Mi iliwahi nitokea huyu mtoto hakunicheki na namba akanipa akawa hana ushirikiano kama huyu wako nikasema dawa nikufuta namba, siku nikakutana naye mtaani daah mtoto ni anaita hilo wezere na rangi yake ni chocolate colour kwanza alipita mbali nikiwa nami nimempotezea akiwa anapita.
Hapo mi nilikuwa nina nunua mboga mahali kwa muuza duka la nyama, sasa mimi na huyo muuza duka tumezoeana hapo kitaa na mimi ni mteja wake hapo dukani alisimama mama mmoja hivi naye alikuwa ana nunua nyama, mi nikajiropokea baada ya demu kupita, nikasema yaani hili toto linaringia matako linajiona sana limefika wakati hayo ni mavi tu 😅😅 Amini usiamini yule muuza duka akanitazama kwa kuhamaki nikashutuka paaap😝😝😝 kumbe yule aliyekuwa shop ni mama mzazi wa mtoto lakini hakuwa mashallah kama mtoto.
Wacha mama aanze wewe kijana kweli we ndiyo umeamua kunitukania mtoto wangu yaani tena mbele yangu, mama alisononeka sana huku akisema ndiyo maana mabinti hawaolewi wanaogopa dharau zenu sijui imepanda imeshuka daaah.....
Muuza duka akanihakikisha yule ndiyo mzaa chema baada ya mama kuondoka pale na hasira nyingi.
mi nilibaki naduwaaa kama sio kweli yule sio mama yake, lakini nilifutaga namba ya binti mwanzo kabisa nilivoona hanipi ushirikiano nikapiga chini.
so hata nilivojiropokea pale ni lile tako lilivo pita pale kwa madaha huku nikijua kaniona fala tu mi nikaona isiwe kesi takorooo zipo nyingi tu kwani Shilingi ngapi?