Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Chama cha Soka nchini Uingereza FA wamethibitisha kuwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Sergio Kun Aguero amefungiwa michezo 4 kutokana na kadi nyekundu aliyoonesha katika mchezo wa timu yake dhidi ya vinara wa ligi kuu soka nchini Uingereza Chelsea Fc the Blues.
Sergio Kun Aguero amekumbana na kifungo hicho baada ya kumchezea rafu mbaya beki wa Chelsea Fc, David Luiz na kusababisha mtafaruku mkubwa uliosababisha mchezo kusimama kwa dakika kadhaa kutokana na wachezaji wa timu zote kuzoza.
Aidha mchezaji mwingine wa Manchester City Fernandinho nayeye amefungiwa michezo 3 kwa kosa alilofanya la kumsukuma Fabregas na kuoneshwa kadi nyekundu wakati wa mchezo huo.