifanya manunuzi ya stationery za kwenda shule Januari hii.
Mama anashikilia kwamba hela ni hatari kwa mtoto (hasa wa bweni) kwamba yeye mama enzi zake kama mwanafunzi hakupewa hela ambazo mtoto wake anadai apewe leo.
Mtoto anashikilia kwamba bila kupewa hela za kumtosha basi asitegemee atasoma masomo ya mchepuo wanaotaka wazazi wake wa ECA ili awe Mhasibu.
Mtoto anaamini kupewa hela za kukidhi matakwa yake siyo dhambi bali dhambi ni kupewa hela kidogo maana akipewa za kumtosha basi hata ukubwani atazitafuta kwa bidii maana atakuwa ameishafundishwa utamu wake.
Akipewa kidogo au kunyimwanyimwa basi ukubwani hatofanya bidii kutafuta hela maana atakuwa hajazizoea (ataziogopa kwamba ni hatari) na kwamba wazazi wake wasipokuja kupata hela toka kwake wasije kumlaumu.
Kumzoesha mtoto hela ni dhambi?
Nini ushauri wako kwa hii familia.
Taswira kwa hisani ya google.