Hongera kwa vipimo "vya awali" kuonesha huna maambukizi.
Kuna aina kuu mbili za vipimo vya HIV/AIDS. Aina ya kwanza ni hiyo Antibody test ambazo huangalia chembe chembe za mwili zinazotengenezwa ili kupambana na vijidudu (antibodies). Hizi mara nyingi sio conclussive, japo ndo kipimo kikuu hapa kwetu. Sio conclussive kwa kuwa kinapima only antibodies ambazo zinachukua muda kutengenezwa na mwili. Kwa hiyo kama umepata maambukizi ndani ya wiki mbili say, hakiwezi ku-detect any antibodies. Pia huwa hakiko 100% specific., japo kiko sensitive kiasi, ila hii ndi sababu mtu hufanyiwa zaidi ya test moja kama hapo juu ulivyofanyiwa. Hizi Antibody tests ziko za aina mbali mbali. Kuna rapid test, yaani ambayo unatumia tone moja tu la damu, na unaweka kwa kiji-test unapata majibu in 5minutes, hizi huitwa rapid tests (zipo SD. Bioline, determine, unigold na kadhalika), pia kuna ELISA, ambayo nayo ni antibody test. Hii hufanyika maabara maana inahitaji titration na huchukua muda zaidi. Aina nyingine kuu kati ya mbili nilizonitaja juu ni ya DNA ama RNA particle ya virus mwenyewe. Hii hutumia PCR nahuhitaji maabara kubwa zaidi. PCR-DNA ama RNA ndo superior test zaidi ya hizo za antibodies, hii huweza ku-detect HIV kwa haraka, uhakika, na haikosei kosei kama Antibody tests. Ni gharama, na hutumika kwa sababu maalum pekee. Sababu hizo ni kama, neonatal HIV tests, kuhakikisha mtu ana immediate infections in case of rape etc. Sio kawaida kufanya kipimo hiko hapa kwetu kwa sababu za gharama.
Having said that, nakupongeza kwa ushujaa wa kwenda kupima, na naamini utarudi tena kupima baada ya miezi mitatu kama ulivyoshauriwa (naamini ulishauriwa hivyo). Mean while jitahidi kuzuia maambukizi mapya, zingatia mwenendo bora, na tumia kinga katika tendo la ndoa.
stun