Kuna haja gani ya kwenda kusikiliza mafunzo ambayo si mageni kwako?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
unaamka asubuhi, unatumia pesa, muda na nguvu kwenda sehemu fulani kusikiliza mtu akikuambia mambo ambayo tayari unajua.Unaenda kanisani, mchungaji anasema tuwe waaminifu, tusameheane, tusiibe, tusizini na tupendane. Unatikisa kichwa kwa nguvu huku ukisema "Amen!" wakati ukweli ni kwamba hayo mambo uliambiwa tangu ukiwa darasa la pili.Unaenda msikitini, Sheikh anasema umuhimu wa ibada, kuheshimu wazazi, kusaidia masikini na kujiepusha na maovu. Unasikiliza kwa makini kana kwamba leo kuna siri mpya itafunguliwa, lakini moyoni unajua kabisa haya mambo umekuwa ukiyasikia miaka yote.

Unaenda semina ya mafanikio. Motivational speaker anasimama na kusema Fanya kazi kwa bidii.Tumia muda vizuri.Kuwa na nidhamu.Usikate tamaa.Na watu wanapiga makofi kwa nguvu mpaka meza zinatikisika. Wengine wanaandika notes haraka sana kana kwamba formula ya kutengeneza dhahabu imetolewa, wakati ukweli ni kwamba hata kabla ya kuingia ukumbini walikuwa wanajua hayo yote.Mikutano ya kisiasa nayo ni burudani nyingine. Mwanasiasa atasema tunahitaji ajira, barabara, maji, umeme na kupambana na rushwa. Umati unapiga makofi. Lakini ukimuuliza mtu mmoja mmoja atakwambia ndiyo, hayo matatizo tunayajua na hayo mahitaji tunayajua pia.
 
Umefikiri vizuri sana .
 
Sasa we mzee unataka sisi tukale wapi?
Wajinga wakiongezeka na mshiko wetu unaongezeka pia.
Halafu unavorudiarudia kumwambia mtu kitu kile kile ndiyo anakielewa kwa ufasaha. Ameeen!
 
Walipoteza muda kwa kakobe, Joshua na sasa kwa mwamposa.
Zipo semina ambazo ukienda unarudi na ujuzi mpya kabisa ambao hukuwa nao.kama za mashamba darasa, mafunzo ya kilimo cha kisasa, ufugaji wa kisasa, matumizi ya mashine, software mpya, teknolojia mpya au mafunzo ya kitaalamu. Huko unaweza kuoneshwa kitu kwa vitendo ambacho hukuwahi kukijua. Unaondoka na maarifa mapya kabisa.
 
Umefikiri vizuri sana .
semina nyingi za maneno ndio huwa zinanifanya nicheke.Mara zuchu imbeja Masterclass..mara kikao cha wanaume.Mara mtu maarufu anaitisha darasa la kutoa madini.Ukienda unakuta mada ni Kuwa na nidhamu.Fanya kazi kwa bidii.Kuwa tofauti ....Usikate tamaa.hahaha mtoa mada ndiye anaondoka na madini halisi kuliko washiriki. anapata udhamini, followers, matangazo, connection na hela za tiketi.Washiriki wanaondoka na notebook iliyojaa maneno ambayo walikuwa wanayajua..
 
Usiende. Problem solved
nikialikwa kwenye semina za aina hiyo naweza kwenda, nitakuwa nimeenda zaidi kusalimiana na watu au kubadilisha tu mazingira. siwezi kujifanya niko na notebook naandika madin ya amini ndoto yako,jiamini,usikate tamaa hapo nitakuwa najidanganya mwenyewe
 
Makanisani mara nyingi watu wanakwenda ku-socialize tu na si kingine. Na eti wakifa waje wazikwe vizuri kwa kuimbiwa kwaya na kuombewa. Hakuna jipya!

semina nyingi za maneno ndio huwa zinanifanya nicheke.Mara zuchu imbeja Masterclass..mara kikao cha wanaume.Mara mtu maarufu anaitisha darasa la kutoa madini.Ukienda unakuta mada ni Kuwa na nidhamu.Fanya kazi kwa bidii.Kuwa tofauti ....Usikate tamaa.hahaha mtoa mada ndiye anaondoka na madini halisi kuliko washiriki. anapata udhamini, followers, matangazo, connection na hela za tiketi.Washiriki wanaondoka na notebook iliyojaa maneno ambayo walikuwa wanayajua..
Wanafanya upigaji tu hakuna jipya
 
Uzi wa maana kabisa.
Saa nyingine bora hata hao wanao rudia yale ya jana juzi na kadhalika, kuliko wale wanao danganya , unaona kabisa hii ni kamba ila una vumilia tu kwa vile ni kanisani.
Wengine waongea ujinga hadi unatamani ungepewe wewe hilo jukwaa, wengine wanachekesha kisicho chekesha, na watu wanacheeeeka , usipo cheka wewe unaonekana wa ajabu inabidi ucheke tu, wengine hawana uwezo wa kujenga hoja nk nk nk.
 
Unaamka asubuh unajikuta unapumua wakati miaka yote umepumua... Unajiuliza hili mbona nina uzoefu nalo?😀

Tubadilishiwe maisha tupewe mapya kwakweli
 
Back
Top Bottom