Kuna bomu linakaribia kulipuka muda wowote

Hana Serikali ndio maana hana ajira?
Hawezi kuwatengenezea ajira vijana kwa sababu hakusanyi Kodi Wala Hana serikali. Sasa kama ccm imefeli tuendelee kuteseka tu wakati Kuna alternative. We unaonaje, tuendelee kufa kwa njaa na kuendesha boda boda? Ccm inasema inazalidha ajira za bodaboda kila siku
 
Kumbe hukuelea swali maskini wa Mungu! Nilikuuliza, Lema ana ajira gani! Yaani anafanya kazi gani? Simple!
 
Hao waliomaliza masters na degree wameshauriwa waende VETA ili wakapate ujuzi
Mambo kama haya utayasikia Tanzania pekee
 
Kwahiyo Lema analipwa kwakuwa mwanasiasa kama anavyolipwa Rais na Mawaziri?
Yule ni mjumbe wa halimashauri kuu ya chadema Kanda Ile hivyo kwa Sasa kabla ya kuchukua ubunge 2025 ni mwajiliwa wa chadema na analipwa kwa kazi hiyo
 
Wanazalisha ajira za bodaboda kwani hizo pikipiki nizakwao?
Waseme wamezalisha ajira za ma V-8
 
Yule ni mjumbe wa halimashauri kuu ya chadema Kanda Ile hivyo kwa Sasa kabla ya kuchukua ubunge 2025 ni mwajiliwa wa chadema na analipwa kwa kazi hiyo
Kwahiyo Chadema inawalipa mshahara wajumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kwa kwakuwa tu wajumbe una habari kwa kufanya hivyo, kitakuwa kimevunja rekodi ya Dunia ya vyama vyote? Kwani kitakuwa ndio chama pekee kuwalipa mshahara wajumbe kitu ambacho hakifanywi na chama chochote duniani! Au Mkuu unahabatisha haya mambo huyajui?
 
Kwani chongoro na mjema wanalipwa na serikali au chama
 
Hari ni mbaya sana mkuu,
Ni mbaya kuliko unavyoweza kufikiria,
Kuna wa kati huwa nakaa ndani peke ywngu,kimya,nawaza kesho ya hawa vijana,inatia huruma sana.
Nipo kwenye mipango,nifungue japo ka kampuni nitoe ajira japo kwa kijana mmoja
 
Jana kulikuwa na kongamano la wamachinga Dar ambapo waliwekewa mabasi ya kusombwa kutoka kila kona ya Jiji, lengo ni kutengeneza kura za 2024 na 2025.

Baada ya kuwawinda kwa migambo, kuwaharibia biashara zao kila baada ya chaguzi, hivyo kila inapokaribia uchaguzi serikali inaandaa program fake kabambe za wamachinga ambao hata mkuu wa nchi amewabrand kuwa wanachafua taswira ya majiji.

Programu hizi ni pamoja na kuhakikisha wanawekwa mapandikizi kwenye kitu kinachoitwa umoja wa wamachinga. Umoja ambao kazi yake kubwa ni kutoa matamko ya kusapoti projects haramu za serikali dhidi ya wamachinga. Haijawahi kutokea viongozi wa umoja wa wamachinga nchini au kwenye mikoa yao wakadai kurejeshwa maeneo ya masoko ambayo yalipangwa kwa ajili ya vendors na yakapewa watu wengine.

Juzi kati, serikali imewalipia nauli ya ndege viongozi kadhaa wa wamachinga kwenda semina huko Rwanda ambapo tutarajje pambio za kusifu watakaporejea. Hautakaa uone implementation ya walichokipata huko.

Wamachinga wa kweli hawataki blah blaha, wanataka fursa wauze bidhaa wanazpchuuza ili wahudumie familia zao. Enzi za yule mtu aliweza kugeuza dhamira za vijana kukimbilia uhalifu kwa kuwapa vipaumbele wamachinga na kuagiza wapangiwe masoko yao. Na siyo masoko ya pembezoni mwa miji au kusikofikika bali masoko yanayowapa unafuu wa kufika hata wateja wao.

Serikali inachojua ni kuwa adui yake mkubwa ni mwananchi ndo maana tuna zana na silaha nyingi za kudhibiti cold blooded citizens kuliko vifaa na vikosi vya uokozi wa majanga mbalimbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…