Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
Bila kubadili mfumo wa uongozi ni ngumu kutokuwa tegemeziInawezekana ila ni vema kupunguza nao mazoea taratibu kwanza tukijiandaa kujijenga.... Lakini hilo litawezekana zaidi kama tutaimarisha benki yetu ya Africa na kuwa na common fund plus kujenga uchumi wa afrika usio na mashiko na mataifa ya nje ya afrika kwa maana kujitegemea kwa mikopo ya masharti nafuu.
Lakini pia, ni vema kujijenga upya kitaasisi kwa kuanza na taasisi namba moja ambayo ni familia ili kujenga ustawi wa jamii ngazi ya kata hadi taifa.
Viongozi wanaopiga madili hawa ni wakuwadhibiti kwa kila namna na kuwacontain na pia turekebishe mifumo ya kisheria ya biashara, kiuchumi, na haki za kiraia.
Nilikasirika sana kusikia hata ile kampeni ya "Nawa challenge" eti imefadhiliwa na Watu wa marekani..!!
hakuna nchi imewahi kuvunja uhusiano na WB na IMF, kuhusu Marekani athari yake ni tutakosa misaada lakini kuvunja uhusiano nao inawezekana mfano Zaire ilivunja uhusiano na Marekani kwa sababu Marekani ilishiriki jaribio la kumpindua Rais na ikavunja uhusiano na Belgium kwa sababu kuna mwandishi wa ki belgiji aliandika kitabu cha kumkashifu rais
Hivi Bavicha mnamatatizo gani kwani sasa tuvunje mahusiano ili iweje?
Au umetumwa Mkuu
Hardworking pays!!!
Kwa Tanzania bado hata kuthubutu hatuwezi kuvunja uhusiano na USA
Mkuu be serious. Hapa Tanzania, hakuna kiongozi mwenye utashi, nia wala jeuri ya kuvunja uhusiano na taasisi hizo. Kinachoendelea ni politiki uchwara kuwafunga kamba “wanyonge” - period.
Hata Nyerere alijua hana jeuri hiyo. Angalau alisimamia mwiko wake binafsi wa yeye kutokuwa na mkono katika makubaliano ya kushinikizwa na “mabeberu” hao; akampasia mzee ruksa urais na zigo lake la kumwaga wino kwenye makubaliano na IMF.
Tusimame na kutembea kwa miguu yetu wenyewe? Won’t happen kwenye jamii iliyojaa watu wanaoshindana kuwa wajanja, kula bata kwa sana kwa utajiri wa harakaharaka wa kufisidi dola, kuchezesha kamari, kuchuuza upako, miujiza, ulozi n.k.
Tumeachwa mbali kabisa na nchi za Asia ya mbali (China, Japan, Malaysia, Singapore, n.k.) zenye utamaduni wa kufanya kazi kwa juhudi kubwa na maarifa ambazo, pamoja na yote, hazina mpango wa kilevi wa kukorofishana na Marekani, WB, IMF.