1. Viti vya daraja la kwanza vina nafasi ya kutosha, pia unaweza kuvilaza unavyotaka pindi unapotaka kulala au kupumzika.
2. Huduma za ndani ya ndege ni ya kiwango cha juu tofauti na daraja la kawaida. Mfano, abiria wanaosafiri daraja la kwanza wanapewa mvinjo tofauti na ujazo tofauti, vyakula pia wana uhuru wa kuchagua zaidi ya daraja la kawaida.
3. Hakuna msongamano kama kwenye madaraja mengine.
4. Bei ya kusafiri daraja la kwanza ni kubwa kuliko.
Pamoja na tofauti hapo juu, saikolojia ya daraja la kwanza na mengine ni uthibitisho wa ubinadamu wetu. Watu wengi wakiwa na vijisenti kidogo tofauti na wengine au madaraka yatokanayo na vyeo, tunapenapenda kuonyesha hela au vyeo kupitia tofauti hizi.
Binafsi sijaona umuhimu wa kusafiri daraja la kwanza toka nimeanza kusafiria ndege 2008. Sababu kubwa ni uwiano wa bei na pia mimi siyo mtu wa kupenda sifa au ulimbukeni.