GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
GENTAMYCINE hivi ni kwanini Siku hizi hapa Kwenu nchini Tanzania kila kukiwa tu na Shughuli ya Kitaifa Uhuru au Muungano au Mapinduzi mnapenda mno Kuwaonyesha Makomandoo wenu wakifanya Mambo ya Kimedani?
Hii ina faida gani hasa kwa Watanzania wengi wasio na uhakika wa hata Maisha yao na wengine Wanataabika tu? Na mbona wakati wa Awamu za Kwanza ya Nyerere, ya Pili ya Mwinyi na ya Tatu ya Mkapa hatukuona hivi?
Lakini ni kwanini tumeanza kuyaona yakizuka katika Awamu ya Nne ya Kikwete, Awamu ya Tano ya Magufuli na inayosemekana Awamu ya Sita ( wakati bado ni ya Tano ) ya Rais Samia?
au labda kuna nchi mnaviziana nazo Kivita hivyo kwa Kupenda Kwenu kila mara Kuwaonyesha hawa Makomandoo huenda mnawatumia Ujumbe indirectly ili labda Wawaogope?
Na je, kana mnawaonyeshea hawa Makomandoo wenu kila mara ili kuwatishia / kuwatisha mna uhakika kuwa Wao hawana Makomandoo imara pengine maradufu ya hawa Wenu ila wameamua tu Kunyamaza na huenda Wanawasanifu na Kuwadharau au hata Kuwaona ni Washamba?
Tafadhali nijibuni upesi ili nami nimtafsirie hapa kwani ana Shauku ya kupata Majawabu na Mimi GENTAMYCINE nimemwambia siyo Great Thinker kama Yeye bali ni 'Popoma' tu niliyetukuka, hivyo kwakuwa nyie JF Members wote hapa ni 'Great and Critical Thinkers' naamini mtaserereka na kutiririka na Madini yenu ili nimfahamishe nae.