Kuna gari hizi, suzuki escudo old, Rav4 old na spacio new 1490 cc toeni ushauri

Duuu! Sawa haya kati ya hizo mbili rav4 na hiyo suzuki hasa katika swala la mafuta na spare maana kuhusu uimara sina shaka nazo zote kwa mujibu wa michango hii michache.
Mafuta -suzuki
Uimara-suzuki
Offroads -suzuki hii ngoma ina difu mbili sio civiljoint ka rav 4
 
Hapo chukua Rav 4, hizo Suzuki escudo ni ngumu kweli ila spear zake no ghari kidogo pia upatikanaji wa spear zake ni shida kidogo maana hizo gari ni za zamani Sana ndio zinaphaze out
Kwa maana ya gharama nakubaliana ila uzamani hata rav 4 model hio ya masawe ni ya zaman pia
 
Mwqka bado ni kipindi kifupi sana kwa kutoa recommendations kuwa gari ni zuri au si zuri..

Ni kawaida sana kuendesha gari mwaka bila kubadilisha spea zaidi ya service za oil na matairi tu.
 
Mwqka bado ni kipindi kifupi sana kwa kutoa recommendations kuwa gari ni zuri au si zuri..

Ni kawaida sana kuendesha gari mwaka bila kubadilisha spea zaidi ya service za oil na matairi tu.
Mzee nipe pia ushauri wako kati ya hizo tatu spacio new, suziki old na Rav4 old kikubwa ni running cost ziwe rafiki kwa mazingira ya mkoani , huwa naona michango yako humu naona uko vizuri kwenye haya mambo
 
Kwa mkoani chukua RAV4 kwa sababu huko spea za Suzuki ni mtihani!
 
Sijawai kusikia Suzuki Escudo ina kesi za ajabuajabu kama izo gari zingine ulizozitaja.

Kuna msemo usemao "alitumia Babu hadi mjukuu" hii kauli inaihusu Suzuki Escudo.

Piga shimo uwezavyo wala habari haina ndo kwanza nati na bolt zinajikaza zaidi
Kuna siku nilienda milimani huko upareni. Tukakodi Escudo maana gari tulizokuja nazo sio rafiki sana na mazingira ya kijijini.
Tangu siku hiyo hii gari naipa salute. Ni chuma hasa
 
Mm kwa ushauri wangu hapo inategemea mazingira ya mama lakini kama ni mtu wa shamba tafuta escudo iliyo katika hali nzuri mpelekee huto sikia kelele, lakini kama ni mizunguko midogo midogo ya hapa na pale mpe rav4.
 
Daah! Alafu upate kitu manual gearbox. Unapanda mlima kama unashuka vile
Mambo ya manual forget about it.Tunakoelekea gari zitakuwa full computerized and full automatic na mafundi washauri waende vyuo pia kwa sababu watapata taabu sana.Mkoloni manual hana muda mrefu tena sokoni.Technologia inakua in exponential form!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…