MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Wakuu kwa hali ilivyo naona kabisa Burundi ni taifa lililofeli kabisa kiuchumi. Ndani ya wiki hizi 2 nimeona raia wa Burundi wakifukuzwa nchini Kenya, Tanzania na Zambia kwa mamia. Yaani jamaa hawatakiwi. Kwa mfano juzi Zambia imewarudisha makwao wahamiaji haramu 143 ambapo waburundi ni 133, wanyarwanda 7 na watanzania 3. Na katika hao watanzania wawili ndo wana makosa ya kiuhamiaji na mmoja amemaliza kutumikia kifungo baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha madawa ya kulevya.
Kwa uzoefu wangu kwenye hizi nchi zetu kuna wahamiaji wengi wasio na documents. Wanaoishi kinyume na sheria. Ila kwa sasa ni kama nchi zote zimeweka macho kwa waburundi. Huenda vyombo vya usalama vinajua kwanini focus ipo wa waburundi zaidi ila ninasihi hizi nchi zisaidie hawa majirani zetu kwa wanachopitia kwa namna itakayowezekana.