Kuna bomu linakaribia kulipuka muda wowote

Kuna bomu linakaribia kulipuka muda wowote

Boss huko kwenye mifuko ya kijamii wamekula pesa zote na ndio sehemu iliyobakia ya wao kupiga ndio maana kila uchwao kikotoo cha mstaafu kinachezewa na pesa yake imeisha. Acha utani wewe[emoji23][emoji23]
Yaani mkuu Zambia nimeona wamerudisha hiki kitu sisi ndio kwanza tunakifuta, huko mbele tutakuwa na taifa ambalo vijana wanategemea wazee sijui itakuwaje? Yaani wangeweka Ile Hela Kwa vijana iwe hata dhamana ya kukopea, tunaona wanasiasa wakitolewa kwenye vyeo wanafanya shughuli nyingine hata kulima nyanya, lakini wewe wa muhindi akikuachisha ndio basi
 
Mawazo mgando haya au wewe huna watoto wanaosoma shule za serikali? Nenda kule uone kulivyo na uhaba wa walimu wakati huo huo wasomi kibao wanazurura mitaani.
Mikoa ya kusini Haina watumishi hasa walimu ,
Shule moja Ina wanafunzi mpk la tano in walimu 2.
Shule nyingine 1 mpk 7 walimu 6
Shule nyingine 1 mpk 7 walimu 7
Nyingine 1 mpk 7 walimu 5..sitaki kumaliza lakini hebu jiulize rate hii ya walimu wanawezaje kila darasa SI chini ya masomo 5 huwa wanafundishaje ...

Hali Ni mbaya Sana wanasiasa hakuna anayejali
 
Kwanini tatizo la tangu 2015 ila lionekane sasa? Ajira hakuna miaka mingi nchi hii but awamu ya tano ndio kbs issue ya ajira ilikua changamoto hata kupandishwa madaraja marufuku kulipwa pesa wafanyakaz ilikua mtihan hasa madeni yao! Sometimes tuwe tu wakwel tatizo la ajira asitupiwe Samia kbs cz ni janga la muda mref!!! Hili jumba bovu watupiwe CCM in general but sio Samia!!
Ila wewe inaonekana kichwa chako kina maji na sio ubongo
 
Tunambebesha Samia lawama za bure tu. Yule Magufuli aliharibu mfumo mzima wa ajira na kipato katika nchi. Kwanza kwa kuanzisha miradi ambayo haina maana kama bwawa la Mwl Nyerere, kujenga viwanja vya hovyo vya ndege, kujenga Dodoma pasi na sababu, kunyima wafanyakazi haki ya msingi ya nyongeza ya mshahara na kuharibu kipato cha familia, kufukuzisha watu kazi hovyo, kuharibu mfumo wa mafao kwa wastaafu na sekta binafsi, kuharibu sekta binafsi, kuharibu mfumo wa siasa wa nchi na mwisho kufa kifo cha kizembe kwaajili ya ujuaji wa kijinga tu. Bye Magufuli.
mfalme juha.
 
Tujitafakari sana kama taifa maana wazungu wametuingiza kwenye mtego wa mda mrefu na sasa tumenasa maana walituletea elimu ambayo ilitakiwa ituwezeshe kutumwa na wao na sasa tumekuwa watumwa wa kifikra.
Sasa hapo mzungu unamlaumu kwanini yaani akujengee miundombinu akukopeshe mapesa kibao then unamlaumu.

Mm naona sababu ya hali hii ni akili zetu tu mbaya hatujielewi viongozi janjajanja watendaji janjajanja hakuna weledi.

Huna fadhira.
 
Kazi yenu ni kujilinganisha na ulaya. We unajua number ya wasomi ulaya? Karibu nchi nzima wana minimum kuanzia high school ama diploma.

Tanzania wamesoma wangap hata ngazi ya cheti?

Pia hao roll model wenu wa mchongo ulaya wanalipa unemployment alawance kila mwez kwa vijana wasiona ajira wakijua ni jukumu la serikali inayochukua kodi kila siku.

Je nyie mnawapa nini hao vijana pamoja walioko mtaani wengine tangu mwaka 2014?
Chief unamjua niliyemjibu alikuwa anaongelea hoja gani! 😂😂😂😂dah chief acha kukurupuka nakushauri, yaani acha kweli. Hivi unajua aliyelinganisha ni yupi boss😂😂😂
 
Unaelewa maana ya overpopulation?
[emoji23][emoji23][emoji23] boss nchi yetu haina overpopulation bali ina bajeti ndogo ya taifa. Kwa overpopulation hatujafika huko sema Dar ndio inaoverpopulation
 
Overpopulation ni tatizo kubwa linalochangia ukosefu wa ajira. Kasi ya ukuaji wa idadi ya watu inabidi kudhibitiwa ukichangia kasi ya ukuaji uchumi wetu ni ndogo.
Ewaaaaaa
 
Tatizo wengi hawana uelewa kuhusu overpopulation, hawafahamu kwamba overpopulation ni suala linalohusiana na balance ya kuzifikia rasilimali, huduma za kijamii, miondombinu na mifumo ya ku support hiyo idadi ya watu na sio ukubwa wa eneo tu.
Hii sababu isipozingatiwa tutaendelea kulalamika tu, Taifa lolote lenye mipango thabiti linazingatia sana namna ya kubalance idadi ya watu wake, ongezeko la watu ni muhimu liendane na fursa na ukuaji wa uchumi wa taifa husika, muhimu sana. Mataifa ya ulaya wamefanikiwa kuwa na Uchumi mkubwa, fursa zinazodi idadi ya watu. Hii inawafanya tatizo la ajira kuwa na athari ndogo kwao
 
Hata hao mafundi, madaktari na ma engineer wako wengi wamejaa mitaani wanamaliza soli za viatu tu kutafuta ajira.
Cha muhim jamii ibadilike kila nyumba ina mwalim wa arts watu waanze kusomea fani zingine tatizo vijana tunafikiri kazi za ufundi ni kazi za watu waliofeli ila huko ndo hela zilipo tena hubembelezi mtu ni wewe tu unaamshwa na sim za wateja
 
Jamaa kaandika kile anachokiona wewe unakuja kumuuliza swali. Kwanza hakuna serikali duniani inaweza kuajiri watu wake wote iwe ajira za muda mrefu au mfupi. Inachofanya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kujiajiri au kutengeneza ajira za muda mfupi ikiwa ajiri za muda mrefu hazipo, hii itasaidia vijana kupata mitaji ya kujiajiri.
Namuumiliza juu ya conceptions zake kuhusu maridhiano na asali! Je hayo yanaingiaje kweny ukosefu wa ajira? Hilo ndilo swali langu. NB; Ukileta hoja humu iwe ni mtazamo wako ama umepewa hoja uilete jiandae na maswal ya kila aina!!
 
Huwa nasikitika mno kwa kiwango cha kuugua ninapoona wale wasiosoma wanamcheka msomi wa digrii wanamwambia elimu yako imekusaidia nini.

Wakat wao wanaishi mjini kwa ushirikina na chuma ulete.

Yan inasikitisha mno.
Hakuna ushirikina hakuna chuma ulete changaamsha ubongo huo tafuta kazi ya kufanya.
 
Ila wewe inaonekana kichwa chako kina maji na sio ubongo
Kuliko ku attack personally ni vzr san ungejibu kilichopo au ungekuja na unachoona ni kwel au ni sahihi!! NB; Hakuna kitu kibaya kwa mwanadam kama kutojua kama hujui!!
 
Na hawa ndio watu pekee watakao tusaidia kuwatoa CCM madarakani, acha wajae tu mkuu siku wakichoka itakuwa rahisi sana kukitoa hiki kizazi cha watu walio laaniwa(CCM), mimi nikiona ma-jobless wanaongezeka mitaani kwakweli nafarijika sana naamini hawa ndio watu pekee wa kulikomboa hili taifa siku wakiamka.

Hawa CHADEMA na act wazalendo ni CCM wale wale tu hawana jipya tena, wazazi tafadhali sana pelekeni vijana wenu vyuoni wakasome taifa linaangamizwa na wajinga wachache.
uko sahihi sana, kweli jobless ndio mtaji mkubwa wa kuleta mabadiriko.
 
Back
Top Bottom