Kuna aina ngapi za pitch(viwanja ) za mpira wa miguu?

MONA WA KYEN

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2016
Posts
340
Reaction score
271
Wakuu namiini mnaendelea vema na shughuli zenu nimekukuwa mshabiki wa mpira lakini kiukweli bado sijaweza kufahamu vema kuna aina ngapi za pitch.

Kiukweli sijawahi kuona mimi binafsi mtu akifunga goli uwanja wa taifa ule mpya aka slide(kuteleza ) huku akishangilia nashindwa kuelewa kwa nini huku ninaona old trafford mtu akifunga anaslide bila matatizo na viwanja vingine vya ulaya darajani, emirate, benabeu, ethadi n.k

Je wanajamvi kuna aina ngapi za pitch?

Nilikuwa naangalia mpira siku moja ule uwanja wa chamazi mpira ukidunda unatoa mchanga kabisa hata shamba la bibi vilevile kaitaba sasa lakini ule mkuu wa taifa mpira ukidunda mchanga hata hauonekani ila watu hawaslide, nisaidieni aina za pitch tafadhali
 
Chamazi, shamba la bibi, karume na kaitaba ni nyasi bandia na vile vinavyoruka mpira ukidunda ni vipira vidogo vyeusi vinasaidia kushikilia nyasi..

Taifa ni nyasi asili but sio first class kama OT, BERNABEU, CAMP NOU na kwingineko
wow asante sana mkuu, kwa hiyo kuna tofauti kati ya nyasi bandia na asili? na kwa maana hiyo mkuu OT na wengine sio bandia?
 
wakuu namiini mnaendelea vema na shughuli zenu
nimekukuwa mshabiki wa mpira lakini kiukweli bado sijaweza kufahamu vema kuna aina ngapi za pitch.
kiukweli sijawahi kuona mimi binafsi mtu akifunga goli uwanja wa taifa ule mpya aka slide(kuteleza ) huku akishangilia nashindwa kuelewa kwa nini huku ninaona old trafford mtu akifunga anaslide bila matatizo na viwanja vingine vya ulaya darajani, emirate, benabeu, ethadi n.k
jee wanajamvi kuna aina ngapi za pitch?
nilikuwa naangalia mpira siku moja ule uwanja wa chamazi mpira ukidunda unatoa mchanga kabisa hata shamba la bibi vilevile kaitaba sasa lakini ule mkuu wa taifa mpira ukidunda mchanga hata hauonekani ila watu hawaslide, nisaidieni aina za pitch tafadhali

Kuna viwanja wa Asili kabisa ambavyo majani yanapandwa na kutunzwa, pili kuna viwanja vya nyasi Bandia ambazo ni aina fulani za plastic kwa hiyo zinatengenezwa kama carpet

Kwa viwanja vingi vya ulaya huwa ni nyasi asilia, lakini huwa hazipandwi hapo kiwanjani kunakuwa na kampuni zenye vitalu maalumu za kupanda na kutunza hizo nyasi na huwa zinapandwa kwenye kitu kinachoitwkuna kitu kinaitwa GEOTEXTILE , Hii ni aina fulani ya zulia hivi ambalo huwa linamatumizi mbalimbali kama kwenye Barabara, mabwawa nk. Kwa hiyo zinachukuliwa nyasi halisi na kupandwa juu ya hilo GEOTEXTILE (ni kama watu wengine wanavyootesha ulezi au njegere kwenye kunia la katani) kisha zikisha kuwa kwenye kiwango kinachotakiwa kuna mashine inakuja kuzikata kadiri ya uhitaji wa mwenye kiwanja kama draft, round, au mistari yenye patern tofautitofauti, wakati huo kiwanja kinachenda kuwekwa hizo nyasi kinakuwa kiko kwenye level na kiko compacted vizuri sana
Hiyo Geotextile ikiwa na majani yake inakuja kuwekwa kwenye hicho kiwanja na kisha wanakishindilia na Roller, na majani yakichakaa wanatoa kipande kizima na kuweka kinginge maelezo marefu nadhani utakuwa umenielewa japo nimeshindwa kukuelekeza vizuri
Angalia picha hapa ya nu camp-Barcelona, wao walikiwa wanataka kuweka majani ya rangi tofauti hivyo wamekata kipande hicho cha yellowish-green na watakuja kuweka deep Green

wow asante sana mkuu, kwa hiyo kuna tofauti kati ya nyasi bandia na asili? na kwa maana hiyo mkuu OT na wengine sio bandia?
Nyasi bandia mtachezea nyie masikini tu

Nyasi bandia huwezi kuchezea majira ya joto sababu huumiza nyayo na miguu kwa joto Kali mfano karume pale watu hutia maji ndani ya njumu kupoza

Viwanja vya nje na vinavyotakiwa ni za nyasi asili mfano hivo viwanja ot ,bernabeu,camp nou,Emirates nk nk huoni halftime au kabla ya mechi kuna bomba zinamwagia maji au wakati wa matengenezo mashine za kupunguza nyasi

Au wakati wa mvua matope,nyasi kutoka

Ulaya hawatumii nyasi bandia,
Sie tunatumia nyasi bandia sababu matunzo ya uwanja ni gharama sana
 
Synthetic Grass(plastic grasses) pitches and natural Grass pitches.
Natural Grass pitches zinakubarika zaidi kuliko synthetic grass pitches ila kuna-exception kwa nchi za ulaya Mashariki.
.
 
Nyasi bandia mtachezea nyie masikini tu

Nyasi bandia huwezi kuchezea majira ya joto sababu huumiza nyayo na miguu kwa joto Kali mfano karume pale watu hutia maji ndani ya njumu kupoza

Viwanja vya nje na vinavyotakiwa ni za nyasi asili mfano hivo viwanja ot ,bernabeu,camp nou,Emirates nk nk huoni halftime au kabla ya mechi kuna bomba zinamwagia maji au wakati wa matengenezo mashine za kupunguza nyasi

Au wakati wa mvua matope,nyasi kutoka

Ulaya hawatumii nyasi bandia,
Sie tunatumia nyasi bandia sababu matunzo ya uwanja ni gharama sana
asante sana mkuu kwa maelezo yako.
 
Kuna viwanja wa Asili kabisa ambavyo majani yanapandwa na kutunzwa, pili kuna viwanja vya nyasi Bandia ambazo ni aina fulani za plastic kwa hiyo zinatengenezwa kama carpet

Kwa viwanja vingi vya ulaya huwa ni nyasi asilia, lakini huwa hazipandwi hapo kiwanjani kunakuwa na kampuni zenye vitalu maalumu za kupanda na kutunza hizo nyasi na huwa zinapandwa kwenye kitu kinachoitwkuna kitu kinaitwa GEOTEXTILE , Hii ni aina fulani ya zulia hivi ambalo huwa linamatumizi mbalimbali kama kwenye Barabara, mabwawa nk. Kwa hiyo zinachukuliwa nyasi halisi na kupandwa juu ya hilo GEOTEXTILE (ni kama watu wengine wanavyootesha ulezi au njegere kwenye kunia la katani) kisha zikisha kuwa kwenye kiwango kinachotakiwa kuna mashine inakuja kuzikata kadiri ya uhitaji wa mwenye kiwanja kama draft, round, au mistari yenye patern tofautitofauti, wakati huo kiwanja kinachenda kuwekwa hizo nyasi kinakuwa kiko kwenye level na kiko compacted vizuri sana
Hiyo Geotextile ikiwa na majani yake inakuja kuwekwa kwenye hicho kiwanja na kisha wanakishindilia na Roller, na majani yakichakaa wanatoa kipande kizima na kuweka kinginge maelezo marefu nadhani utakuwa umenielewa japo nimeshindwa kukuelekeza vizuri
Angalia picha hapa ya nu camp-Barcelona, wao walikiwa wanataka kuweka majani ya rangi tofauti hivyo wamekata kipande hicho cha yellowish-green na watakuja kuweka deep Green

kwanza nikushukuru kwa maelezo yako mazuri nimekupata kwa asilimia nyingi tuu. kuna kitu umekisema "majani yakichakaa wanatoa kipande kizima na kuweka kinginge" kwa hiyo
1. hizo nyasi asilia zina muda kwa kukaa kabla ya kuwekwa nyingine?
2. kinachochakaa ni nyasi au GEOTEXTILE?
3. muda wa hiyo GEOTEXTILE kuktumika ni miaka mingapi kabla ya kuweka nyingine?
 
1: Kaka nyasi ni nyasi tu, zIkikanyagwa sana zinachakaa/zinachokanna ndio wanazibadirisha,
2: Mara nyingi kinachochakaa ni nyasi kwani wakati wa kuzitoa huwa wanabandua pande zimazima, so kamaningekuwa geotextile ndio zimechakaa isingekuwa rahisi kubandua hivyo
3: Geotextile ziko za aina tofauti kulingana na kazi, zinazotumika kwenye ujenzi zinakaa miaka mingi tu, nadhani hizi za kwenye viwanja ni za muda mfupi, sina uhakika ni miaka mingapi
 
nikushukuru ten MKUU kwa maelezo yako nimekuelewa asante sana.
 
Pia Kuna aina ya nyasi original zaidi kama kule Jamhuri na Nangwanda Sijaona!
 
1: Kaka nyasi ni nyasi tu, zIkikanyagwa sana zinachakaa/zinachokanna ndio wanazibadirisha,
2: Mara nyingi kinachochakaa ni nyasi kwani wakati wa kuzitoa huwa wanabandua pande zimazima, so kamaningekuwa geotextile ndio zimechakaa isingekuwa rahisi kubandua hivyo
3: Geotextile ziko za aina tofauti kulingana na kazi, zinazotumika kwenye ujenzi zinakaa miaka mingi tu, nadhani hizi za kwenye viwanja ni za muda mfupi, sina uhakika ni miaka mingapi
baadae naenda kuanzisha ubishi baa.....watanikomaaaa....kwa nondo hizi
 
Back
Top Bottom