Kuna faida gani ya kuendesha miradi iliyoanzishwa na wazazi?

Kuna faida gani ya kuendesha miradi iliyoanzishwa na wazazi?

Joined
Jan 26, 2019
Posts
87
Reaction score
113
Naomba kuuliza humu wanaJF mnsaidie.

Mimi ni kijana wa kiume 26yrs .Nimemaliza form six mwaka jana na mzee kaamua kutoniendeleza chuo ili tu nikafanye kazi kwenye miradi zake na ukiangalia katika familia tupo watoto 12.

Pia mzee ana mali nyingi tu.< ng'ombe 200, Na mradi wa mashine ya kukoboa mpunga, mashamba ya mpunga hekari 500 Na viwanja mbalimbali kama 12.

Binafsi mimi nilikuwa nimeamua kutoroka ili na mimi nikajaribu ku hustle lakini mzee kanirudisha.

JE KUNA FAIDA GANI AU NAWEZAJE KUJIWEKEZA NA MIMI ILI NIWE NA VYANGU?

Mzee wangu pia anabana sana kuwa na pesa mpaka akupe au umuombe
 
Penye miti hapana wajenzi,simamia miradi yake huku ukijipanga kupata mtaji wako hata kama kwa "kumpiga" mzee wako ili ukafungue mradi wako,connections na uzoefu utakao upata ktk miradi ya baba yako vitumie vizuri.
 
Acha upimbi, simamia mali za mzee wako, hakikisha zinazaliana, watafaidika wengi zaidi.
Jamii za wenzetu wanatoboa kwa kusimamia mali za familia.
Baba katola kwenye 0 mpaka 5, we unapaswa kuikamata 5 kusogea mbele, sio kuisusa hiyo 5, eti nawe unaenda kuanza 0. Huo pia ni ubinafsi.
 
Naomba kuuliza humu wanaJF mnsaidie.

Mimi ni kijana wa kiume 26yrs .Nimemaliza form six mwaka jana na mzee kaamua kutoniendeleza chuo ili tu nikafanye kazi kwenye miradi zake na ukiangalia katika familia tupo watoto 12.

Pia mzee ana mali nyingi tu.< ng'ombe 200, Na mradi wa mashine ya kukoboa mpunga, mashamba ya mpunga hekari 500 Na viwanja mbalimbali kama 12.

Binafsi mimi nilikuwa nimeamua kutoroka ili na mimi nikajaribu ku hustle lakini mzee kanirudisha.

JE KUNA FAIDA GANI AU NAWEZAJE KUJIWEKEZA NA MIMI ILI NIWE NA VYANGU?

Mzee wangu pia anabana sana kuwa na pesa mpaka akupe au umuombe
Huwa ukiwa Chuo ama Shule unaona Maisha marahisi sana na unahisi ukimaliza tu chuo utatoboa, ila uhalisia ni mgumu sana, kama una opportunity kama hio usiiachie unaweza kuja kujuta baadae.

Ushauri kama unahofia mambo ya Urithi na kuingiliwa kwenye maamuzi ongea na mzee wako akupe sehemu yako ambayo wewe utakua ndio unafanya maamuzi. Kama ni mashine ya kukoboa wewe uwe msimamizi.

Una opportunity ambayo wenzako wengi kwa mamilioni wanatamani waipate, usiiachie.
 
Watoto kumi na mbili,
Siku akienda Mbinguni huyo mzee wako utabaki mikono mitupu.

Fanya yako.
 
Watoto kumi na mbili,
Siku akienda Mbinguni huyo mzee wako utabaki mikono mitupu.

Fanya yako.
Akili zetu.

Kwanini usimshauri aite ndugu zake wakae chini washirikiane kuimarisha miradi yao iwanufaishe na watoto wao? Waarabu na wahindi wanawezaje?
 
Aisee kama mpo 12 hapo inabidi baba awaandae vizuri sana sio kukomaa na kusimamia mali za familia hafu mzee akifa kila mtu anataka chake pasu kwa pasu.
 
Huwa ukiwa Chuo ama Shule unaona Maisha marahisi sana na unahisi ukimaliza tu chuo utatoboa, ila uhalisia ni mgumu sana, kama una opportunity kama hio usiiachie unaweza kuja kujuta baadae.

Ushauri kama unahofia mambo ya Urithi na kuingiliwa kwenye maamuzi ongea na mzee wako akupe sehemu yako ambayo wewe utakua ndio unafanya maamuzi. Kama ni mashine ya kukoboa wewe uwe msimamizi.

Una opportunity ambayo wenzako wengi kwa mamilioni wanatamani waipate, usiiachie.
Kweli lakn alikuwa anataka aniweke pamoja na mdogo wangu kwenye mradi wa mashine ya mpunga Ndo nikawa nimetoroka nyumban
 
Mko watoto 12 na kila mmoja anatarajiwa kurithi mali hizo. Na sio kila mmoja atafanya kazi kuziendeleza, utafanya kazi miaka 10 mzee adondoke ndugu zako waliotafuta maisha yao waje kugawana sawasawa na wewe uliyetafuta na mzee. Fanya mawili.
Ama ukubaliane na mzee awe anakulipa kulingana na kazi yako au awe anakupa commission mfano mkivuna na kukoboa.

Ingekuwa ni more organised business ningesema mzee aanzishe kampuni mali zake zote utakazosimamia zihusishwe humo, achukue shares nyingi kama 70% wewe 30% kisha yeye kwenye wosia wake atasema 70% yake mgawanyo wake ukoje ila wewe 30% yako ibaki palepale hata usipoongezewa baadae. Mali kauli huwa zinakufa haraka kuliko mali za kwenye maandishi, kisheria na kimahesabu.

Najua lengo lake ni mali zake kuendelea, hii ya pili inazuia mali kugawanywa kwa wasio na akili na inaziweka pamoja, sio umempa huyu ekali 10 kauza 5 miaka 10 baadaye zile ekari 500 zimebaki 50 mnarudi kwenye umaskini wa asili. Na ana sababu za msingi kwanini kakutaka wewe kati ya 12.

Lengo ni kutoamini familia za watu weusi, si unaona mzee Mengi eti watoto wamefanya kazi miaka yote alafu wosia feki unasema wapewe buku.
 
Mostly likely inaelekea Mzee anakuona wewe ndio unaweza kusimamia hizo shughuli kwa sasa,; na hili sio jambo baya.
What if ikatokea Mzee anashindwa kuendelea na usimamizi labda kutokana na sababu mbali mbali kama ugonjwa... N.K; huoni miradi ndio itakufa !!
Huoni kuwa unapatiwa uzoefu na kufanyiwa maandalizi kwa wakati ujao (Mentorship) !!!
Ila Wahindi wako vizuri sana kwenye'FAMILY BUSINESS CONCEPT' na ndio maana miradi yao haifi kizembe.
 
Naomba kuuliza humu wanaJF mnsaidie.

Mimi ni kijana wa kiume 26yrs .Nimemaliza form six mwaka jana na mzee kaamua kutoniendeleza chuo ili tu nikafanye kazi kwenye miradi zake na ukiangalia katika familia tupo watoto 12.

Pia mzee ana mali nyingi tu.< ng'ombe 200, Na mradi wa mashine ya kukoboa mpunga, mashamba ya mpunga hekari 500 Na viwanja mbalimbali kama 12.

Binafsi mimi nilikuwa nimeamua kutoroka ili na mimi nikajaribu ku hustle lakini mzee kanirudisha.

JE KUNA FAIDA GANI AU NAWEZAJE KUJIWEKEZA NA MIMI ILI NIWE NA VYANGU?

Mzee wangu pia anabana sana kuwa na pesa mpaka akupe au umuombe
Unapowekewa jiwe la kukanyaga ili uvuke mto likanyage na uvuke.. Usilete kiburi cha kusema ntavuka mwenyewe bila kukanyaga jiwe hili.. Baba amekuwekea jiwe.. Ameona kitu ndani yako.. Shirikiana na baba yako.. Faida utaiona.. Shauriana na baba yako kuhusu haki zako katika kazi hiyo.. Usifanye kazi ya Bosi ndugu mshahara tonge.. Mzee akikuelewa maisha yataenda sawa.. Asipokuelewa ni sawa pia.. Ila akili kichwani.. Aliye jikoni si sawa na anayesubiri kuletewa mezani.. Ndio maana hata madada wa kazi huwa wananona kuwazidi hata wenye nyumba.. Jiongeze hapohapo utoke na mtaji wako hapohapo bila kuathiri biashara ya mzee..

Ukumbuke kuwa utakapoenda kupambana mwenyewe mapambano yatakuwa makali na yasiyo na huruma kwako jinsi ile utakavyopambana katika himaya iliyokwishaanzishwa.. Wenzetu wana biashara za familia na zinaajiri hata ukoo mzima.. Lakini sisi kila mtu anataka ubinafsi.. Hili ni tatizo kubwa sana kwetu sisi ngozi nyeusi.. Shirikiana na baba yako uwahi kutoka kimaisha..
 
Back
Top Bottom