Niliangalia matamasha ya Simba day na Yanga day ya mwaka huu nikaendelea kushuhudia kitu ambacho nilidhani hakikupaswa kufanyika kutokana na ukubwa wa vilabu hivi kwa sasa na umaarufu wa matamasha haya kwa sasa barani afrika na duniani kwa ujumla.
Msanii kiongozi kwenye tamasha la simba day bwana Mbosso aliifanya kazi yake ya usanii, yaani kuburudisha waliokuwa wakimwangalia na kwa hakika alifanikiwa.
Waliokuwa uwanjani na walioangalia tamasha la simba kwenye tv lengo lao kubwa lilikuwa ni burudani, waliipata kutoka kwa mburudishaji aliyejiandaa kuburudisha.
Kitu hicho kilikuwa tofauti upande wa yanga, karibia wasanii wote waliotumbuiza walilenga kutoa "burudani" kwa watazamaji sio kwa kutumia burudani asilia iliyowafanya waalikwe pale (usanii wao wa kuimba) bali walitoa burudani kwa kutumia vijembe (naamini akina meja na voisi sio wasanii wa vijembe).
Hoja yangu ndio inaanzia hapo. Kwakuwa kwa thamani yanga ni ya pili barani afrika baada ya al ahly (kwa mujibu wao yanga), nilidhani hata tamasha lao wataliendesha kwa kujikita katika kuelimisha, kuburudisha na kutoa taarifa za klabu yao kwa wapenzi wao badala ya kujikita kupiga vijembe na kujikuta wakiitaja timu nyingime mara nyingi kuliko timu yao.
Fikiria ni mara ngapi neno "Yanga" lilitajwa kwenye Simba day na mara ngapi neno "Simba" lilitajwa kwenye Yanga day. Ukipata majibu ya hoja hii kuna kitu utajifunza kuwa bado timu hizi zinaendeshwa kiujanja ujanja na kiswahili swahili kama vile ni amacha wakati zilishaingia kwenye professionalism.
Hitimisho
Kuna haja ya viongozi wa timu hizi kubadili mentality zao juu ya uendeahaji wa timu hizi kutoka amacha kwenda professional. Hii ni kwa sababu kwa sasa hizi timu zimekua na zinatambulika vizuri sana kimataifa kiasi kwamba kwa kuziendesha kiswahili swahili kama amacha wanazishushia hadhi na kuwapa fursa wapinzani wa kimataifa kuzidharau na kuzifanyia chochote bila woga pale wanapokutana nazo kwani wanajua "hawa hawana lolote zaidi ya uswahili wao".
"Tulibhalegha"