Kuna binti anataka kufanya partnership (biashara) na wifi yake (mke wa kaka yake)

Kuna binti anataka kufanya partnership (biashara) na wifi yake (mke wa kaka yake)

Kama biashara ni kubwa basi atafute kampuni nzuri ya sheria waweke mkataba mzuri wa partnership kwa namna watakavyowekeza na kugawana faida
Kama ni ya kawaida aifanye peke yake na asione shida kabisa kusema "hapana nataka kufanya mwenyewe"
 
Kama sio wasomi. Bora waendelee tu na uwifi wa amani kuliko uadui wa milele
 
Hapa ushauri unahitajika maana nimeshauri mpaka nimechoka.

Kuna binti kaja kuniomba ushauri kuna biashara anatamani kufungua ila wifi yake yaani mke wa kaka yake anatamani kufanya naye partnership.

Watu wenye uzoefu na biashara za kufanya na ndugu hili swala mnaweza kushauri vipi.
Ila wewe una akili sana! Hutaki ifahamike kuwa ni wewe na wifi yako😀

Well! Mnaweza mkafanya, tena vizuri tu, ila muende kisheria na si "kindugu".

Makubaliano yawe clear from the beginning, na myaweke kisheria. Kwamba:
1. Nafasi na wajibu wa kila mmoja ifahamike
2. Vigezo vitakavyopelekea mtu kupoteza haki ya umiliki na fidia atakayopata endapo atakosa sifa ya kuendelea kuwa mshirika katika biashara
3. Mgawanyo wa mapato au faida/ hasara ya biashara
4. Na mengineyo yatakayoshauriwa na wakili

Wakati wa kusainishana, baadhi ya ndugu washiriki kama mashahidi ili mmoja akikengeuka huko mbeleni mwenzake asije kulaumiwa akimchukulia hatua kwa mujibu wa mkataba.

Muhimu ni Sheria kuzingatiwa. Undugu ni mkiwa nyumbani mnakunywa juisi, wakati wa kazi SHERIA NA KANUNI zitawale.

Mkienda kwa staili hiyo mtafika mbali!
 
Back
Top Bottom