DOKEZO Kuna dalili 'Vigogo' wanajigawia bila kufuata taratibu eneo la Tanganyika Packers kipande cha ufukwe wa bahari

DOKEZO Kuna dalili 'Vigogo' wanajigawia bila kufuata taratibu eneo la Tanganyika Packers kipande cha ufukwe wa bahari

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Nawasilisha hoja yangu ambayo nimekuwa nikitafuta muda wa kuileta hapa jukwaani kama dokezo, ili kama mamlaka zitakuwa na uwajibikaji, vifuatilie hususan idara yetu na TAKUKURU.

Kama tunavyofahamu, eneo la Tanganyika Packers lililopo Kawe, Dar es Salaam, kwa sasa linamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Kwa historia fupi ya eneo hilo kwa wasiofahamu, awali lilikuwa ni kiwanda cha kusindika nyama (Tanganyika Packers) kilichojengwa na wakoloni na kumilikiwa na Waingereza hadi miaka ya 1975, wakati Serikali ya Tanzania ilipopitisha sera za Ujamaa na kukichukua kiwanda hicho kama ilivyofanyika kwenye maeneo mengine.

Baadaye eneo hili likawa mali ya Serikali chini ya usimamizi wa NHC. Serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikija na mipango ya kuliendeleza, ambapo mpaka sasa mpango unaoendelea kwa mujibu wa NHC ni ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika eneo la Tanganyika Packers.

Pia tuliwahi kuelezwa kuwa kuna mpango wa kuendeleza eneo hilo, zikiwemo juhudi za kuanzisha kiwanda cha burudani (Arena) kinachopangwa kujengwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa idhini ya Rais Samia Suluhu.

Soma ~ Kabudi: Mwaka 2026 Serikali itajenga Arena kubwa hapa Tanganyika Packers

Nimeeleza hayo kwa ufupi ili kuweka msingi wa jambo ambalo nataka kuwasilisha baada ya udadisi kutoka vyanzo mbalimbali na kubaini kwa macho yangu.

Nataka kusema nini?
Wakati jamii na watu wengi wakifahamu zaidi kuwa eneo hilo linaishia kwenye barabara inayotokea kona ya Kawe kuelekea Mbezi Beach kwa Zena, wengi wakidhani eneo hilo ni sehemu ya juu pekee au sehemu za mwanzo kwenye ghorofa ambazo awali ujenzi wake ulisimamishwa (japo sasa naona ujenzi ukiendelea).

Niwasanue eneo lilikuwa linafika karibia na ufukweni, kuna taarifa kutoka vyanzo vya ndani baada kudadisi ni kwamba limekuwa likigawiwa kinyemela kwa Vigogo (majina nayahifadhi) hususani kipindi cha hivi karibuni. Wengine tayari wameanza kuliendeleza na kufanya ujenzi binafsi.

Jambo la kushangaza, hakuna mchakato wowote wa wazi uliotangazwa kuhusu kuuza au kugawa maeneo hayo kwa Vigogo hao. Kwa sasa, ukipita eneo hilo na kufuatilia kwa wenyeji, utagundua kuwa kuna mchezo mchafu unaoendelea.

Natoa wito kwa mamlaka husika, ikiwemo vyombo vya uchunguzi, kufuatilia kwa kina mgawanyo huu wa maeneo ya umma kwenda kwa umiliki binafsi hasa kwa Vigogo. Utaratibu wa aina hii ukiachwa bila hatua za uwajibikaji utajenga mwendelezo wa kuporwa kwa maeneo mengine ya umma kutokana na uzembe wa wachache.

Wito wangu kwa mamlaka
Ni vyema Serikali kupitia NHC ikaweka wazi ramani ya eneo zima la Tanganyika Packers, ili kama kuna uwajibikaji na usimamizi wa kisheria, Wananchi wafahamu ukweli na kuondoa sintofahamu.

Nimeleta suala hili baada ya kufuatilia kwa kina na kutofurahishwa juu ya namna mali za umma zinavyochotwa na kumegwa na wachache bila taratibu za uwazi.

Pia soma:
~
Isihaka Mchinjita: ACT tukichukua nchi Tanganyika Packers Kawe halitokuwa eneo la Mwamposa kuombea watu wapate kazi
 
Acha wajenge ili tukivirudisha wapate hasara ya mabilioni, huwa nayaelewa mabossi yanapopita kwenye viwanja vyao yanakuta mnajenga wananyamaza ukikaribia kupiga lenta unakutana na bango simamisha ujenzi
 
Asante kwa taarifa, pia nasikitika kusema kuwa, hoja yako imetupiliwa mbali na mamlaka...
 
Wasichukue Chuo Cha Mwalimu Nyerere na Eneo la Navy Kigamboni ni vyangu.
 
Mkuu huo wito kwa mamlaka ipi? Zipi? Hasa kwa awamu hii ya kula kwa urefu wa kamba.
 
Back
Top Bottom