Kuna haja Police General Orders (PGO) ziwekwe hadharani kwa matumizi ya umma

Kuna haja Police General Orders (PGO) ziwekwe hadharani kwa matumizi ya umma

Kwani hakuna hatua za kisheria zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya polisi wanaokiuka maadili ya kazi zao?
Zipo kinadharia ila kiuhalisia hazipo hasa linapokuja suala dhidi ya CCM.

CCM mara nyingi ni kama vile kupingana nayo ni kupingana na Polisi.

Ukipigwa na CCM utakamatwa na Polisi na ukiwapiga CCM pia utakamatwa na Polisi.
 
wabongo wanaoshabikia siasa hawapendi kusoma. Labda ziwekwe kwa nyimbo za Bongo Flavour au waact movie ya Police order iwe inarudiwa kama isidingo.
 
Zipo kinadharia ila kiuhalisia hazipo hasa linapokuja suala dhidi ya CCM.

CCM mara nyingi ni kama vile kupingana nayo ni kupingana na Polisi.

Ukipigwa na CCM utakamatwa na Polisi na ukiwapiga CCM pia utakamatwa na Polisi.
Hii ni hatari kwa ustawi wa utawala wa Sheria. Hivyo katiba mpya ni muhimu ili pia Police force ifanyiwe reforms!
 
PGO inaelekeza kwamba Polisi wanaruhusiwa kuja kukukamata nyumbani kuanzia saa 12 Asubuhi mpaka Saa 12 Jioni nje ya hapo hawaruhusiwi unless labda Kesi nzito na si hizi ambazo unaweza hata kupigiwa simu na kwenda mwenyewe ,utakuta una kesi ya Cyber lakini unakuja kutekwa nyumbani....Mwabukusi nilimsikia akieleza Wasafi FM kupitia section 4.

Polisi akija kukukamata kwanza lazima atoa arrest warrant na pili lazima aje na mtendaji wa serikali ya mtaa.

Polisi akija kukukamata lazima kwanza ajitambulishe na ikibidi atoe kitambulisho ,asipofanya hivyo una haki ya kuresist maana hapo atakuwa hana tofauti na "JAMBAZI" au "MWIZI".

Tatu una haki ya kuomba uwasiliane na mtu wako au mwanasheria kwa kutoa taarifa kwamba kuna mtu flani kaja antaka kunichukua naomba uje tuongozane naye.

NNe ,Polisi inabidi akutajie kosa ambalo unatuhumiwa nalo.

My Take: Hapa kuna issue ya polisi kusingizia kwamba ulikuwa unazuia wao kutekeleza majukumuj yao ,kwahiyo mtuhumiwa hapa inabidi uwe makini hautakiwi kumgusa askari kwa mikono hata kidogo ,wewe ni kumueleza tu huku ukiwa mbali naye naomba arrest warrant,knionyeshe kitambulisho chako wewe ni nani unatoka kituo gani na na tuhumiwa kwa kosa gani ,hakikisha aje na mjumbe/mtendaji wa mtaa wenu.
 
Back
Top Bottom