Kuna baadhi ya watalii wa kigeni wanaroho mbaya sana

Kuna baadhi ya watalii wa kigeni wanaroho mbaya sana

Sasa amekuja kuamua ugomvi wa nature au kaja kutalii

We ukiona paka anavizia panya unamfukuza

Sasa wakale wapi gengeni ama
Mnyama anaepewa nyama ni zoo tu ila hao wanajitafutia wenyewe Sasa ugomvi usiomhusu auingilie wa nini?

Kama umewahi kumsikia Kevin Carter basi huyu ndio ungemtukana sana na hata kulia kwa uchungu

Alikuwa anarekodi vulture akimsubiri mtoto wa kike afe ili amle
Ilikuwa mwaka 1993 huko Sudan

Dunia nzima ilimlaani ila alikuwa best photographer na alipewa tuzo NY

Baada ya miezi 4 tangu apate tuzo alijiua mwenyewe
Alishindwa kuvumilia maneno kwani angeweza kumsaidia yule mtoto na hata kumpa maji na chakula pia kumpeleka katika kambi ya wakimbizi iliyokuwa nusu maili tu kutoka hapo

Sasa yeye anasema alikuwa anafanya kazi ya kuripoti matukio anaeliwa sio kazi yake

Hii picha iliniliza pia

Hivi iliishia wapi
 
Jamaa anawachota akili na nyie mnachoteka mnaanza kumuelekeza😁😁😁😁
 
Mfumo wa maisha ya wanyama pori hautakiwi kuingiliwa. Hivyo ndivyo wanavyoishi siku zote
 
Hakupitiwa kumsaidia bali aliona amepata bonge la picha na litamuingizia hela ndefu sana

Kujiuwa kwake sio kuwa Ali feel guilty hapana bali tulimlaani sana kila kona ya mitandao mwisho akapata depression akajiua

Haya kuhusu mleta Mada sidhani kama ni mjinga la hasha anajua kabisa anachoandika anataka hoja ijibiwe tu
Hoja gani hapo? Hakuna hoja bali kuna wazo la mtu asiyejua yaani mjinga. Kuhusu mpiga picha: Unategemea mtu mwenye roho ngumu ajiue kwa sababu tu ya kusakamwa? Hiyo kujiua inaonyesha kuwa alijua ni kosa alifanya na siyo kuwa alijiua kwa sababu ya kusakamwa. Wanasakamwa watu waliofanya makosa mkubwa zaidi na hawajiui!
 
Ilaumu Serikali yako ndugu! Hapo angeingilia si ajabu angebambikiwa shutums za kutaka kuiba nyara za Serikali, na chochote ambacho angelipa kingeenda kwenye matumbo ya watu.

Mi naumia sana napoona anauliwa mbele yangu sio kwamba sitaka aliwe hapana ila kuuliwa mbele yangu pale anapohitaji msaada wa kumuokoa alafu ndio kwanza unaseti camera vizuri.mi miliwahi okoa sunguea alitaka kuliwa na tai,yaani sungura aliingia mvunguni mwa gari katulia tulia tai kayua juu ya keria ya gari ki nikashuka nikamtimua
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Yaani unakuta mtalii tena mgeni yuko mbugani na mikamera yake alafu akikuta mnyama anaekula mnyama mwenzake kama fisi simba au chui anataka kula mnyama badala ya kumsaidia huyo mnyama anaeliwa asiliwe eti ndio kwanza anaseti kamera vizuri kushoti video mnyama anavyoliwa.

Kinachouma zaidi unakuta mnyama kama twiga au pundamilia na nyati ambae serikali ndio inawathamini zaidi ndio wanauwawa, badala ya kuzuia wanawaacha. Inauma sana/nimeumia sana, hawa watalii hata kama wanatuingizia hela nimewachukia sana.

Mbona kwao wanyama wao wanawapa nyama, tena mara nyingi naona ya ng'ombe hawaachi wakaua ovyo ovyo kama huku kwetu? Au wanafurahia wanyama wetu wanavyouliwa?
Mkuu, huyo ng'ombe nae hajauliwa?
 
Back
Top Bottom