Kuna athari zozote kama tukivunja uhusiano na WB,IMF au Marekani?

Dah!.. Sasa tukivunja itakuwa vipi kuhusu madeni tunayodaiwa na hizo taasisi? Je tugome kuwalipa?
Tugome kuweka mfano kwa nchi zingine duniani kwamba mabeberu inawezekana kugomewa!!
 
40% .... 60% iliyobakia na wahisani...


Cc: mahondaw
Kumbe kama ni kwa 40% basi tuachane nao tu. Maana bila ya kuachana nao nchi yetu itaendelea kugawanyika kati ya Vibaraka wa mabeberu na wazalendo. Nadhani tukiachana nao Tanzania itabaki na wazalendo tu wanaopambana kwa manufaa ya nchi yao!!
 
Kumbe ni watu wazuri. Tuendelee nao.
 
Sio kujiondoa.. Waweke vikwazo tu.. Muulize Mugabe
Kwanza lazima ujue nchi yako ipi kundi gani? In short ni nchi masikini
IMF, Ukiishiwa fedha za kigeni utanunua nini nje ya nchi kwa Tshillings?
WB inakupa tafu Sana mikopo mingi... Ingawa inakudai pesa kibao.
marekani ina piga tafu miradi mingi ikiwemo ukimwi etc.. Pia inaushawishi kwa mataifa mengi.. Ni rahisi mataifa mengine kukutaaa..
Bado hujafika kiwango cha kujitegemea... Hata hao Iran, North Korea etc wanalia Marekani iwaondolee vikwazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kujiuliza hilo SWALI, weka kwanza list ya mikopo na misaada tunayopewa na inakotoka. usisahau huu wa juzi wa kupambana na COVID-19... THEN BAADA YA HAPO CHECK HIYO LIST NS KAMA HAO ULIOWATAJA WAPO, BADI JUA MADHARA YAKE NI MAKUBWA.. utakosa yote yaliyosababisha tupewe mikopo na misaada
 
Hakuna.

As long as we have our own 'Moses' as described by Prof. wa Jalalani, Kalamaganda Kibudu.

However, as soon as we are without him, in one way or the other; ni lazima kuwarudia hao jamaa haraka. Hakuna tunachopoteza kwa kuwa nao, mradi tunajua tunachofanya.
Hawatulazimishi kufanya lolote bila ya matakwa yetu wenyewe, na kujua hali yetu ipoje, inaruhusu kukataa/kukubali masharti?
 
Huko nyuma Mwl.Nyerere Nyerere aliwahi kuvunja uhusiano na Marekani sababu ya Rhodesia enzi za Mlowezi Ian Smith lakini haikuleta mabadiriko yoyote kwa USA haikubadirisha sera yake juu Rhodesia. Akarudisha baada ya muda mfupi.
Kipimo cha "kuleta mabadiliko" kukoje mkuu sblandes'?
Unajuaje kuwa hakukuleta mabadiliko, au ulitaka siku hiyo hiyo ya "kuvunja uhusiano na Marekani" Uhuru wa Zimbabwe upatikane?
 
Baniani mbaya kiatu chake dawa..
Bosi hanuniwi..
Hata mpalestina anashindwa kuvunja uhusiano na muisraeli..
Palestinians cross border kwenda vibaruani Israel..
Tumbo tumbo lazima tulihudumie...

Everyday is Saturday.........................😎
 
China tu kila siku anaomba marekani amuondolee vikwazo kwenye makampuni yake na kwenye jeshi lake aweze kununua vifaa na technolojia ya kijeshi nchi za nje.

Sisi ndio tuvunje mikataba na mahusiano? Kikwazo kimoja tu njaa inatuua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…