Kuna anayemuelewa Mtangazaji Maulid Kitenge na 'Interview' yake EFM akiwa na Gerald Hando?

Kuna anayemuelewa Mtangazaji Maulid Kitenge na 'Interview' yake EFM akiwa na Gerald Hando?

Kwa dakika 50 natafuta ya maana siyaoni sana sana ninachosikia tu ni 'Kujimwambafai' Kwake kingi tu kuwa amekaa Marekani, kaenda CNN, BBC, Facebook, Instagram, VOA, nimeachana na Mke wangu.

Nimeenda katika Kaburi la Bruce Lee, nimeenda alipouwawa Yule Mwafrika Floyd,zote Mimi ni Mtangazaji mkubwa sana Tanzania. sijaona bado wa Kunirithi Kiutangazaji wa Michezo, sina nina Watoto Wanne na Upuuzi mwingine mwingi na Ushamba lukuki.

Naomba aliyemuelewa anidadavulie pia.
Mpaka hapa umeshamuelewa
 
Mtangazaji kama huyu,hawezi kuajiriwa nje ya mipaka ya Bongo.

Ana jina kubwa lakini,Elimu yake haiwezi kumfanya awe kama Raly king wa CNN,au Jeff Koinage wa Kenya,au hata Hussein Mohamend wa Citizen.

Huyu kitenge ilibidi aajiriwe hata na Aljazeera kwenye kipindi Cha michezo,lakini sidhani,amekalia story za kimanzichana, mwanakwelekwe, Tandale, Kawe, local issues,ambazo hazivuki mipaka.
Duuuuh..... yan Kitenge alikuwa wa kuajiliwa Aljazeera...? Me mbona sioni umaalum wake katika tasnia, au n sikio langu tu ndilo linamsikia vbaya...?
Namuona kama mpiga makelele Radioni mwenye jina kubwa kwenye tasnia.
 
labda ndo vitu alivyotamani kuvikamilisha katika uhai wake [emoji2375]
 
Back
Top Bottom