Kuna haja gani ya kujenga sekondari mpya zaidi ya 1000 ilihali za Sasa hazina nyumba za walimu, maabara na mabweni huku wasichana wakipigwa mimba?

Ni bora wangejenga VETA, shida mkopeshaji kaweka masharti ziboreshe elimu ya secondary hasa kwa watoto wa kike. Sasa kwanini wasijenge mabwei au hostels kwa shule za kata ili kuwapunguzia mimba na kushindwa kuhitimu?
Dishi langu lina tabia ya kuyumba hasa kipindi cha mvua. Hivi huu mkakati wa kuboresha watoto wa kike wa kiume wanaachwa utakoma lini?. Hivi kiki kizazi cha kiume tunakipeleka wapi? Ki ukweli huwa naumia sana.
 
Dishi langu lina tabia ya kuyumba hasa kipindi cha mvua. Hivi huu mkakati wa kuboresha watoto wa kike wa kiume wanaachwa utakoma lini?. Hivi kiki kizazi cha kiume tunakipeleka wapi? Ki ukweli huwa naumia sana.
Lengo na chimbuko la Mkopo huu ni kitendo cha Rais Magufuli kuzuia wanafunzi wenye mimba kuendelea na masomo, vinginevyo usingetolewa.
 
Alitakiwa aboreshe hizi za Sasa?
Exactly!!!!!!

Wanaweza;

1. Kuboresha za sasa

2. Kupitia upya system ya utoaji wa elimu inavufanyika sasa hivi

3. Kwa kufanya hivyo inaweza ikatoa picha kwamba inawezekana hata hiyo idadi ya madarasa haitakiwi

4. Je tukija na suala la shift kama wanavyofanya wenzetu jirani what will be the cost implication.

5. Professor Ndalichako anatakiwa atengeneze hadidu za rejea na kuunda kamati ndogo haraka ili ifanye hiyo kazi.

6. Nafikili kwa kufanya hivyo, Ndalichako utakuwa umemsaidia Mh. Rais wetu mpendwa kwenye eneo la elimu.

Tufanye hivyo ili tusiendelee kukimbizana na ujenzi wa madarasa kila kukicha na matokeo yake tukamaliza ardhi yote.

Issue ya shift imewaifanyika miaka ya zamani lakini halikufanikiwa kwasababu lilikosewa mahali fulani na wataalamu hawakuhusishwa ipasavyo.
 
Ni wakati wa serikali kuwekeza katika VYUO BORA VYA ELIMU YA KATI VYA UFUNDI katika kila wilaya. Watoto/vijana wa kitanzania walio wengi wanakosa haki yao ya msingi ya kupata ELIMU/UJUZI/MAARIFA mbalbali kwa ETI kinachoitwa wamefeli kwenda sekondari.

Huko sekondari wanakwenda kufanya nini??? Lazima tufikiri upya na tubadilike kwa kuzingatia mahitaji ya jamii kulingana na wakati tulio nao.
 
Sawasawa
 
Kabisa badala ya kuanza upya...wangejenga mabweni na kuboresha zilizopo ili zichukue wanafunzi wengi...
Si wangejenga mabweni ktk shule za Sasa kuepuka kutembea huko kwa miguu kuisaka elimu?[/QUOTE]
 
So sad.

Hivyo hivyo maisha yenyewe hayaeleweki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…