Kuna aina ya Ukristo ambayo ni ushetani

Kuna aina ya Ukristo ambayo ni ushetani

Aisee kuna jamaa yetu aliowa mjeda hawa mabaka mabaka bidada kabezi huko kanisani humwambii kitu. Mshahara karibu woote wanapeleka huko mume akimwambia anamjibu Zaka, nadhiri, malimbukuko, sadaka basi taflani ndani. Mwisho jamaa kamwacha bidada aendelee na maisha yake na yeye kala kona ndoa chali wamegawana fito hakuna kujenga nyumba moja teena. Ni mwaka wa sita sasa toka watengane.
Hao wa kwenu
 
Umeongea yote..,wanafanana tabia. Kuna mmoja nilikuwa sijui kama ni hao nilikuwa namuona mstaarabu mwenye hekima, akata kuniletea pigo hizo..,nikapiga chini.
Nawafahamu ukiacha huyu mwenzangu, kuna jamaa yake nae alikuwa mke wake anaingia huko akampiga marufuku kamuweza. Huyu wa kwangu imagine alikuwa na ujauzito wa miezi kati ya saba au nane, katoka nyumbani saa kumi na moja alfajiri kaelekea kwa Mwamposa kuwahi nafasi za mbele na nimemkataza apumzike kakataa. Katoka nyumbani Kitunda hadi Tanganyika Packers kwa Mwamposa na usumbufu wa usafiri na tumbo kubwa 😭😭 na shida inakuja mama yake ni muumini nambari moja wa hizo mambo na humwmabii kitu kuhusu Mwamposa. Yani humwambii chochote akuelewe aisee kama karogwa.
 
Kupotoka kwa mke wako kimaadili ya ndoa na kikristo usiu type ukristo kuwa kuna ukristo wa kishetani. Huo alionao mkeo sio ukristo, ni ushetani unaouona wewe. Kama nawe ungekuwa mnaabudu pamoja usingeona huo ushetani. Hebu jaribu kuungana na mke wako uwe unasali pamoja ili picha ya ushetani ikutoke. Ukristo ni mmoja hakuna aina nyingine zaidi ya upotokaji tu
Anasingizia Ukristo na ulokole je angekuwa mcheza Ngoma au mama shughuli kila kukicha kwakijumbe vipi hapo? Wanafiki tu hawa.
 
Simsemi mke wangu vibaya, ila ndio tumecharurana na saa hizi naenda kulala bar.

Mkiona napost post za kilokole, basi junior kwamba mke wangunni mlokole nguli, ila ulokole wake unanifanya na mimi niwe mlevi nguli.

Mke wangu ana mabanda ya kuku hapa uani, kuku wake wanamulikwa na taa za umeme lukuki kupata joto.

Mi nikiwasha ac au hata feni dakika kidogo tu, tutagombana wiki nzima. Leo katoka shopping ya wiki kakuta najipepea na feni tu, kawasha moto namaliza umeme, utadhani matako yake yameshawahi kununua hata unit moja.

Hii mianamke ya kilokole isiyo na akili msiioe, ni hatari kwa furaha ya nyumba yenu.

Anafuga kuku, ten pasenti inaenda kwa mchungaji. Kuku wakubwa wa mwanzo anawaita limbuko anampa mchungaji, yaani ujinga mtupu.

Kasheshe ni kubwa kuishi na likitu hili. Mchungaji analishwa makuku wakubwa wakubwa, mimi sili kuku hadi nilishwe magendo vibudu vya kuku waliokufa.

Good enough nina mahusiano mazuri sana na watenda kazi wangu, kuanzia bandani, garden hadi jikoni, navujishiwa za ndani zote.

Mara mlokole ajaribu kuniwekea sumu, mara ajaribu kunikisha limbwata, mar amfukuze.mama yangu na ndugu zangu, mara aniambie utakufa mapema, hutakiwi kutuficha mali zako.

Jamani wanawake mmepatwa na kinyamkera gani?
Je huo mtaji wa kuku ulimpa wewe?
 
Ukishaanza tu kuwa mfuasi wa hizo imani zao za mchongo automatic hata akili zinaruka.

Angalia maisha ya walokole 90% hufanana kwa kila jambo mpaka kiuchumi hali yao huwa ni moja, umasikin+ufukara ni sehemu ya maisha yao.

Uvivu wa kutumia akili na kutegemea miujiza bila kusahau kuendekeza kuwachangia pesa na mali hao matapeli wanaojiita wachungaji, mitume na manabii.

Kama mke wako anakwenda hayo makanisa mpige marufuku akigoma fukuza akakae na mchungaji wake, kama ni mpenzi achana nae huyo atakutesa hapo baadae.

Walokole wote akili zao ni moja na akili zao zimelegea, kiufupi hawana akili, haiwezekan unaacha mtaani kwako wagonjwa, mayatima na wahitaji huwasaidii lakin unavuka miles+kilomita za kutosha kwenda kupeleka pesa kwa mchungaji+kanisani eti unamtolea Mungu, Mungu gani huyo unamtolea kwa kubagua watu wake wenye uhitaji ambao ndio ndugu zako hapo mtaani?.

Walokole na wenye tabia mbovu kama hizo acheni kupoteza muda wenu huko ktk makanisa yenu ya mchongo, fanyeni kazi, waheshimumi waume zenu, saidieni wahitaji mlionao karibu na sio hao wachungaji.someni biblia zenu msiwe wapumbavu
 
Walokole ni mazuzu yanayosomewa Bible ikiwa imegeuzwa juu chini
yaani jitu ambalo maandiko yanasema Mungu yupo ndani yake still usiku ukifika linaomba maombi ya kumfunga shetani na mkuu wa anga ambaye anazuia maombi yake yasifike Mbinguni kama sio uchizi ni nini?
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Indoctrination ni mbaya sana Mkuu. Ujinga huu ndio uliosababisha hayo yanayoendelea huko kwa kina Mackenzie. Dini ni ulevi mbaya zaidi ya madawa.

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
 
Daaaah ndo maana ulipoteaaa kumbeee hujapungua kweli mkuu? weka hata picha tukupe pole
 
Back
Top Bottom