Kuna haja wakongwe hawa katika siasa za Tanzania kuachia ngazi au kutumikia nafasi nyingine, la sivyo Gen Z wa taasisi zao watawaondoa kwa fedheha

Kuna haja wakongwe hawa katika siasa za Tanzania kuachia ngazi au kutumikia nafasi nyingine, la sivyo Gen Z wa taasisi zao watawaondoa kwa fedheha

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Nyakati na zama mpya zina wakataa, fikra, maoni na mitazamo mipya ya urika, mvuto na ushawishi zinawapushi kwa nguvu sana kuwabandua nje ya mfumo.

Kiufupi mfumo na nyakati vimewatupa mkono. Hakuna haja ya kusubiri fedheha. ni muhimu kujifunza kusoma alama za nyakati na kuvhukua hatua, kabla mambo hayaja waendea kombo. Hakuna sababu hata moja kung'ag'ana unapokataliwa na nature yaani mindset na generations.

Mmejenga heshima zenu binafsi na taasisi mnazoziongoza kwa weledi na kwa kujitolea sana, kwa hali na mali bila kuchoka kwa mafanikio makubwa sana. Kaeni pembeni, pumzikeni sasa inatosha, nawashauri, ng'atukeni kwa hiyari na heshima, muda si rafiki tena kwenu.

Kwa mfano na kwa uchache sana, hapa naongea na mwenyekiti taifa wa chama cha wananchi CUF, Mwenyekiti taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mwenyekiti Taifa wa United Democratic Party UDP na wengineo ambao wamekua vinara wa vyama vyao kwa miongo zaidi ya mi2 au zaidi. hilo halina afya wala usalama kwenu tena.

Katika hali ya kawaida kiongozi wa aina hii hawezi tena kua na nia, dhamira, mtazamo, maono, ama fikra mpya kabisa, zinazoendana na wakati na mahitaji ya generations mpya.

Hali hiyo ya kung'ag'ana muda mrefu uongozini, hujenga mazoea ambayo mtu anaweza kuona na kudhani taasisi ile ni kama mali yake na familia yake, kumbe ni mali ya wanachama na umma wa Watanzania.

Na matokeo yake, viongozi hawa wakongwe hujikuta wanaondolewa kwa nguvu na fedheha kwa hasira za generations na wasiwe na mtetezi wala la kufanya, kwasabb mfumo na wanachama unawakataa katu katu, kwasabubu wakati na muda wa fikra zao vimewatupa mkono.

Ni vizuri wakasoma alama za nyakati mapema kabla mambo hayajaenda kombo. nashauri , hakima na busara zao, ziwaelekeze kuachia ngazi kwa hiyari na heshima, ili historia iendelee kuwakumbuka kwa mazuri yao na kujifunza yaliyo mema kutoka kwao 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
GEN Z wa nchi ipi? Labda tuwakodi toka nje ya nchi maana hawa wa Tanganyika ni mdebwedo sana bora hata GEN Z wa nchi ya Zanzibar ni wakakamavu.
 
Back
Top Bottom