Kuna haja gani ya kujenga sekondari mpya zaidi ya 1000 ilihali za Sasa hazina nyumba za walimu, maabara na mabweni huku wasichana wakipigwa mimba?

Kuna haja gani ya kujenga sekondari mpya zaidi ya 1000 ilihali za Sasa hazina nyumba za walimu, maabara na mabweni huku wasichana wakipigwa mimba?

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Mada hapo juu yaeleweka.

Serikali ya awamu hii imeibua mradi mwingine wa Matrilioni wa ujenzi wa secondary mpya zaidi ya 1056. Katika shule hizi 26 zitakuwa za bweni huku kila mkoa Tanzania bara ikipata shule moja ktk hizo 26. Hapo naipongeza serikali kwa hilo la shule 26.

Shule nyingne zaidi ya 1030 zitakuwa za kutwa na zitajengwa maeneo mbalimbali nchini.

Swali: Kwanini tuhangaike kujenga shule nyingne ilihali secondary za Sasa hazina nyumba za walimu, maabara na mabweni huku wasichana wakipigwa mimba kila siku?
 
Mi naona tofauti na wewe.

Mi naona kuna haja gani ya kuongeza walimu wakati hawa waliopo bado wana changamoto hata ya kipato tu?

Hamna 'fringe benefits' zozote wanazopata?

Tuboreshe kwanza maslai kisha ndio majengo na hatimae waajiri wengine
 
Mi naona tofauti na wewe...
Mkuu watakuja hapa kusema zitaajiri walimu lakini ukweli ni kuwa ni ubabaishaji tu, hizi za Sasa hazina walimu hasa wa sayansi. Pia shule za msingi zina uhaba mkubwa wa walimu. Hakuna awazaye hayo, kila siku kuibua miradi ya Matrilioni na Billions. Nani anaishauri hii serikali?
 
Secondari zote zingeboreshwa kuwa veta, elimu sekondari olevel iunganiswe primary.Wachache ufaulu wa juu waende A level na vyuo. Itaongeza tija nguvu kazi na kupunguza tatizo la ajiri.
 
Secondari zote zingeboreshwa kuwa veta,elimu sekondari olevel iunganiswe primary.
Ni bora wangejenga VETA, shida mkopeshaji kaweka masharti ziboreshe elimu ya secondary hasa kwa watoto wa kike. Sasa kwanini wasijenge mabwei au hostels kwa shule za kata ili kuwapunguzia mimba na kushindwa kuhitimu?
 
Acha wajenge shule za kata sifa yake ni kuwa na walimu 3, mkuu na wataaluma, nyie mnao taka mwalimu 1 wanafunzi 3 nendeni USA.

Hii ni awamu ya miundo mbinu tuuu subilieni mitano ipite na ile ya offa ndo ije awamu ya 7 ya ajira sasa.
 
Mada hapo juu yaeleweka.

Serikali ya awamu hii imeibua mradi mwingine wa Matrilioni wa ujenzi wa secondary mpya zaidi ya 1056. Katika shule hizi 26 zitakuwa za bweni huku kila mkoa Tanzania bara ikipata shule moja ktk hizo 26. Hapo naipongeza serikali kwa hilo la shule 26....
Tuacheni tufanye siasa jamani, tuko bizeee
 
Secondari zote zingeboreshwa kuwa veta,elimu sekondari olevel iunganiswe primary.Wachache ufaulu wa juu waende A level na vyuo.Itaongeza tija nguvu kazi na kupunguza tatizo la ajiri.
Hili tunashauri sana

Chuo cha Veta kimoja kilichokamilika ni bora zaidi kuliko shule za Sekondari 100

Serikali inaweza kufanya vizuri endapo itatengeneza Vyuo vya Veta badala hata ya hizo sekondari 1000
 
Hili tunashauri sana

Chuo cha Veta kimoja kilichokamilika ni bora zaidi kuliko shule za Sekondari 100

Serikali inaweza kufanya vizuri endapo itatengeneza Vyuo vya Veta badala hata ya hizo sekondari 1000
Mkuu nadhani hizi hela za mkopo wa World Bank zina masharti. Wameambiwa waboreshe elimu ya secondary hasa kwa wasichana, wao wamekimbilia kujenga shule mpya ili wale 10 percent kupitia ujenzi.
 
Swali: Kwanini tuhangaike kujenga shule nyingne ilihali secondary za Sasa hazina nyumba za walimu, maabara na mabweni huku wasichana wakipigwa mimba kila siku
Hizo shule 1056 zitakuwa za kisasa full package Zina kila kitu,acha kukariri maisha
 
Kwahiyo itakuwa kila kijiji badala ya kila kata au kata moja itakuwa na shule 2
 
Asante sana kwa kuileta mada hii hapa.

Kuna umuhimu wa Serikali ku-review au kupitia tena mfumo wa elimu wa nchi hii, tena Serikali ilichukulie jambo hili seriously kabisa!

Kuendelea kujenga madarasa kila kukicha kakutasaidia kuboresha elimu katika Taifa hili la Tanzania. Najua Serikali imefanya mambo mazuri sana kwenye sector ya elimu. Bila kuupitia upya mfumo wa elimu tutajikuta tunamaliza viwanja vyooote kwa kujenga madarasa na bado tusifanikiwe.

Prof. Ndalichako ajaribu kubuni mbinu iliyosahihi ya kuboresha elimu ya Taifa hili badala ya kuendelea kukimbizana na ujenzi wa madarasa.

Ukiwa tayali kupata ushauli tutakupatia.
 
Na wakati huo walimu wapo hoiiii maslahi yao duniiiii
 
Tusipinge kila kitu.

Ujenzi wa shule mpya kuna saidia kupunguza changamoto hasa katika maeneo ambayo watoto wanalazimika kutembea umbali mrefu kuitafuta elimu.
 
[/QUOTE]
Tusipinge kila kitu
Ujenzi wa shule mpya kuna saidia kupunguza changamoto hasa katika maeneo ambayo watoto wanalazimika kutembea umbali mrefu kuitafuta elimu.
Si wangejenga mabweni ktk shule za Sasa kuepuka kutembea huko kwa miguu kuisaka elimu?
 
Ni bora wangejenga VETA, shida mkopeshaji kaweka masharti ziboreshe elimu ya secondary hasa kwa watoto wa kike. Sasa kwanini wasijenge mabwei au hostels kwa shule za kata ili kuwapunguzia mimba na kushindwa kuhitimu?

..aibu nyingine ni kununua midege kwa fedha taslimu toka kwa mabeberu, halafu tunaomba mkopo kwa mabeberu kwa ajili ya ujenzi wa shule.

..kitu kibaya zaidi ni kwamba failure rate ktk shule zilizoko sasa hivi ni kubwa sana. sijui kwanini hatujielekezi kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa ni ya viwango vya kuridhisha, na wanafunzi wanaelewa masomo na kufaulu mitihani.
 
So wangejenga mabweni ktk shule za Sasa kuepuka kutembea huko kwa miguu kuisaka elimu?
Hujui kama idadi ya wanafunzi imeongezeka mara dufu hadi shule zingine zimeelemewa kupokea wanafunzi?
 
Back
Top Bottom