Simsemi mke wangu vibaya, ila ndio tumecharurana na saa hizi naenda kulala bar.
Mkiona napost post za kilokole, basi junior kwamba mke wangunni mlokole nguli, ila ulokole wake unanifanya na mimi niwe mlevi nguli.
Mke wangu ana mabanda ya kuku hapa uani, kuku wake wanamulikwa na taa za umeme lukuki kupata joto.
Mi nikiwasha ac au hata feni dakika kidogo tu, tutagombana wiki nzima. Leo katoka shopping ya wiki kakuta najipepea na feni tu, kawasha moto namaliza umeme, utadhani matako yake yameshawahi kununua hata unit moja.
Hii mianamke ya kilokole isiyo na akili msiioe, ni hatari kwa furaha ya nyumba yenu.
Anafuga kuku, ten pasenti inaenda kwa mchungaji. Kuku wakubwa wa mwanzo anawaita limbuko anampa mchungaji, yaani ujinga mtupu.
Kasheshe ni kubwa kuishi na likitu hili. Mchungaji analishwa makuku wakubwa wakubwa, mimi sili kuku hadi nilishwe magendo vibudu vya kuku waliokufa.
Good enough nina mahusiano mazuri sana na watenda kazi wangu, kuanzia bandani, garden hadi jikoni, navujishiwa za ndani zote.
Mara mlokole ajaribu kuniwekea sumu, mara ajaribu kunikisha limbwata, mar amfukuze.mama yangu na ndugu zangu, mara aniambie utakufa mapema, hutakiwi kutuficha mali zako.
Jamani wanawake mmepatwa na kinyamkera gani?
binafsi naishi kwa namna hiyo pia, na nimebarikiwa sana kwasababu hiyo, na hakuna mtu ambaye huwa anasimama kupambana na mimi kwa chochote lazima ashindwe kwasababu mimi sipigani peke yangu, ninapiganiwa na Mungu. kama haujui, Mungu sio fukara, Mungu sio maskini, ila anahitaji ushirikiano nasi just kuonyesha kwamba tunampenda na kumtiii, that's all he needs. ndio maana ipo sheria ya kiroho kabisa (sio sheria kama za wasabato, ila ni spiritual law) ambayo kwa kitu chochote unachozalisha, kabla haujakula matunda yake, yale mavuno ya mwanzo unatakiwa kumpa Mungu, na sio lazima umpe yoooote, hapana ni vile moyo utakavyoamua ila cha muhimu usile kabla Mungu hajala, unampa Mungu ale kwanza ndio wewe ule. (INAITWA MALIMBUKO), kwa namna hiyo, nimeshuhudia kwa maisha yangu, kila project ninayofanya hivyo huwa inakuwa bora kuliko chochote.
kitu kingine, fungu la kumi limekuwa likipingwa na wengi sana hasa siku hizi za manabii wa uongo, mimi pia nilishawahi kuwa convinced sana nao hasa wale wanaopiga, lakini cha ajabu nikamsikiliza mtu wa Mungu mmoja hivi aliyesema na yeye alishawahi kuhubiriwa sana moyoni kwamba fungu la kumi sio la nyakati hizi, ni la nyakati za kale, LAKINI AKASEMA, AKAAMUA AJARIBU MAISHA YA FUNGU LA KUMI NA YASIYO YA FUNGU LA KUMI YANAFANANAJE? Akaja kugundua kwamba, miezi ile ametoa fungu la kumi anapokea faida na baraka kuliko miezi ile ameiba fungu la kumbi ambayo matatizo mengi hutafuta mtaji na pesa zake, conclusion yake ikawa ni kwamba fungu la kumi ni lazima kwa kumtii Mungu na bado ni spiritual law. hata Yesu alisema, mafarisayo wamekazania kutoa fungu la kumi na kusahau mambo ya msingi (utakatifu) akawaambia mnatakiwa kuushika utakatifu, "na hayo pia (akimaanisha fungu la kumi) msiache". hivyo Yesu mwenyewe alisema hata pamoja na kufuata mambo mengine ya kimungu hatutakiwi kuacha kutoa fungu la kumi.
Mimi pia nilifanya utafiti kwa experiencwe yangu kabisa, na ninashuhudia kwa moyo wangu wote wala sisemi uongo, nimethibitisha kuwa fungu la kumi ni la lazima kama unataka kubarikiwa na Mungu. Roho Mtakatifu pia ananishuhudia kila siku kwamba fungu la kumi ni lazima na usipotoa ni dhambi kwasababu unakaidi sheria ya rohoni ya Mungu aliyoitoa kitabu cha Malaki. kuna project moja nilihangaika nayo sana miaka 5, ikasimama, sikutoa limbuko, wala fungu la kumi, ile project niliishia tu kupata mtaji nilioanzishia, faida yote ililiwa na magonjwa, ndugu, wezi na mambo kibao.
mwaka 2019 nikaanzisha project tena kama ile ile ya awali, maana ile ya awali ilikufa nikasahau kabisa shughuli hizo. nikauza, mauzo yangu ya awali, tena yalikuwa laki moja tu, nikaipeleka church kama sadaka ya malimbuko kabla sijaanza kula matunda ya ile project. kilichofuata, products zangu au niseme shughuli zangu zilianza kubarikiwa na hakuna ambaye huwa anasimama dhidi yangu, ni kama kuna kaupako/kibali fulani, wengi wanaanzisha project kama yangu na hata wakiweka karibu yangu wanaondoka wenyewe, na situmii uchawi wala dawa.
Mungu ameahidi tukitoa fungu la kumi yeye atamkemea alaye na kuharibu mazao/shughuli zetu. na pia kwa habari ya malimbuko, ukimpa Mungu ale kwanza faida ya kile ulichoanzisha nakuhakikishia along that business Mungu ataenda pamoja na wewe, atapambana na wale wanaokuhujumu na wewe binafsi hautapambana bali Mungu atakupambania. unakuwa umemheshimu Mungu, umemuweka yeye kwanza na wewe ufuate, hivyo Mungu atakutangulia kwenye shughuli zako zote na kila unachokifanya, nimethibitisha hili na ninawashauri wote msisikilize maneno ya manabii wa uongo na wapotoshaji wanaotumiwa na shetani. pia jueni kumtii Mungu ni uamzi wa binafsi, chagueni kufuata au kutofuata, kwasababu kwa kila uamuzi utakaoutumia utafuatana na matokeo ya kule ulikochagua.
nilikuwa nashangaa zamani kwanini Mungu ameandika kuwa, "onjeni muone kwamba Bwana yu mwema, heri mtu yule atakayemtumaini", kumbe Mungu anajua wanadamu ni wabishi na wanapenda kufuata upotoshaji wa mashetani, ndio maana anasema jaribuni kufanya hata haya kwa mfano, jaribuni kwa maisha yenu kutoa fungu la kumi na kutoa limbuko, halafu muone kama Bwana hatakuwa mwema kwenu. nina uhakika Mungu ni wa kuaminiwa, na atajidhihirisha hata wewe uliyeandika hapa utakuja kuwa balozi wa wenzako. jaribu tu, ukiona kweli haujaona matokeo chanya, basi labda atakuwa sio huyu Mungu ninayemwamini mimi na ambaye nimemwona maishani mwangu.
NB: fungu la kumi sio la kutoa kila sehemu, unaweza kutoa kwa manabii wa uongo wanaotumiwa na shetani, ikawa haijaenda kwa Mungu imeenda kwa mashetani, toa sehemu ambako kuna Mungu wa kweli, sehemu wanayoamini wokovu wa Yesu Kristo, sio sehemu wanayoabudu masanamu na maria, na sio sehemu wanayotumia mafuta na chumvi badala ya kutumia Jina la Yesu. toa sehemu ambayo wameokoka na wewe uokoke ndio matokeo yote hayo utayaona. all in all, utii ni wa muhimu kuliko dhabihu, na kwenda kwako kanisani, tii Neno la Mungu.