Kuna haja SIDO na karakana za Engineering kupewa semina ili wawe na bei rafiki katika uhunzi wao

Kuna haja SIDO na karakana za Engineering kupewa semina ili wawe na bei rafiki katika uhunzi wao

Kiukweli gharama za uendeshaji hasa kupata raw materials ni pasua kichwa ndani ya bongo. Kwa mfano mimi nilijipinda kufungua kiwanda kidogo cha ushonaji ila nikakwama vibaya kupata fabrics. Nakumbuka bei za vitambaa Sunflag ilikuwa sio poa... yaani ukipiga hesabu unaona bora uagize tu nguo China kuliko kushona mwenyewe. Ilibidi niuze mashine zote. Huenda pia SIDO wanapata wakati mgumu kupata materials. Ila kwa ubora naweza thibitisha mashine za SIDO ziko poa kabisa.
Kwahiyo changamoto ni raw material wala siyo bei?

Lakini wakati mwingine ishu ya material ndiyo kichaka cha kujifichia!

Nenda kaulizie gharama ya geti pale SIDO watakupatia gharama kubwa sana!
Lakini ukinunua material mwenyewe ukaita fundi mtaani ukaunda geti lilelile utaona bei inapungua karibia nusu ya bei ya SIDO!

Hauoni kwamba wakati mwingi ishu ya material inatumika kama kichaka?
 
Uko sahihi ila SIDO wanaunda mashine zenye ubora kuliko China. Mimi nilinunua mashine ya screen printing ilikuwa poa sana. Hata mimi naunga mkono kuwa washauriwe kuhusu biashara kwa sababu inaonekana wao akili yao kubwa ipo kwenye ufundi wao ila biashara hawako poa.
Umesomeka vyema
 
Bei zao nyingi katika uhunzi wa vipuri siyo rafiki kabisa kwa mtanzania ukilinganisha na bidhaa ileile ukiiagiza kutoka kiwandani inje ya nchi.
Hata ukiamua kununua material mwenyewe unagundua kabisa kuna unafuu ukilinganisha na wao.

Kichaka wanachotumia kujifichia ni raw material's lakini ukitazama kwa kina wakati mwingine si kweli! Maana hata fanicha za mbao za kutoka misitu ya hapahapa kwetu ukitaka mlango, kitanda au kabati unaweza kushangaa sana ukubwa wa bei unadababishwa na nini.

Milango ya bati ya kichina ilipotambulishwa hapa nchini na wachina waliuza bei rafiki!
1741762077789.png
 
Mafundi wengi kwenye bei huwa na mpigo mkubwa sio poa, ukiuliza tu ka mara ya kwanza unakimbia.

Nadhani pia mzunguko wa hizo bidhaa ni changamoto, hawana soko la uhakika la bidhaa zao. Akipiga mahindo mmoja walau umsave mpaka aje kuuza tena miezi miwili baadae.
 
Kwahiyo changamoto ni raw material wala siyo bei?

Lakini wakati mwingine ishu ya material ndiyo kichaka cha kujifichia!

Nenda kaulizie gharama ya geti pale SIDO watakupatia gharama kubwa sana!
Lakini ukinunua material mwenyewe ukaita fundi mtaani ukaunda geti lilelile utaona bei inapungua karibia nusu ya bei ya SIDO!

Hauoni kwamba wakati mwingi ishu ya material inatumika kama kichaka?
Sijakataa wapo wanatumia kama kichaka ila mimi nimeelezea kwa uzoefu wangu mwenyewe. Raw materials ni changamoto.
 
Mafundi wengi kwenye bei huwa na mpigo mkubwa sio poa, ukiuliza tu ka mara ya kwanza unakimbia.

Nadhani pia mzunguko wa hizo bidhaa ni changamoto, hawana soko la uhakika la bidhaa zao. Akipiga mahindo mmoja walau umsave mpaka aje kuuza tena miezi miwili baadae.
Wakipunguza bei wateja watakuja wengi
 
Back
Top Bottom