Kuna changamoto ipo

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Habari za wakati huu
Kwa mujibu wa mwenendo wa maisha ya leo, ambapo athari nyingi hasa za kimfumo wa uzazi zinamwangukia mwanamke, ni vyema kuona anapata watoto mapema.

Ni nadra kwa mwanamke wa miaka 35 ambaye hajawahi kuzaa, apate ujauzito kirahisi. "Kuzaa ni afya" kwa mujibu wa daktari fulani. Katika hili kuna masuala ya kujiuliza;

Mosi; kama mwanamke hajazaa na umri umeenda na ana mpango wa kuzaa afanyeje?

Iweje mwanamke ambaye aliweza kujizuia kuzaa nje ya utaratibu (japo alikuwa akishiriki), pia hakutumia njia hatarishi kuzuia ujauzito, leo hii asipate mimba?

Iweje mwanamke ambaye ujana wake allishiriki ngono na ndani yake akapata mimba na kutoa, huyu hata akifika miaka 37 anazaa? Ni kwa kuwa mfumo wake ulishajaribiwa, na unaendelea kusubiria uzazi

Kiimani kwa nini huyu aliyejisitiri aje kukosa uzazi? Na akiupata basi iwe kwa mbinde?

Itafika wakati mabinti wengi sana watabeba mimba ili tu kutunza kizazi, ili ikifika wakati sahihi waje kupata watoto bila shida.

Itafika wakati mwanamke ambaye hajaolewa na ana mtoto, na umri umesogea, huyu atapata wa kuwa nae.

Itafika wakati mabinti watabeba mimba kwa lengo la kufanya abortion ili kulinda afya ya kizazi.

Mwisho ningependa kupitia uzi huu tupate wataalam ambao wana ushauri chanya kwa mazingira yaliyoainishwa hapo juu. Nini kifanyike ambacho kitalinda afya ya kizazi (cha mwanamke) ambaye umri umeenda na hajabahatika kumpata mwenza, na ambaye hapendi kuzaa nje ya utaratibu?
 
Kabla ya mipango ndoa kutimia ukigusa tu imo, ngoja sasa ikishakamilika ndipo utaelewa kesho ni tamu au chungu, "the life is not fair at all".

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Kabla ya mipango ndoa kutimia ukigusa tu imo, ngoja sasa ikishakamilika ndipo utaelewa kesho ni tamu au chungu, "the life is not fair at all".

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
😁😁 Hatari sana
 
Maelezo mazuri. Pengine yamekosa majibu ya moja kwa moja kuhusiana na mada husika. Mfano kipengele cha tatu kinahitaji ufafanuzi zaidi
 
Ndoa ni sheria, kuzaa ni majaliw

Elimu ya kuwapa hawa wanawake sijajua inatakiwa iweje maana kama mfumo wa uzazi utaacha kufanya kazi ipasavyo baada ya miaka 30, na mwanamke huyu hajawa na hakika ya kupata mwenza, ni wazi atachagua kati ya hayo mawili; kuzaa ili kutunza kizazi, au kubeba mimba kisha kutoa. Nasikitika kuyasema haya kama vile ni kuwafundisha watu, ila ukweli ni kwamba haya mambo yanafanyika sana. Bora tu mwanamke azae kuliko kutoa mimba.

Sasa kwa maendeleo haya makubwa ya kisayansi tungependa kuona umri hauathiri ubebaji mimba angalau kwa mwanamke wa miaka hadi 40
 
wanawake wenzangu kamwe usibebe mimba kama haujawa tayari kua mama, kuzaa sio matako kwamba kila mtu anayo ya size tofauti.
 
Nisemetu kuzaa ni majaliwa au baraka kutoka kwa Mungu. Hiv unajua kwanin tumefika tuliko fika?
Vyakula
Madawa
Uzazi wa mpango
Mifumo ya ki electronic
Utandawazi
Na kujifanya tunajua kumbe hatujui

Shetani yuko kazin kiinani (kidini)
Kuna nguvu ipo nyuma ya haya yote kiimani(waaminio nguvu flan ulimwenguni)
Mwisho wakupotea kwa kizazi hichi cha mwanadamu(wasoamin katika Mungu)

Ila yote katika yote ilitabiriwa acha itimie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu kama kuzaa nje ya utaratibu. Kuzaa ni kuzaa tu.
 
Ukweli ni kwamba chakula kinachangia sana, pia mwili wa mwananke kukosa mshikemshike (mishughuliko ya kuweka mwili sawa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…