Kuna haja SIDO na karakana za Engineering kupewa semina ili wawe na bei rafiki katika uhunzi wao

Kwahiyo changamoto ni raw material wala siyo bei?

Lakini wakati mwingine ishu ya material ndiyo kichaka cha kujifichia!

Nenda kaulizie gharama ya geti pale SIDO watakupatia gharama kubwa sana!
Lakini ukinunua material mwenyewe ukaita fundi mtaani ukaunda geti lilelile utaona bei inapungua karibia nusu ya bei ya SIDO!

Hauoni kwamba wakati mwingi ishu ya material inatumika kama kichaka?
 
Umesomeka vyema
 
 
Mafundi wengi kwenye bei huwa na mpigo mkubwa sio poa, ukiuliza tu ka mara ya kwanza unakimbia.

Nadhani pia mzunguko wa hizo bidhaa ni changamoto, hawana soko la uhakika la bidhaa zao. Akipiga mahindo mmoja walau umsave mpaka aje kuuza tena miezi miwili baadae.
 
Sijakataa wapo wanatumia kama kichaka ila mimi nimeelezea kwa uzoefu wangu mwenyewe. Raw materials ni changamoto.
 
Wakipunguza bei wateja watakuja wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…