Kuna faida katika kutoa sadaka na misaada kwa wahitaji/wanyonge

Kuna faida katika kutoa sadaka na misaada kwa wahitaji/wanyonge

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
4,014
Reaction score
4,600
SADAKA YA KUTOA MISAADA KWA WAHITAJI Yakobo 1:27
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu

Methali 19:17
Anayemsaidia maskini anamkopesha Mwenyezi-Mungu; Mwenyezi-Mungu atamlipa kwa tendo lake jema

Zaburi ya 41:1-3
• 1 Heri mtu anayewajali maskini; Mwenyezi-Mungu atamwokoa wakati wa shida.
• 2 Mwenyezi-Mungu atamlinda na kumweka hai, naye atafanikiwa katika nchi; Mungu hatamwacha makuchani mwa maadui zake.
• 3 Mwenyezi-Mungu atamsaidia awapo mgonjwa, atamponya maradhi yake yote.

Maana kwa Ufupi

• Kuwajali wanyonge/maskini: Kusaidia au kuwakumbuka watu walio katika uhitaji kunaleta baraka na ulinzi wa Mungu.

• Wakati wa shida na ugonjwa: Mungu anaahidi kusaidia, kulinda, na kuwategemeza wale wanaowatendea wengine wema, hata wanapokuwa wagonjwa au kwenye magumu.

Mdo 20:34-35
Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.

Blessed is the hand that giveth than the one that taketh(the hand that giveth)

Mathayo 25:32 mpaka 40. Mstari wa 40 unatoa jibu kuu ambalo ndilo siri kubwa ya ufalme wa mbinguni kuhusu matendo ya huruma:
32 Mataifa yote duniani watakusanyika mbele zake. Kisha atawatenganisha watu katika makundi mawili kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi.
33 Atawaweka kondoo upande wake wa kuume na mbuzi upande wake wa kushoto.
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kuume, ‘Njoni ninyi mliobarikiwa na Baba yangu. Urithini ufalme mlioandaliwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
35 Nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkanipa maji ya kunywa, nilikuwa mgeni mkanikaribisha nyumbani kwenu.
36 Nilikuwa sina nguo mkanivisha, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nilikuwa gerezani mkaja kunitembelea.’
37 “Kisha wale wenye haki watamjibu wakisema, ‘Bwana, ni lini tulikuona una njaa tukakupa chakula, au una kiu tukakupa maji ya kunywa?
38 Ni lini tulikuona ukiwa mgeni tukakaribisha nyumbani kwetu, au ukiwa huna nguo tukakuvisha?
39 Ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au gerezani tukaja kukutazama?’
40 Mfalme atawajibu, ‘Amin, nawaambia, kwa kuwa mlitenda neno hili kwa mmoja wa hawa ndugu zangu walio wadogo kabisa, mlitenda kwangu.’

Waebrania 13:2.
Aya hiyo kamili inasema:
"Msisahau kuwakaribisha wageni, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, watu wengine waliwakaribisha malaika pasipo kujua."

Luka 3:11,
"Akajibu akawaambia, Mwenye nguo mbili na ampe asiye na nguo; na mwenye chakula na afanye vivyo hivyo."

Luka 12:15,
"Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo."

Luka 9:25)
"Kwani itamfaa mtu nini kuupata ulimwengu wote, kama akipata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?"

1 Petro 4:8.
upendo mwingi ninyi kwa ninyi; kwa sababu upendo husitiri wingi wa dhambi."

Hakuna UPENDO bila kutoa,UPENDO hukamikishwa na kutoa au kujitoa.Yohana 3:16,
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee,

Luka 6:38,
"Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa, hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa kifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa."

SADAKA ZAKO HUWA ZINAONGEA MBELE YA KITI CHA REHEMA BADALA YAKO HATA KIPINDI WEWE UMENYAMAZA AU UMESAHAU
Matendo ya Mitume 10:4.
Aya hiyo kamili inasema:
"Akamkazia macho, akaogopa, akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu."

Na unaweza kumkumbusha Mungu kama mfalme HEZEKIA
Unaruhusiwa kupeleka HOJA zako kwa Mungu,sio malalamiko au manunguniko peleka HOJA zenye mashiko mbele ya Mungu

Isaya 41:21.

"Leteni hoja zenu, asema Bwana; toeni sababu zenu zenye nguvu, asema Mfalme wa Yakobo."

Isaya 38:3 na pia 2 Wafalme 20:3.

"Ee Bwana, kumbuka hayo sasa, nakusihi, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia kwa majonzi mengi."(HII NDIO ILIKUWA HOJA YAKE ALIYOIOELEKA MBELE ZA MUNGU

Isaya 38:5 na 2 Wafalme 20:6.
Mungu alimjibu Hezekia kwa maneno haya kupitia Nabii Isaya:
"Nenda, ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako, asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zake miaka kumi na mitano."

SOMO LA SADAKA: SEHEMU YA KWANZA

SADAKA ni kitu chochote Cha halali Cha kwako WEWE unachomiliki chenye THAMANI KWAKO wewe unayeokitoa(kisiwe kilema,kisiwe kibovu,kisiwe kigonjwa,kisiwe mapooza,kisiwe ambacho huna KAZI nacho) unachokitoa kwenye madhabahu unayoitumainia/iamini WEWE,ZIPO madhabahu za aina kuu mbili ya Mungu WETU YAHWE na za miungu ya Giza za miungu,mizimu,waganga WA kienyeji,matambiko n.k)

Sadaka ni kitendo cha rohoni* kwanza kwani tunatoa kwa **imani. Kumbuka imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo (Warumi 10:17). Imani ni kuwa na uhakika na mambo yatarajiayo (Waebrania 11:1). Kwa hiyo ili uwe na uhakika katika utoaji sadaka, lazima uwe na neno linalohusu sadaka ili Mungu akisema nawe jinsi ya kutoa sadaka uweze kusikia.

Kama huna neno la Kristo juu ya sadaka, huwezi kusikia Mungu akisema nawe jinsi ya kumtolea. Biblia imetoa maelekezo jinsi ya kutoa sadaka hivyo ni vigumu kutolea Mungu sawa sawa na mapenzi yake kama huna hufahamu maandiko yanasema nini juu ya sadaka. Kumbuka usiende mbele za Bwana mikono mitupu (Kumbukumbu 16:16) na pia mtolee Mungu kadri alivyokubariki (Kumbukumbu 16:10).

KWANINI TUNATOA SADAKA
1) Kumshukuru Mungu kwa yote na vyote ikiwemo kutuumba,kutupa,uhai,kwa neema na rehema kwa kila kitu,hata kama tunapitia MAJARIBU ama changamoto tuna Imani ni za muda TU Mungu WETU anaweza kutuokoa,IMANI KUMWAMINI Mungu WETU katika kila jambo
Hata kama hujaongea maneno kile kitendo ukipeleka sadaka tu madhabahuni MAANA yake una maanisha Mungu nakushukuru kwa kinibariki katika KAZI ZANGU (inabidi iwe KAZI halali,sio ukahaba,sio wizi,sio rushwa,sio dhuluma) hivyo nimekuletea sehemu ya baraka ulizonibariki kama ASANTE YANGU KWAKO.

2) Kumuheshimu na kumtumikia Mungu kwa mali zetu

3)Kumpenda Mungu WETU , UPENDO ni kutoa,kumuamini(IMANI) ,hata Mungu alitupenda ulimwengu hata akamtoa mwana wake WA PEKEE,UPENDO ni kutoa na kujitoa kwa wengine,kumpenda Mungu ni kujitoa kutoa kwa Mungu na kwa jirani zetu(kuwapenda wanadamu wenzetu,na kusikia NENO lake na KUTII.
Utii wa NENO la MUNGU ni Bora kuliko dhabihu iliyo nona. Mfalme SAULI alitoa sadaka vibaya bila utii,akavuna LAANA badala ya baraka.
1 Sam 15:22
Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

Kinachofanya sadaka yako iwe sadaka ni imani yako kwa Mungu. “Kwa imani Habili alimtolea dhabihu iliyo bora kuliko Kaini (Waebrania 11:4). Unaposikia neno la Mungu juu ya sadaka linatakiwa likupe uhakika juu ya maelekezo ya Mungu jinsi gani umtolee sadaka. Ukishakuwa na uhakika ndipo unaweka katika matendo kwani imani pasipo matendo imekufa (Yakobo 2:26).

Ili uwezi kumpendezesha Mungu katika utoaji wako lazima utoe kwa imani. Maandiko yanatuambia “pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu” (Waebrania 11:6). Usitoe sadaka kidini au kidhehebu ila toa sadaka kwa imani.
Hivyo soma sana biblia juu ya sadaka kwani ukishajenga imani jinsi ya kumtolea Mungu huhitaji mtu kukuhimiza kutoa.

Kuna uhusiano kati ya moyo wako na sadaka yako. Mungu akitaka kuujua moyo wako, anaangalia utoaji wako. Maandiko yanasema weka hazina yako mbinguni kwani hazina yako ilipo ndipo moyo wako upo (Matayo 6:20—21). Kitu kikubwa ambacho Mungu anataka siyo sadaka yako ila moyo wako kwanza. Moyo wako ukiwa kwake na sadaka yako itakuwa kwake.

Hivyo kitu cha msingi kabisa ni kujitoa maisha yako kwa Mungu na kumruhusu Yesu Kristo atawale maisha yako. Sadaka yako mbele za Mungu haina maana kama hujautoa moyo wako kwa Mungu. Maandiko yanasema “Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA” (Methali 15:8).

Kwa hiyo sadaka ya kwanza ya kumtolea Mungu ni roho na ya pili utoe mwili wako kama dhabihu kwake. Yesu alitupenda na kujitoa kama sadaka na dhabihu kwa Mungu (Waefeso 5:2). Vivyo hivyo yatupasa nasi tuitoe miili yetu kwa Mungu kwani ndio dhabihu iliyo hai (Warumi 12:1).

Hivyo kitu cha msingi zaidi ambacho kanisa inatakiwa ihimize ni watu kuacha njia zao mbaya na kumrudia Mungu ndipo watu wafundishwe juu ya sadaka. Tutengeneze kwanza maisha yetu na Mungu ndipo tutoe sadaka. Yesu anasema “basi ukileta sadaka yako mbele ya madhabahu, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iacha sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako” (Matayo 5:23—24).

Moja ya kazi za Roho Mtakatifu ni kutuongoza (Warumi 8:14). Hivyo inapofika kwenye utoaji wa sadaka, Roho Mtakatifu atakuongoza wapi pa kutoa na jinsi ya kutoa. Moja ya vitu sadaka inaachilia ni wewe kukubalika kwa Mungu (Walawi 19:5). Lakini Mungu hakukubali kwa sababu tu umetoa sadaka ila kwa sababu umetoa sawasawa na maelekezo aliyokupa. Ndio maana ni muhimu sana kujua wakati Mungu anaongea na wewe.

Sadaka haipelekwi mahali popote ila pale ambapo kuna jina lake au uwepo wa Mungu (Kumbukumbu 12:11). Maandiko yanatutahadharisha kutoa sadaka mahali popote (Kumbukumbu 12:13) ila tupeleke mahali Mungu amepachagua. “Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni [makao yake], elekezeni nyuso zenu [hapo], nawe uende [huko]; pelekeni [huko] sadaka zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo (Kumbukumbu 12:5—6).

Hivyo inapofika kwenye suala la utoaji sadaka, Mungu lazima akupe maelekezo ya wapi pa kutoa na jinsi ya kutoa. Muhimu zaidi hakikisha jina lake lipo hapo. Usipeleke sadaka yako mahali ambapo jina lake halipo. Usitoe sadaka kwa sehemu kwa sababu umeona kila mtu anapeleka hapo.

Pia sadaka inatakiwa iwe siri yako wewe na Mungu. Yesu anasema utoapo sadaka hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume (Matayo 6:3). Dini zingine zinaweka mfumo wa utoaji ambao siyo haupo kwenye maandiko. Ukiona unatoa kiasi kikubwa kwa sababu ya mfumo dini yako imeweka, haumtolei Mungu kibiblia ila unatoa kidini. Unatakiwa utoea jinsi Mungu alivyokubariki na kadri Roho Mtakatifu anavyokuongoza.

Anayetakiwa kujua sadaka yako ni Mungu. Kitu ambacho Mungu anaangalia katika sadaka siyo kiasi unatoa ila imani yako. Unaweza kutoa kiasi kikubwa na Mungu asiikubali sadaka yako na mwingine akatoa kiasi kidogo lakini Mungu akaipokea. Mjane alitoa kiasi kidogo lakini sadaka yake ilikuwa kubwa kuliko zote (Marko 12:41—44).

USITOE SADAKA KWA KULAZIMISHWA,USITOE KWA MOYO WA HUZUNI*
2 Wakorintho 9:7, unaosema: "Kila mtu na atoe kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu (au kwa kupenda)."

KISA CHA ANANIA NA SAFIRA
Anania na Safira ni wanandoa waliokuwa waumini wa kanisa la kwanza huko Yerusalemu, ambao kisa chao kimeandikwa katika Matendo ya Mitume 5:1-16 kwenye Biblia.

Matukio Makuu ya Kisa Chao

• Kuuza Mali: Waliamua kuuza shamba lao ili wachangie fedha kwa ajili ya kanisa, kama walivyokuwa wakifanya waumini wengine.

• Kusema Uongo: Walikubaliana kuficha sehemu ya fedha za mauzo ya shamba hilo, huku wakijifanya kuwa wametoa kiasi chote cha pesa walizopata.

• Kukabiliwa na Petro: Mtume Petro alimwambia Anania kuwa hakumdanganya mwanadamu bali alimdanganya Mungu na Roho Mtakatifu, kwa kuwa hawakulazimishwa kutoa fedha hiyo yote—ilikuwa hiari yao.

• Vifo Vyao:
• Anania alianguka chini na kufa pale pale alipofichua au kusikia maneno hayo.
• Baada ya saa tatu, mke wake Safira akaingia bila kujua kilichomtokea mumewe; Petro alipomuuliza kuhusu bei ya shamba, yeye pia alidanganya, kisha akaanguka chini na kufa.

Somo la Kisa Hiki*

• Kisa hiki kinasisitiza uaminifu, hofu ya Mungu, na kwamba unafiki au kujaribu kuonyesha watu kuwa unafanya jambo kubwa la kiroho wakati moyoni una Imani hiyo,haupo tayari,unataka upate SIFA mbele za watu tu kwa udanganyifu kunaweza kuleta madhara makubwa KWAKO,ukavuna LAANA badala ya baraka.

Mtu haamui jinsi ya kutoa sadaka wala dini/kanisa haiamui jinsi watu watoe sadaka. Mungu ndiye anatoa maelekezo jinsi ya kumtolea. Malekezo haya ni binafsi kwani watu wamebarikiwa tofauti. Kanisa inapoweka kiasi cha utoaji kwa kila mtu, hiyo haipo kwenye biblia. Unaweza kusema “kipindi cha Musa walikuwa wanaambiwa watoe nini na nini.”

Kipindi cha Musa watu waliishi chini ya sheria ila sisi tunaishi kwa imani (Warumi 1:17) kwani sheria imeandikwa katika mioyo yetu (Waebrania 10:16). Kumbuka Yesu Kristo ndiye Kuhani Mkuu wetu na “kila kuhani mkuu huwekwa ilia toe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima naye awe na kitu cha kutoa. Kama angekuwa juu ya nchi asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria” (Waebrania 8:3,4).

Lakini maandiko yanatuambia Yesu ni mjumbe wa agano lililo bora zaidi kwani kama agano la kale lisingekuwa na mapungufu, kusingekuwa na nafasi ya agano jipya (Waebrania 8:6,7). Hivyo sheria ya kutoa sadaka ipo pale pale ila tofauti ni kwamba sisi tunatoa kwa imani. Ndo maana lazima uwe unasoma agano la kale kwa jicho la agano jipya.

Hivyo jenga imani yako juu ya utoaji sadaka ili utoe kadri ya maelekezo Mungu anakupa. Kufuata maelekezo ya Mungu katika utoaji sadaka ni muhimu sana kwani unaweza kutoa sadaka na Mungu akaikataa (Mwanzo 4:5).

Watu wengine wanatoa hera kanisa badala ya kutoa sadaka kwa Mungu. Mungu hahitaji hera yako kwani kila kitu ni mali yake (Zaburi 24:1). Hivyo usitoe sadaka kwa sababu tu umehimizwa na mhubiri au kanisa ila toa kwa sababu umepata maagizo kutoka ya utoaji kwa Mungu. Mungu anaweza kumtumia mhubiri kukupa maelekezo jinsi ya kutoa lakini hakikisha kuwa yanaendana na neno lake.

Mungu hawezi kukupa ujumbe nje ya neno lake. Hivyo ukiona mhubiri anakupa maelekezo ya utoaji sadaka ambao haupo kwenye biblia hiyo sauti ya Mungu. Kuna watumishi wanakuambia toa kiasi fulani ili Mungu afungue milango ya baraka na usipotoa huwezi kubarikiwa. Lakini maandiko yanasema tayari tumebarikiwa na baraka zote za rohoni (Waefeso 1:3).

Ndio maana ni muhimu neno la Kristo likae ndani yako katika hekima yote (Wakolosai 3:16) ili wewe mwenyewe uweze kusikia sauti ya Mungu. Kuna watumishi wanaweka mifumo ya kukusanya hera kinyume na neno la Mungu.

Kuna sadaka za aina nyingi. Mfano sadaka ya hiari, nadhiri, zaka, malimbuko, mbegu, na zingine ila leo tuangalie sadaka za aina mbili:

1. SADAKA YA NADHIRI: Nadhiri ni sadaka ambayo unamuahidi Mungu kwa kinywa chako (Kumbukumbu 23:23). Kwa mfano unaweza kumwambia Mungu “Mungu ukinifanikisha katika biashara yangu, nitakutolea hiki na hiki.” Sadaka ya namna hii inaitwa “nadhiri.” Sadaka ya nadhiri ni sadaka ambayo inafunga nafsi yako (Hesabu 30:2).

Ukiweka nadhiri kwa Bwana hakikisha umeiondoa ili kuondoa kifungo cha nafsi yako (Walawi 27:2). Unapoweka nadhiri kwa BWANA tayari inakuwa sheria ambayo unatakiwa uifuate sawasawa na jinsi hiyo sheria ilivyo (Hesabu 6:21). Hivyo huwezi kuweka nadhiri katika kanisa A halafu ukaenda kuitoa kanisa B.

Maandiko yanatuambia “Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuindoa, kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako” (Kumbukumbu 23:21). Hivyo ukiweka nadhiri Roho Mtakatifu atakukumbusha.

Kama Roho Mtakatifu akikukumbusha juu ya nadhiri ambayo umeiweka wewe ukapuuza au ukashindwa kusikia, atakuja kukudai kama dhambi na maandiko yanatuambia mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23). Hivyo usiweke nadhiri kama njia ya kumtaka Mungu afanye kitu kama maisha yako halafu hutoi. Weka nadhiri kwa sababu unamwamini Mungu wako kuwa anaweza kukufanikisha katika jambo lolote na usisahau kuiondoa nadhiri yako kwani nadhiri inafunga nafsi yako.

2. SADAKA YA ZAKA: Hii siyo sadaka ya hiari. Maandiko yanatuambia kuwa zaka ni ya BWANA. Zaka siyo sadaka ambayo wewe unamtolea Mungu. Zaka ni mali ya BWANA ambayo ipo mikononi mwako. Maandiko yanasema mwanadamu anaweza kumuibia Mungu (Malaki 3:8). Huwezi kuiba kitu ambacho ni chako. Ile kwamba unaweza kuiba, maana yake siyo chako.

Hivyo 10% ni ya BWANA. Mungu ametoa maelekezo kuwa peleka zaka katika “nyumba ya Bwana” (Malaki 3:10. Kumbuka “zaka ni ya BWANA. “Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA” (Walawi 27:30). Hivyo usitoe zaka na fikra ya “naenda kumtolea Mungu” bali “nampa Mungu vilivyo vyake.” Yesu alisema “mpeni Mungu yaliyo ya Mungu” (Marko 12:17).

Watu wengi huwa wanapata shida “kuamua” wapi pa kupeleka zaka. Zaka huamui wapi pa kuipeleka ila unaipeleka kwenye “nyumba ya Bwana.” Watu wengine huwa wanauliza “nikitoa zaka kwa yatima na wajane ni vibaya?” Kumbukumbu 26:12—14 inatoa jibu. Hakikisha umeelewa kitu Mungu anasema katika mistari hii. Ukiona wewe ndiwe unaamua pa kupeleka zaka, unamuibia Mungu.

Hesabu 18:21 inatuambia “Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israel kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.” Walawi hawakuwa na urithi katika Israel ila Mungu ndio alikuwa urithi wao (Hesabu 18:20). Kwa hiyo zaka ndio ilikuwa urithi wao (Hesabu 18:26). Hivyo unaweza kumpatia zaka mlawi kwani zako ni ya Mungu na Mungu ndio urithi wao.

Je natumia njia gani kuamua jinsi ya kumtolea Mungu? Ukitaka kujua kama unavyotoa ni sawa na mapenzi ya Mungu au la jiulize swali hili: Ukiwa unaenda kutoa sadaka yako ghafla Yesu akatokea karibu na kitunga cha sadaka na macho yake yapo kwenye mkono wako, je bado utakuwa na ujasiri wa kutoa kile ulichokuwa unaenda kumtolea?

Kama ujasiri utapotea na utatamani uongeze, basi hautoi sadaka kwa imani. Hivyo rudi kwenye maandiko mpaka upate uhakika ili uweze kutoa sawasawa na mapenzi yake. Sadaka ambayo unaitoa na Mungu haipokei umepoteza hera. Hivyo kabla ya kutoa sadaka, kuwa na uhakika umepata maelekezo yote na kuwa Mungu ameipokea sadaka yako.

Sehemu ya pili tutaangalia baadhi ya sababu za kutoa sadaka. Kama Mungu hajapokea sadaka yako, sababu ya wewe kutoa sadaka inakuwa haipo. Hivyo kile ambacho sadaka inatakiwa iachilie katika ulimwengu wa roho juu maisha yako hupati. Lakini je unajuaje kama sadaka yako imekubalika mbele za Mungu au haijakubalika? Itaendelea…

“Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya” (Methali 3:9—10
 
Blessed is the hand that giveth.(Mkono unaotoa ndio unaobarikiwa,ni heri kutoa kuliko kupokea.
 
Attachments

  • 45725.jpeg
    45725.jpeg
    52.2 KB · Views: 7
Sijalisoma bandiko mpaka mwisho….nikifika maskani nitalimzalizia lakini nimeona mada hii inanihusu au kunigusa moja kwa moja.

Tangu wakati nikiwa mdogo mpka lei hii japo sijawa mkubwa sana kiasi cha kusema nimekua lakini ni kama nina bahati ya kupata zaidi ya mahitaji yangu ya muhimu saana ivo ninaweza kusema moja kwa moja ni mtoaji kwa kitambo kidogo pia me sio shabiki kindaki wa falsafa za kale ya mashariki ya kati.
By default naona kuna wale watu by nature wameumbwa kutoa na sio kupokea mfano me hua n mzito sana kuomba na endapo nikiomba huishia kwenda apeche pro max tofauti na nikitoa hua napata zaidi ya nilichonacho baada ya kutoa hii nishawai ifanyia personal research sijajua kwa wengine

Swali kwa wanaulumbi…mama yangu mzazi ambae ni mfuasi kindaki wa falsafa za mashariki ya kati na imani zisizo rasmi hua ananisihi sana kutoa mdhabahuni akiamini kua madhabahu yana nguvu compare na nikiwapa wahitaji…,ninaomba kupata ufafanuzi wa suala hili pasi na falsafa nikimaanisha pamoja na majumuisho wa uhalisia kutokana na jamii/mazingira yanayotuzunguka.
 
KUTOA madhabahuu ni suala la kiimani na kiroho na Lina utaratibu wake,kwa kuwa umesema huna Imani inakuwa ngumu KUMPENDEZA Mungu pasipo Imani...na Mungu anaangalia zaidi moyo WAKO..hatua ya kwanza ni IMANI ya pili ni moyo WAKO u surrender kwa Mungu..

Kwa WEWE usiye na Imani kwa Mungu nakushauri uendelee na kutoa SADAKA za KUSAIDIA WAHITAJI MASIKINI mana hiyo utabarikiwa TU kwa sababu ni SHERIA YA MUNGU ni ahadi yake ,hii ni kwa Wanaoamini na wasioamini Ina cut across

Mana hata wachawi, fremansory,waganga WA kienyeji nao wanapeana mashrti ya kutoa MISAADA sadaka KWA WAHITAJI MASIKINI,WANYONGE,walemavu,wajane,wagonjwa wafungwa n.k(katika MFUMO WA NJIA mbili kuna wanafanya kama ni HISANI au Matendo ya HURUMA TU kwa moyo na kuna wanafanya kama sehemu ya KAFARA MAKAFARA ya KUSAIDIA MASIKINI watu WA Imani za kishetani kama waganga WA kienyeji fremansory wao wanaota charity group..NA WANABARIKIWA kwa sababu ni SHERIA ahadi ya Mungu mkono unaotoa ndio unaobarikiwa kuliko unaopokea.

Advantage ya kutoa madhabahuni unakuwa connected na nguvu ya madhabahu spiritual power ya madhabahu unayoitumikia kama ninya Mungu,ila KWA Imani, kiroho,kwa moyo kwa utaratibu maalumu,hasa kwa muumini ambaye ameyatoa maisha yake moyo na mwili KUMTUMIKIA MUNGU..

SADAKA inakuwa sehemu ya IBADA.

summary
SADAKA na madhabahu zinatumika katika pande zote mbili upande WA Mungu Nuru na upande WA Giza
Na MFUMO unafana kwa sababu shetani anaiga MFUMO WA Mungu.
Na pande zote zinatoa sadaka .

SHAURI NI BORA UCHAGUE UPANDE MMOJA EITHER UWE KWA MUNGU AU SHETANI (na upande utakao kuchagua ukomae nao KWELI KWELI usiwe vugu vugu.
Ila katika hizo pande mbili (UPANDE WA MUNGU UNA NGUVU ZAIDI NA UNA AMANI,FURAHA,UPENDO,UTU WEMA,FADHILI...na uhakika WA UZIMA WA MILELE afterlife baada ya MAISHA ya DUNIANI una uhakika WA kurithi UFALME WA MILELE WA mbingu.

Mimi nazijua pande zote mana nilianzia UGANGA WA KIENYEJI nikaja nikaokoka ,KWA SHETANI kuna mateso ila KWA YESU kuna RAHA NA AMANI,UPENDO,FURAHA ,NA UZIMA WA MILELE.

Ukiwa KATIKATI ni as good as upo kwa shetani TU.YESU ANAKUPENDA alikufa masalabani kwa AJILI YETU akafufuka siku ya tatu sasa yu hai,kwa AJILI ya dhambi zetu,ili mateso YETU,mizigo YETU , maumivu YETU ,shida zetu zote azichukue atusamehe dhambi zetu,TUPATE UZIMA WA MILELE.

YESU ANAKUPENDA.
 
SUMAARY FUPI ZAIDI
Ukiwa connected na madhabahu hata Ile SADAKA ya kuwapa MASIKINI WAHITAJI nayo inakuwa connected na madhabahu Yako unayoabudia,
Kuwa connected na madhabahu sio lazima upeleke madhabahuni per say ,ila Ile nguvu ya kiroho inayotoka madhabahuni inaweza kukupa muongozo uwapelekew yatima,MASIKINI... wagonjwa,n.k,nguvu ya ROHO ya madhabahu inakuwa ndani YAKO ni kama Roho WA Mungu INAYO ku connect popote utakapo kuwa utakapoto sadaka

Hata WAGANGA WA kienyeji,fremansory na wachawi
Wanaota sadaka KWA WAHITAJI, charity group,lakini wakiwa connected na madhabahu za vilinge vya waganga WA kienyeji,na kuzimu, lucifer gerefokale..kama MAKAFARA..mfano wanaweza wakachinja ngamia au wanyama wakapita kugawa nyama mitaani kwa watu zikiwa kama MAKAFARA yaliyofanyiwa ritual matambiko au kunenewa maneno kunuiziwa katika spiritual realm,mana Ile nguvu ya madhabahu inakuwa ndani yao ni Roho chafu ya mapepo
 
Mama Yako amekushauri vizuri sana ,NI LAZIMA UWE NA MADHABAHU UNAYOITUMIKIA ,ndiyo itakavyokuwa inakupa nguvu.
Amekushauri UCHAGUE madhabahu ya Mungu,amekushauri UCHAGUE fungu jema,msikilize na KUMTII mzazi WAKO.
 
MAFANIKIO NI YA KIROHO nguvu ya madhabahu unayoabudia ndiyo inayoachilia MAFANIKIO,
kwa pande zote ,walioko Giza wanaotegemea mizimu matambiko,ndio mana utaona wanatambika kila baada ya muda hata mara moja kwa mwaka,ikifika mwezi WA 12 Xmas utaona wanaenda wengine kuaga nyumbani kwako,kwa wazee WA Mila na tamaduni,hizo ni madhabahu pia za mizimu ya ukoo.
Wakimaliza kula Xmas wanarudi mjini kwenda kufanikiwa sasa mpaka mwakani Tena na cycle repeats continuously

Hata wachawi anapokuja kululoga
Lazima apokee nguvu kutoka kwenye madhabahu yake VIZIMBA.VYAKE na Huwa wanavitolea MAKAFARA sadaka ili madhabahu zao ziwe na nguvu

NA WEWE LAZIMA UWE NA MADHABAHU
Na madhabahu Yako unakula sadaka ,sadaka zako zinaipa nguvu madhabahu Yako ili IACHILIE NGUVU KWAKO
Maombi pia ,IMANI kwa Mungu ,na NENO la MUNGU..hizi ni baadhi ya SILAHA ,ila sadaka Ina IMARISHA MADHABAHU YAKO.

KUWA NA MADHABAHU NI SUALA LA MUHIMU SANA KIROHO...MSIKILIZE MAMA YAKO AMEKUSHAURI VIZURI SANA.

na pengine maombi yake mama Yako,na nguvu ya madhabahu ya mama Yako ,pia inakusaidia na WEWE kwa sababu ya maombi na madhabahu ya mama Yako kuna namba Ina ku sustain.
 
NGUVU YA MADHABAHU INAKUWA NA WEWE POPOTE UTAKAPOKUWA SIO LAZIMA UWE ENEO LA IBADA,NA CHOCHOTE UTAKACHOKIFANYA AMBACHO NI MATAKWA YA MADHABAHU YAKO..KINAONGEZA NGUVU KWENYE MADHABAHU YAKO.(kama sadaka wahitaji,MASIKINI).

Japo hata kama huna madhabahu bado utabarikiwa TU vilevile mana ni ahadi ya Mungu,ila ni vizuri zaidi ukiwa na madhabahu.
 
MAFANIKIO NI YA KIROHO nguvu ya madhabahu unayoabudia ndiyo inayoachilia MAFANIKIO,
kwa pande zote ,walioko Giza wanaotegemea mizimu matambiko,ndio mana utaona wanatambika kila baada ya muda hata mara moja kwa mwaka,ikifika mwezi WA 12 Xmas utaona wanaenda wengine kuaga nyumbani kwako,kwa wazee WA Mila na tamaduni,hizo ni madhabahu pia za mizimu ya ukoo.
Wakimaliza kula Xmas wanarudi mjini kwenda kufanikiwa sasa mpaka mwakani Tena na cycle repeats continuously

Hata wachawi anapokuja kululoga
Lazima apokee nguvu kutoka kwenye madhabahu yake VIZIMBA.VYAKE na Huwa wanavitolea MAKAFARA sadaka ili madhabahu zao ziwe na nguvu

NA WEWE LAZIMA UWE NA MADHABAHU
Na madhabahu Yako unakula sadaka ,sadaka zako zinaipa nguvu madhabahu Yako ili IACHILIE NGUVU KWAKO
Maombi pia ,IMANI kwa Mungu ,na NENO la MUNGU..hizi ni baadhi ya SILAHA ,ila sadaka Ina IMARISHA MADHABAHU YAKO.

KUWA NA MADHABAHU NI SUALA LA MUHIMU SANA KIROHO...MSIKILIZE MAMA YAKO AMEKUSHAURI VIZURI SANA.

na pengine maombi yake mama Yako,na nguvu ya madhabahu ya mama Yako ,pia inakusaidia na WEWE kwa sababu ya maombi na madhabahu ya mama Yako kuna namba Ina ku sustain.
Asante kwa somo zuri siku ya leo
 
Hakuna dhaka siku hizi,inabaki kuwa sadaka ya hiyari.sadaka zote agano jipya ni za hiyari ndugu yangu
 
Kuna mafundisho mengi yanayowakataza watu kutoa ZAKA na wengine wanawashauri Watu watu wale wenyewe sehemu za ZAKA.
Hayo yote ni mafundisho potofu,ya mpinga KRISTO..LENGO la hayo mafundisho yanayokataza watu wasitoe ZAKA ni kuwwondolea waumini nguvu ya SADAKA YA ZAKA,
ULINZI zaka inaweka ULINZI WA mali zako,afya Yako,ZAKA NI MWISHO WA YOTE ukimjaribu Mungu JARIBU UONE ukitoa ZAKA kwa uaminifu , Mungu anakufungulia madirisha ya mbinguni MVUA YA BARAKA ITAKUNYESHEA ,ULINZI WAKO UTAIMARISWA NA ULINZI WA MALI ZAKO NA KAZI YAKO BIASHARA YAKO.

KWA UZOEFU WANGU
SADAKA MBILI AMBAZO NIMEONA ZOTE ZINA NGUVU SANA
1)ZAKA
2)KUSAIDIA MASIKINI WAHITAJI WASIOJIWEZA

ZAKA ni mwisho WA YOTE..wachawi HAWAPENDWI ujue nguvu ya kutoa SADAKA ya ZAKA ,ndio mana kuna mafundisho mengi ya kupinga watu wasitoe ZAKA ,kwa sababu ZAKA Ina baraka nyingi na uliinzi KWAKO,Tena UNAPATA MATOKEO NDANI YA MUDA MFUPI Yani ukitoa ZAKA kwa uaminifu ,NDANI YA MIEZI MICHACHE TU 3-6 UNAPATA MAJIBU YAKO UTAONA MABADILIKO..

hata wachawi watakukimbia unakuwa HAUSHIKIKI HAUGUSIKI kiroho,ZAKA NI HATARI...

NDIO MAANA INAPIGWW VITA WATUBWASIPATE MAARIFA YA KUTOA ZAKA.
 
Hata watoto WAKO ukiwatolea ZAKA ni vizuri,we wape tu watoto WAKO SADAKA ZAKA..utawasaidia..ZAKA ..INA FAIDA SANA KIROHO.
 
Back
Top Bottom