Kun Aguero na Fernandinho wakumbana na rungu la FA

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Chama cha Soka nchini Uingereza FA wamethibitisha kuwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Sergio Kun Aguero amefungiwa michezo 4 kutokana na kadi nyekundu aliyoonesha katika mchezo wa timu yake dhidi ya vinara wa ligi kuu soka nchini Uingereza Chelsea Fc the Blues.

Sergio Kun Aguero amekumbana na kifungo hicho baada ya kumchezea rafu mbaya beki wa Chelsea Fc, David Luiz na kusababisha mtafaruku mkubwa uliosababisha mchezo kusimama kwa dakika kadhaa kutokana na wachezaji wa timu zote kuzoza.

Aidha mchezaji mwingine wa Manchester City Fernandinho nayeye amefungiwa michezo 3 kwa kosa alilofanya la kumsukuma Fabregas na kuoneshwa kadi nyekundu wakati wa mchezo huo.
 
Naionea huruma cty maana kwa adhabu hyo n kuiangusha tim hapo ndo gadiola ataanza kuona kuna umuhimu wa kumrudisha ture kikosn
 
Namuonea huruma sana fundi EL KUN, huu mwaka wake,very sad
 
Afadhali mechi na Arsenal hatakuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…