Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 9,016
- 24,650
Kuna sumu kali sana baina ya mwanamke na mwanamme kwenye jamii ambayo inahitajika kuondolewa kwa faida ya vizazi vijavyo.
Angalia matukio ya kikatili yanayofanyika. Kule Mwanza jamaa kampiga risasi mke wake wanaume wanatetea uenda mwanamke hakuwa mwaminifu kwenye ndoa kule Dar dada kachoma moto nyumba mumewe akiwa ndani wanawake wanatetea kwamba kufika maamuzi hayo uenda kuna mabaya mengi alikua anafanyiwa na mumewe ndio uvumilivu umemshinda, yaani watu hawatoi mawazo kwa kuangalia uhalisia wa kitendo kilichofanyika wanatoa mawazo kwa kutetea jinsia zao.
Mwanamke anaona mabaya yanayomkuta mwanaume ni sawa tu, mwanaume anaona mabaya yanayomkuta mwanamke ni sawa tu. Kila jinsia inaishi na kinyongo kwa mwenzake. Je tumefikaje hapa? Machache ya kuzingatia ambayo binafsi naamini yanaweza kumaliza tatizo.
Kwanza, mafundisho ya jando na unyago yarudishwe. Mamlaka husika ziwe zinachungulia tu yanayoendelea uko kusiwe na vitendo vibaya mfano ukeketaji wa wanawake.
Jamii ya leo wanawake na wanaume tunakutana ukubwani tukiwa hatujapitia haya mafundisho kwaiyo kila mmoja hajui saikolojia na hulka ya jinsia nyingine wala hana muongozo wowote uenda hapo ndo tatizo linapoanzia.
Pili, movements na speechs zote zinazowahusu wanawake mfano gender equality, women empowerment n.k zipitiwe upya kama sio kupigwa marufuku kabisa, wanawake wanaoendesha hizi movements kwa kujua hama kwa kutokujua wanachokifanya sio kutetea haki sawa bali ni kupandikiza wanawake wenzao kiburi, jeuri, ubaguzi na chuki kwa mwanaume.
Tatu, maudhui ya vipindi vinavyooneshwa kwenye tv yapitiwe upya, maudhui mengi hayana afya kwa makuzi na maadili ya familia. Na watoto wa kike wamekua wahanga wakubwa maana ndio wanaoshinda na tv siku nzima.
Directors na hosts wa hizi tamthiliya na vipindi mfano wanawake live ya joyce kiria kwa kujua hama kutokujua wanatekeleza ajenda za mabeberu zenye lengo la kualibu kizazi kijacho cha taifa kuanzia kwenye ngazi ya familia ambayo ndio msingi wa taifa zima.
Nne, tatizo la ajira kwa vijana litafutiwe ufumbuzi wa haraka, ikiwezekana iundwe kamati ya vichwa smart ifanye research ije na mpango wa nini cha kufanya. Vijana wa kiume hawawezi kuoa kwa sababu hawana ajira wamebaki kuchezea tu mabinti wa watu.
Watoto wa kike ambao wanatoka kwenye familia zisizo na uwezo wanaamua kujihusisha na ukahaba na udangaji.
Mwanamke ukijisahau unajazwa mimba unakimbiwa mwanaume ukijisahau unapigwa pesa unakimbiwa matokeo yake victims wanabaki na chuki kwa jinsia nyingine kwaiyo wakipata nafasi na wao wanalipiza kisasi kwa mwingine na cycle iyo inaendelea. Hit and run ndo maisha ya vijana kwa sasa.
Hayo ni mawazo yangu kwa uchache tu wabobezi wa masuala ya ustawi wa jamii watakua na mengi zaidi ya kuyaangalia. Ubaguzi na chuki ya kijinsia ni tatizo ambalo linakua kwa kasi mamlaka husika zinapaswa kuliangalia kwa jicho la tatu.